Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 9,830
- 20,686
Sasa hapa Mungu ana Thibitishika vipi yupo tofauti na mawazo yako tu ya kufikirika?Linathibitisha kwasababu nilimuomba yeye, Kama walifanya standardization Basi Mungu alinijibu kupitia wao ili ipatikane sababu.
That's Why Hatukufaulu wote Kama itakuwa walifanya standardization So, in anyway bado inarudi palepale Mungu alinijibu.
Anything else??
Hapa ni open forum.huoni ata aibu kila mtu anakupuuzia unataka ya kubishana uwepo wa Mungu. soma heading hapa hapakuhusu. nenda kwenye mada yenye mabishano juu ya uwepo wa Mungu.
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na kifo?Mungu huyohuyo ndio anachukua roho za watu mkuu, Sasa watu watakufa bila sababu?
Hau hautaki watu wafe ?
Tukio la watu kufa na wengine kupona kwenye ajali ya ndege linathibitisha uwepo wa Mungu kwasababu zote ni kazi zake yaani anaweza kuokoa na kuangamiza at the same time ndio maana akaitwa Mungu Muweza yote huoni hapo kaweza yote? kaokoa na kaangamiza at once.
Mleta mada ana unganisha hoja mbili tofauti zisizo na uhusiano wowote ule kupata hitimisho potofu.Ngoja nikuulize swali: Je, mwanafunzi aliyefanya mtihani wa kidato cha sita akiwa na mategemeo ya kupata division 1 lakini matokeo yalipotoka hakuamini akajikuata amepata division 4 atasemeja? Atasema hilo tukio linaonyesha ''kweli Mungu hayupo''? Ninachotaka kuku-challenge ni kuwa kupasi kwako hakuonyeshi kweli Mungu yupo kwani kuna wengi walidhani watapasi lakini wakafeli. Na wewe ungepata div 4 ulivyotegemea ina maana usingeamini kuwa Mungu yupo? Kwa nini unadhani matukio mazuri tu yanayotokea kwako ndiyo huonyesha Mungu yupo?
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, Ukweli hauendani na imani.Kwa bahati mbaya sana sources ambazo zinatoa uthibitisho wa uwepo wa Mungu Zina rely kwenye imani, Sasa labda uniambie wewe ni imani gani mkuu?.ili nikupe reference za kuendana na imani yako
Mungu yupo kwa kweli. Mimi Binafsi nimepitia changamoto Nyingi sana.Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.
Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!
Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.
Vipi wewe kwa upande wako please share experience.
ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, kusingekuwa na ajali yoyote kwa yeyote.Nilishushwa kwenye gari (Prado) kisa nlikataa kukaa siti ya nyuma nikaenda kupanda basi kufika chalinze napata taarifa ile gari (Prado) imepatwa na ajali na wote waliokuwa ndani ya ile gari wamefariki..
Daah asee tangu hapo niliona uwepo wa Mungu kabisa na hakuna wakukuepusha/kukuletea majanga isipokuwa Mungu pekeake.
Umeniuzunisha sana!. Pole sana.Honestly binafsi bado sijamuona.
nimeomba sana katika maisha yangu ila haikusaidia kutatua matatizo yangu. Nilichokuja kugundua Maisha ni effect after effect.
Ukiwa na shida usikimbilie kuomba, shirikisha watu utapata msaada.
kuamini kwamba mungu anasaidia,
for me is just betting.
Kupitia yeye ( Mwenyezi Mungu)Tupe experience yako japo kidogo mkuu
Tulia wewe na ujuaji wakoUmejuaje hilo?
Kufanikiwa kwako kunauhusiano gani na kukufanya ujue Mungu yupo?
Who told you that ukweli hauendani na imani?Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika, Ukweli hauendani na imani.
Ukweli una endana na kujua, uthibitisho (proofs), Evidences, facts na Logic.
Imani inaendana na kutokuwa na uhakika.
Kwa hiyo kusema Mungu yupo kwa imani, ni kwamba huna uhakika wa uwepo wa huyo Mungu ila ni mawazo yako tu, ya kufikirika.
Imaginations just an illusion.
Daah! Mbona unajichanganya sana mkuu, Sasa Mungu akiumba dunia isiyo na mateso, dhambi na machukizo mengine si utasema tena Mungu gani hawezi kuumba mabaya.Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na kifo?
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Uovu wala mabaya?
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na Mateso, dhambi,ukatili, Majanga ya asili kama radi, mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, yanayo ua maelfu ya watu kila mara?
Mungu muweza wa yote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu, Wasioweza kutenda dhambi na uovu wowote ule?
