Tukitumia mfumo huu, hakika tutamaliza ajali za barabarani kwa Siku moja Tu

Hizo sio adhabu hapo kuna fidia na faini hizo ni haki kwa waathirika wa ajali. Serikali pia ni mwaathirika namba moja wa ajali, abiria pamoja na watembea kwa miguu bila kusahau wamiliki wa vyombo vya usafiri wote ni waathirika wa ajali.
 
Mauchawi
Ajali za mwaka huu zimetisha. December pekee kwa haraka zaidi ya 100 wamekufa kwenye barabara ya Dar-Arsh-Tarakea. Something must be done.
Mauchawi sometimes hawa wanene wana majambo yao dunia ina upande wa pili ambao sio poa
 
Aina za Uwajibikaji
1). Kwa mtu aliye gongwa na chombo
Mwathirika angelipwa fidia kulingana na viwango vilivyoainishwa (vifo, ulemavu wa kudumu, au majeraha).
Mmiliki wa chombo angelipa faini ya TZS milioni 50 kwa kusababisha ajali hiyo.
Hivi unajua kwanini faini huwa ni realistic na sio kuweka namba ambayo haina uhalisia ? Ni kwam,ba ukiweka vitu ambavyo havilipiki basi havitalipwa au watu kuhonga kidogo ili kupindisha haki..., Pia kumbuka haya mambo yanakuwa na Bima kwahio mwisho wa siku mmiliki yupo covered ila ukileta ubanaji mkubwa katika sekta ambayo UMMA umeshindwa kutoa huduma mwisho wa siku hizo sekta zitakufa.....


Sheria zipo na zifuatwe na katika Usafiri wa UMMA tuboreshe usafiri wa (SGR n.k.) wananchi wapate efficient, affordable alternative sio kuwaachia wabangaizaji (for profit) wanagombania abiria wachache sababu majority can not afford to move from A to B hivyo msimu wa sikukuu ndio kinabakia kipindi cha uchumaji cha hawa watu angalau kulipa mikopo yao...
 
Umezungumzia familia ya MTU akiyekufa ilipwe fidia 200-500 Ila Kwa Kwa aliyepata ulemavu alipwe mil 150-200.


Je umefikiria Kwa kina hapo ukipata ulemavu wa kudumu na ukifa wapi unabidi kulipwa fidia kubwa.?
 
Hizo hela zote ulizotaja serikali ilitakiwa izitumie kupanua miundombinu ya barabara na madaraja ili kuwapa wasafiri highway lanes zisizoingiliana. Walau njia 4 ambazo zimetenganishwa na zege katikati. Mbili za kwenda na mbili za kurudi kisha ungeshangaa rate ya ajali ambavyo zingepungua kwa kasi. Maboresho yanahitajika sababau watumiaji barabara wameongezeka ila serikali ime relax na plan zile zile za kikoloni.

Ajali nyingi za kwetu ni za magari kugongana uso kwa uso kutokana na ufinyu wa barabara na muingiliano wa moja kwa moja.
 
Mimi niko pale pale, miundombinu ndio shida. Barabara nyembamba halafu mnapishana bila barrier ndio shida. Mtu ana overtake bila kuona mbele kukitokea kuna gari ghafla kinaumana baaam!!! Head on Head collision. Hii ndio hufanya 90% za ajali.

Hakuna ajali nyingi za mtu kugonga nyuma gari lililoko mbele yake na hata ikitokea impact huwa sio fatal kama ajali za uso kwa uso.

Tizama miaka ya 2000-2015 ajali zilizokuwa zinatokea kipande cha kibaha-ubungo mara basi limegonga na kuua watu, linganisha na hali ya sasa. Yote ni sababu barabara ni pana na imetenganisha watumiaji. Ni nadra sana kusikia ajali sababu nyingi zilikuwa ni head on head collisions.

Jiulize what if Dar-Moshi njia ikawa multi lanes? Wajaribu hilo waone kama watasikia ajali za ajabu ajabu tena. Hakuna cha fine wala fidia suluhisho ni hili.
 
Waasisi wa Tz wamekufa na siri nzito kuhusu hii nchi hususani Ajali za mwisho wa mwaka, mwenge, na watz kuwa na akili fulani hivi iliyolala

Nadhani kuna k2 nyuma ya pazia
 
Huo itakuwa alternate approach but not the precise one.

