Tukio gani ulishawahi kufanya ukahakikisha umemfundisha mtu adabu?

Kuna jamaa alikuta nishapark gari, then yeye akaja na gari lake na kulielegesha vibaya nyuma ya gari yangu kiasi cha kuzuia namna ya kuweza kutoka vizuri, walinzi walimuelekeza namna ya kuweka gari lake vizuri lakini akawafokea kwa lugha kali, "nimeacha namba ya simu, nipigieni"...

Sasa baada ya kumaliza shughuli zangu, narudi niondoke nakuta nimekula block na namna ya kutoka ni hadi uchekeche gari kama mara 50, upande mmoja una mfereji ukikosea tu unaingiza gari huko.

Jamaa tukampigia simu akawa anakata, tuma meseji hajibu kama dakika 15 hivi.l, nilipata hasira na roho ya Trump ikaniingia kwa ghafla.

Baadaye nikasema ngoja kwanza nitoke kwa kuchekecha, kwa msaada wa mlinzi nikaweza kutoka hapo ni kuchekecha kwa dakika kama 3.

Baada ya kufanikiwa kutoka, nikachukua jerk na wheel spanner yangu, nikafungua tairi zote za ile gari, hapo pembeni kulikuwa na mawe nikaitega ile gari nikaiacha juu ya mawe, wheel nuts nikamkamkabidhi mlinzi nikamwambia huyu usimpe hizi hadi akuombe msamaha...

Nikasepa zangu sijui hata nini kiliendelea...
 
Kipindi nasoma O level wale wanafunzi waliokua wanasoma darasa la sayansi walikua wanatudharau sana sisi tunaosoma darasa la arts...

Kuna dada mmoja alikua ana akili sana pale sayansi, ni mmoja ya watu waliokua wanaowadharau wanafunzi wale wanaosoma darasa la arts... Yule dada yaani naweza nikapishana nae ananipita kwa dharau, alikua anajiona special sana...

Tulivyomaliza form four nikapata division three, yeye akapata one... Nikachaguliwa kwenda advance kwa sababu combination yangu ili balance, hata hivyo kipindi kile kupata Division three ilikua ni mpaka upambane sana. Yeye pia alichaguliwa shule moja maarufu iliyokuwepo mkoani kwetu...

Kumbuka kipindi hicho miaka ya nyuma ilikua big deal sana kufulu kwenda kidato cha tano. Kwa kipindi hicho unakuta mtaa unaoishi watu ambao wana elimu ya advance level ni mmoja au wawili...

Nimefika zangu advance pale from no where hiyo HGL ninayosoma nakuta tu masomo nayaelewa vizuri tofauti na o level,.. Test na mitihani nafaulu vizuri tu... Nimekuja kufanya Necta form six nikagonga Division one nzuri tu.

Chuo nimefika pale Udsm nilikutana nae yule dada mwenye dharau tunapiga course moja.. Yule dada sikuwahi kumsemesha kwa chochote, tunapishana iwe cafeteria au lecture rooms bila kusemeshana... Hata niwe nae group moja la presentation na-interact nae kama simjui vile, mara nyingine anaweza akaniangalia na mimi nikamwangalia kama hatujawahi kujuana.... Mpaka tunamaliza pale Udsm sijawahi kuongea nae jambo lolote, ni ukauzu mwanzo mwisho a.k.a mikausho mikali.
 
hahahahaha watu wa PCB, PCM, CBG, ngoja waje
 
Mmmh ingetokea umeonana naye hata siku moja kabla hajafa, ungeambiwa umemuua.
Ila huyo mzee msuluhishi yuko sahihi, inabidi kuchunga sana maneno tunayoyasema.
 
Kama bi mkubwa wenu kazeeka hamuhitaji huyo mume. Kwa nini alimkaribisha huyo Mzee hapo kwenu wanalala wote?
 
Ushauri kutoka kwa BOSI wangu ambaye ni kama brother wangu na role model wangu ni huu
KWENYE BIASHARA SIO SEHEMU YA KUMSHIKISHA ADABU MTU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…