Tukio gani la kuchepuka lilikufanya upoteze imani kwenye taasisi ya ndoa?

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Mjomba alifia gesti Dodoma akiwa na mchepuko ambaye ni mwanafunzi wa chuo. Huyu baba alikua mtu maarufu kwenye siasa na alivyofariki, ilitangazwa kwamba alifia njiani wakati akikimbizwa hospitali kwa mshtuko wa moyo. Ukweli ni kwamba alifia lodge, msichana aliyekua naye akampigia simu uncle wetu mkubwa wakaja wakamtoa lodge haraka kwa kisingizio amezimia na wanamuwahisha hospitali. Uncle alikua ametoka kuoa miezi kadhaa tu kabla hili tukio lililosababisha umauti wake kutokea.

Kushuhudia hilo jambo ndani ya familia na namna lilivyotokea hasa hasa fact ya kwamba baadhi ya ndugu ambao nao wako kwenye ndoa walikua wanajua uncle ana mchepuko, iliniwia ugumu sana kuamini kwamba uaminifu ndani ya taasisi ya ndoa bado upo.

Mliopo single, timu kataa ndoa au wenye mahusiano, njooni mtushirikishe na nyie mliyojionea.

 
Niko siti ya mbele
 

Attachments

  • Screenshot_20250215_191903.jpg
    140 KB · Views: 3
Unaonekana mdau dizain umetokana na kizazi flani chenye maadili amazing sana maana kwenu even you kwenye maisha yako na umri wako huu unaoweza bado ku-type mitandaoni umesha-experience kila baya lihusulo muunganiko wa jamii.

Sometimes hudhani ni kama unatunga kuchangamsha genge
 
Ni kweli nimeshaona mengi, mengine nikiandika humu hakuna mtu atakayeamini.
Nakua interested kushare ili pia nisikie ya wengine nao wameona nini kwenye maisha.
Why nitunge story, inanisaidia nini sasa?
 
Niliona message ya Mke akimwamwambia mchepuko wake hana hamu na mume wake wakifanya anaona kama anambaka na inabidi awaze yupo na mchepuko wake ili stimu zipande. Vijana kagueni simu za wake zenu muondoe kupe mapema kabla haijamia moyoni.

Nyingine nilidate na mke wa mtu unknowingly...yule mwanmke nilipogundua ni mke wa mtu nikamuuliza kwann unacheat akaniambia yangu inafit vizuri kwake ya mumewe ina pwaya nikagundua shida jamaa alioa mwanamke ambae alishaonja tofauti tofauti...haridhishwi nae. Nilisitisha yale mahusiano baada ya kumla mara mbili.
 
Mimi nilikuwa na mahusiano na binti mmoja lakini bahati dini zilikuwa tofauti baada ya miaka kadhaa ya kudate naye.....kwao akatokea mchumba akamuoa lakini.... aliniambia kuwa pamoja kuwa nimeolewa lakini huu UCHI ni mali yako......na mtoto wa kwanza nitazaa na wewe......

Yale maneno yalinitafakarisha sana kuhusu ndoa....nilimuonea huruma sana mwanaume mwenzangu....yule mwanamke kila akinitafuta namzungusha tu....mpaka akakata tamaa akanipotezea.....
 
Nilikuwa na rafiki yangu tulieshibana sana na alinifaa Sana kwenye shida na raha......siku moja alipata changamoto ya kiafya akalazimika kulazwa karibia wiki mbili......mke wake ambaye ni shemeji yangu akaanza kunionyeshea kama dalili kunihitaji kimapenzi....nilijifanya nampotezea mpaka mwenyewe akaniambia live....nilishtuka sana baada ya hapo nikamtazama Shem kwa jicho la tofauti sana......

Lile jambo baina yangu mimi na yeye lilishindikana....lakini baadae alikuja kufumaniwa na mumewe akifanya mapenzi na mwanaume mwingine ndani kwake...... alikuja kujionea baada ya masiku mengi ya kupokea taarifa kutoka kwa waungwana kuwa mkeo si mtulivu......
 
niliombwa nauli na mke wa mtu kwa madai mme wake anamzingua nikampa ahadi ya kumpa mwisho wa mwezi

kabla sijampa akakosana na shoga ake ndio ananisanua kwamba ile fedha ya nauli aliyo niomba ni kweli anataka arudi kwao ila lengo n kuachana na mme wake maana kapata bwana mpya anataka kumuoa ko kamwambia arudi kwao kwanza

yule mke wa mtu alipo kumbushia hilo suala nili m~mind hadi kesho hana stori na mimi
 
Ahahahhahaha
 
Niliwahi kupanga nyumba moja maeneo ya magomeni miaka kadhaa nyuma......yule Baba mwenye nyumba sikujua shughuli zake lakini alikuwa adimu sana......nadhani alikuwa mtu wa safari sana.....ni mbaba tu wa makamo kwa wakati ule.......

Yule alikuwa kila mume wake akitoka kisafari alikuwa anaingiza wanaume tofauti tofauti nyumbani kwake.....na hao wanaume walikuwa huru utasema wao ndio wenye nyumba....

Kilichokuwa kinanishangaza mpaka watoto walikuwa wanaona lakini hawakuonekana kukerwa wala kushtushwa na hali ile.....dah! Lile jambo lilishangaza sana
 
Daah, huyo mke wa mtu aliyekuficha ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…