Ni sawa na shule ikiwa haifaulishi ukaamua kuibomoa badala ya kubadilisha Management na walimu. Au timu ikiwa na wachezaji wabovu kisha wewe unafukuza kocha wa timu ukitegemea mabadiliko badala ya kusajili upya.
 

Ushauri wa kupanua na kuboresha miundombinu ndo suluhisho.

Hiyo mbinu ya kuwakamua watu pesa ni mbinu ya kijima hata Magufuli alijaribu ikamletea matokeo hasi .



Maana kuna ajari ambazo zinatokana na barabara (miundombinu)
 
Mauchawi

Mauchawi sometimes hawa wanene wana majambo yao dunia ina upande wa pili ambao sio poa
Inawezekana pia. Kwenye huo ulimwengu mtu akimzidi mwenzie kete anampuliza chap.
 
Mkuu wewe ndiwe ungetakiwa utuletee uzi maana wazo lako ni bora kuliko la mleta uzi
Tunahitaji teknolojia zaidi ili kumaliza changamoto zetu

Ajali, rushwa, umaskini, magonjwa, na mambo mengine kama hayo tunahitaji teknolojia zaidi hili kukabiliana nayo.
 
Ongeza hizi muhimu.

1. Serikali ijenge miundombinu mbadala ya usafiri wa treni kwenda mikoa yote.
Hili litapunguza wingi wa malori, wingi wa magari ya abiria na wingi wa magari binafsi.

2. Barabara za lami ziwe dual carriage way/divided highway, wanaoelekea upande mmoja wawe na barabara yao na sio hizi za sasa zilizotengwa na mstari kati.
Kwa kuanzia ujenzi ufanywe kwanza maeneo ambayo ni hatarishi. (Kama walivyofanya Inyala Mbeya).

3. Kupunguza manual intervention na kukumbatia teknolojia kwa magari na barabara...
 
highways kama dar iringa
Au dar Ars ziwe double roads, mbona Namibia wameweza?
Hii itakuwa ndio muarobaini.
 
Ajali zinaweza kupunguzwa kwa Polisi kusimamia Sheria na sio kwa utozaji wa viwango.
Tatizo ni rushwa wanazopewa polisi na mahakama.
 
Siku moja nipo safarini kutokea jijini basi nililppapnda lipo mbio mbio kaa kawaida. Tukafika kwenye kona flani hivi kabla ya kuingia mkoa, dereva wa basi akawa anaovateki Lori ghafla yaani ile ghafla tunaona mbele Kuna Lori jingine ikabidi dereva wa basi arudi kushoto ghafla na kujibamiza kwenye kile Lori. Bahati kwa dereva wa basi ni kwamba dereva wa Lori hakuwa Mtanzania hivyo basi likawekwa kwenye namna ambayo walivyo kuja kupima wakasema Lori limegonga basi....DHULMA
Haya mambo yanapimikaje ili aliyesababisha alipe na kweli iwe halali amefanya adhabu?
 
Mapendekezo yako hayana uhalisia na hayatekelezeki!

Je serikali ipate adhabu gani kwa ubovu wa barabara na kujenga barabara zisizo na viwango?
 
Mnajadili ajali, mnalaumu madereva sijui wamiliki mnatoa mapendekezo blablabla... kumbe ni mwisho wa mwaka watu wanafunga hesabu. Wanasiasa wanafungua njia za madaraka mwakani.
 
Ushauri wa kupanua na kuboresha miundombinu ndo suluhisho.

Hiyo mbinu ya kuwakamua watu pesa ni mbinu ya kijima hata Magufuli alijaribu ikamletea matokeo hasi .



Maana kuna ajari ambazo zinatokana na barabara (miundombinu)
Eeh wanafikiri ku impose heavy fines and penalties ndio suluhu. Watazalisha mianya mipya ya rushwa tu. Hamna mtu atafanya ujinga wa kulipa laki na nusu ilihali kuna option ya kuhonga elfu 20 akaenda zake na safari.

Ajali ziko centred kwenye miundombinu mibovu na finyu. Unakwepa shimo ghafla unajikuta umevaana na mwenzio anayekuja usoni mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…