Mungu yupo kwa kweli. Mimi Binafsi nimepitia changamoto Nyingi sana.
Nakumbuka Mwaka 2015 nikiwa Advance (Form Five PCB) Mubaba Sec Shool - KAGERA nilivunjika Mkono wa Upande wa Kulia ambao do mkono ninaotumiya Kuandikia. Nashukuru Nikafanya NECTA 2017 Nikafaulu kwa DIVISION TWO YA 10. Hadi wa Leo naamini kabisa Mungu Yupo.
Nakumbuka mwaka huo huo 2017 nikaenda BULOMBORA JKT Mujibu wa Sheria OPERATION TANZANIA YA VIWANDA, Nimetoka JKT nina tatizo la Mgongo sababu ya AZABU za JKT. Nimekuja Kupona Mgongo Mwaka Jana 2022. Nikaamini Mungu yupo.
Mwaka 2019 Nikiwa Mwaka wa Pili Chuo Cha RUCU katika Course ya Bachelor's of Computer Science nilitapeliwa Hela yangu Zaidi ya Milioni 3 na MKINGA MMOJA ANAITWA MALANGALILA maeneo ya Mlandege Mwangata _ IRINGA MJINI. (Hiyo Milioni 3 ilipatikana nilikuwaga Nafanya Kazi ya kujitolea katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa IRRH, Ada ya Chuo, na 700,000 ya Mama mmoja ivi Nurse nilimukopanga) nilipoteza kila kitu hata mia sikuwa nayo. Chuo ilibaki Kidogo tu Ni DISCO. Usimuamini mtu, na usitake Maisha ya Haraka. Mungu do hutoa muelekeo wa Maisha ya kila mmoja wetu. Mungu do hufungua riziki ya kila mmoja.
Mwaka 2020 Septemba Mungu akasaidia nika hitimu Degree ya Computer Science pale RUCU, Mungu yupo.
Mwaka huo huo 2020 Octoba kipindi cha Uchanguzi wa Rais. Mungu alinisaidia kupata Kazi katika taasisi ya serikali ambayo ni MAMLAKA YA MAJI SAFI IRINGA ( IRUWASA), nimekaa mtaani Wiki Tatu tu hadi wa Leo nipo Kazini. Namushukuru MUNGU. Mungu Yupo, Mungu Yupo.
Namushukuru Mungu kwa sasa nina Mke wangu wa Kibena, nina Mtoto na Biashara Zangu Safi. NILISHASAHAU KAMA NILITAPELIWA MILIONI 3. MUNGU YUPOOOOOOOOO na ATAENDELEA KUWEPO MILELE.