Huyo Mungu anaweza yote kweli?
Kwani na wewe unavyopinga uwepo wa Mungu si ndio imani yako hiyo mkuu!.Hapa ni open forum.
Ukishaweka imani zako hapa jamii forum lazima tuzijadili.
Kama hutaki imani yako ya uwepo wa Mungu ijadiliwe, Basi ni kubaki nayo huko huko.
Usilete imani yako hapa JF
Vipi na wewe sini mawazo yako tu kuona hathibitiki.Sasa hapa Mungu ana Thibitishika vipi yupo tofauti na mawazo yako tu ya kufikirika?
Una unganisha hoja mbili tofauti zisizo na uhusiano kupata hitimisho potofu.
Logical non sequitur.
Mkuu kuna wakati lazima uchangamshe uzi😂😂Noma sana🤣🤣🤣
Kwakuwa amepitia shida hiyo faida anayopata ni kuwa anaweza kuwashauri ndugu zake wakiume wasije fanya ukatili kama huo kwa watoto wa kike au tukio alilofanyiwa likampelekea aingie kwenye harakati za kupinga ukatili kwa watoto na akawa anapinga kwa kumaanisha kweli na akatoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya ukatili, Sio lazima aishie kujinyonga na ikitokea kujinyonga ni funzo kwa jamii tena funzo la wazi kuwa kufanyia ukatili watoto wa kike kunaweza peleka kifo.Dini Imani ni yako na faida yako..., sihitaji kujua Imani yako ili kuongea na wewe mimi ninachoongelea ni ulichoweka hapa hakileti logic / hakina mtiririko..., Katika magical world ambayo lolote linaweza kutokea sio lazima liwepo baya ili upate zuri ? Niambie mtoto wa kike mdogo anayebakwa na kufanyiwa unyama kitu kinachopelekea anakuwa depressed maisha yake yote na mwisho wa siku kujitia kitanzi anapata funzo gani katika maisha yake ya baadae ?
Kweli kabisa kuna watu wanakera,Natamani Jf waweke option ya muanzisha thread kuweza kublock wachangiaji asiowataka katika thread yake. kuna baadhi ya mada huwa zinaanza vizuri, ila bahati mbaya ikiambukizwa virus wa ubishani hufia njiani, na hali hiyo inapunguza wingi/uwanda wa maarifa ambayo yalitegemewa kupatikana.
That is another topic, Na inahitaji uwe na elimu ya thiolojia kujua why religion contradict .kama source zinatokana na imani, kwa nini hizo imani zina "contradict" kuhusu huyo mungu mmoja?
Asante kwa muda wako pia wakichangia.Kwa kweli MUNGU yupo na anatenda miujiza tunashuhudia wasio amini wapate kuamini. Nakumbuka nikiwa darasa tano, siku ya jumamosi tulikuwa tunarudi shuleni kwa ajili ya masomo ya dini kuna mzungu mmoja mwanamke alikuwa a nafundisha watoto masomo ya dini, binafsi nilikuwa napenda sana kujifunza lakini pia kuimba nyimbo za walimu wale wakiongozwa na huyo mama wa kizungu anapiga gitaa vizuri sana. Nikiwa njiani narudi toka mafundishoni kwa wanaofahamu location ya shule ya msingi kimara baruti, kuna short cut moja unapita nyuma ya shule na kutokea kimara mwisho enzi hizo ilikuwa ni mapori mapori tu! Nakumbuka nilikuwa peke yangu najibu rudisha na nyimbo na furaha ya masomo tuliyofundishwa siku hiyo taratibu natembea kurudi zangu nyumbani!!! Ghafla niliona nyoka mkubwa hata alipo tokea sikujua alijiviriga miguuni mwangu, nilibaki natetemeka sana, na kwa ujasiri nilijikuta nasema kimoyo moyo "MUNGU NISAIDIE" nikiwa katika hali ya hofu kubwa yule nyoka alijikunjua na kuondoka kwa kasi kuelekea vichakani. Nilibaki nimesimama pale barabarani kwa muda sikuweza kunyanyua hata mguu kwa haraka mwili wote ulikuwa unatetemeka!! Baada ya muda nilianza kuondoka taratibu nikiwa siamini kabisa kilichotokea. Kumbu kumbu hii hajawai futika kichwani mwangu mpaka Leo. Na kwa mara ya kwanza nashuhudia hapa. Jamani maajabu yapo duniani hapa na Mungu anatenda kweli. Asante mtoa Mada wengi tutaendelea kujifunza kwa mambo halisi yanayotutokea maishani