Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,345
- 3,503
Mjomba alifia gesti Dodoma akiwa na mchepuko ambaye ni mwanafunzi wa chuo. Huyu baba alikua mtu maarufu kwenye siasa na alivyofariki, ilitangazwa kwamba alifia njiani wakati akikimbizwa hospitali kwa mshtuko wa moyo. Ukweli ni kwamba alifia lodge, msichana aliyekua naye akampigia simu uncle wetu mkubwa wakaja wakamtoa lodge haraka kwa kisingizio amezimia na wanamuwahisha hospitali. Uncle alikua ametoka kuoa miezi kadhaa tu kabla hili tukio lililosababisha umauti wake kutokea.
Kushuhudia hilo jambo ndani ya familia na namna lilivyotokea hasa hasa fact ya kwamba baadhi ya ndugu ambao nao wako kwenye ndoa walikua wanajua uncle ana mchepuko, iliniwia ugumu sana kuamini kwamba uaminifu ndani ya taasisi ya ndoa bado upo.
Mliopo single, timu kataa ndoa au wenye mahusiano, njooni mtushirikishe na nyie mliyojionea.