Tukitumia mfumo huu, hakika tutamaliza ajali za barabarani kwa Siku moja Tu

Ajali zinaweza kupunguzwa kwa Polisi kusimamia Sheria na sio kwa utozaji wa viwango.
Tatizo ni rushwa wanazopewa polisi na mahakama.
😁😁😁😁😁😁😁 Polisi kusimamia sheria ni sababu kuna uwezekano wa hongo. Mkitaka sheria zisimamiwe kweli wekeni robots. Zitatutesa mwanzoni ila tutazoea kutii sheria.
 
highways kama dar iringa
Au dar Ars ziwe double roads, mbona Namibia wameweza?
Hii itakuwa ndio muarobaini.
Nashangaa watu wanazunguka zunguka badala ya kuangalia mzizi wa tatizo. Haihitaji kwenda shule kujua kwamba huo unaoitwa uzembe wa madereva unachangiwa zaidi na miundombinu finyu.

Huwezi kufata malori 6 yanayotembea spidi 20kph kwa zaidi ya nusu saa. Lazma utatanua tu. Sasa je endapo zingekuwa barabara 2 au 3 si ungeya overtake kwa usalama tu na kisha ukasonga mbele na speed yako. Hilo haliwezekani kufanyika kistaarabu sababu barabara ni moja. Inabidi usubirie chaki iruhusu ndipo utanue na kusiwe na mwenzio anayekuja kulia kwako.
 
Nadhani pia barabara za njia mbili pia ni suluhisho hasa kwa ajali za uso kwa uso na Overtake
Ajali zetu nyingi ni za uso kwa uso kwenye blindspots au wrong overtaking. Tuna share lanes badala ya kuwa na multiple lanes kila mtu akae upande wake. Unasingiziwa uzembe wa madereva mara sijui polisi wanachukua rushwa.

Barabara finyu hilo ndio tatizo. Itengwe bajeti ya kutanua barabara zote za highways ziwe multiple lanes.
 
Mkuu wewe ndiwe ungetakiwa utuletee uzi maana wazo lako ni bora kuliko la mleta uzi
Tunahitaji teknolojia zaidi ili kumaliza changamoto zetu

Ajali, rushwa, umaskini, magonjwa, na mambo mengine kama hayo tunahitaji teknolojia zaidi hili kukabiliana nayo.
Teknolojia itasaidia kwa 50% tu ila management itatakiwa ijazie 50% iliyobaki.

Kwenye rushwa lazma kuwepo na double standards. Hatuwezi kufika kwa style hio. Hujuma ni nyingi ili teknolojia ifeli.
 
Mapendekezo yako hayana uhalisia na hayatekelezeki!

Je serikali ipate adhabu gani kwa ubovu wa barabara na kujenga barabara zisizo na viwango?
Kupitia whistle-blowers wao ni kwamba barabara ni kitu kisicho na utambuzi so wewe binadamu ambaye ni dereva unatakiwa ndio upate lawama zote ikitokea umepata ajali.
 
Hata wao ni binadamu kwa hiyo kwa kutambua hilo wanapaswa kuhakikisha barabara zinapitika bila taabu! Barabara ni chanzo kikubwa cha ajali!
 
Huo itakuwa alternate approach but not the precise one.

Ni sawa na shule ikiwa haifaulishi ukaamua kuibomoa badala ya kubadilisha Management na walimu. Au timu ikiwa na wachezaji wabovu kisha wewe unafukuza kocha wa timu ukitegemea mabadiliko badala ya kusajili upya.
Kipi kimebomolewa hapo?, approach hiyo haibomoi Barabara pia haiondoa uwepo wa traffic police, ni magnetism (for detections of reckless driving tu, mfumo huo unawekwa kwenye mikanda ya lanes ku-control utumiaji wa Barabara kwa kuzingatia sheria zilizowekwa barabarani kwa michoro. Ulichoweka hapo hakina suluhisho to the current known problem. Hujatoa suggestion of how to solve the known problem, Umeweka mashakaka TU!
 
Solution ni infrastructure, wala huhitaji teknolojia ya gharama sana kwenye miundombinu finyu. Akili hio unayotoa wewe ime base kwenye restrictions badala ya flexibility.

Ndio akili ile ile iliyotumika kujaza matuta na vibao vya 50kph kwenye highway, kujaza askari barabarani ili kuzuia watu wasikimbize magari eti watasababisha ajali.
 
Yangu haijaongelea speed, Wala inflexibility, inaongelea adherence to rules and regulations kwenye risk area, mfano, sehemu hairuhusu kuovertake, jinga Moja lina-overtake, hairuhusu certain speed, some fools wana speed up. Hairuhusu change of lanes. Etc, ajali za kuparamiana (utuamiaji mbaya wa road lanes) na kugongana ndio nyingi Tanzania, Wala sio kuacha njia (Barabara).
 
Habari za jioni ndugu na marafiki,
Poleni sana kwa wote mnao endelea kuathirika na ajali zinazo endelea kutokea barabarani.

Hili jambo limelilazimu kukaa chini namimi nitoe mapendekezo yangu ili tuweze kutokomeza ajali zinazo endelea kumaliza ndugu na marafiki zetu.

Lakini kabla ya yote nimeona kwanza nilete pendekezo hili hapa jukwaani ili tuone jinsi ambavyo linaweza kufaa au kutofaa.

Kwanza kabisa naomba kuwasilisha kwamba ajali za barabarani huwa hazitokei kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya uzembe, kutokufuata sheria, na ukosefu wa tahadhari. Vyombo vya usafiri kama magari, mabasi, bodaboda, bajaji, na malori vinaweza kufananishwa na zana hatari kama visu, mapanga, au bunduki. Vyote vinahitaji uangalifu mkubwa ili visisababishe madhara.

Ili kumaliza ajali hizi, naomba kupendekeza mfumo huu madhubuti wa uwajibikaji unaolenga kuhakikisha kila mmiliki wa chombo cha usafiri anawajibika kwa matendo yake, huku akifuata sheria za usalama kwa umakini wa hali ya juu.

1. Uwajibikaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri
Mmiliki wa chombo cha usafiri alipaswa kubeba jukumu moja kwa moja kwa ajali yoyote inayosababishwa na chombo chake.

Aina za Uwajibikaji
1). Kwa mtu aliye gongwa na chombo
Mwathirika angelipwa fidia kulingana na viwango vilivyoainishwa (vifo, ulemavu wa kudumu, au majeraha).
Mmiliki wa chombo angelipa faini ya TZS milioni 50 kwa kusababisha ajali hiyo.

2). Kwa vyombo vilivyogongana
Kila mmiliki wa chombo angelipa fidia kwa abiria wake.
Kila mmiliki angelipa faini ya TZS milioni 50 kwa kushiriki katika ajali hiyo.

3). Kwa chombo kilichogonga kingine kikiwa kimesimama
Mmiliki wa chombo kilichogonga angelipa fidia kwa abiria wake na kwa mwathirika wa chombo kilichokuwa kimesimama.
Pia atalipa faini ya TZS milioni 50 kwa uzembe wake.

4). Kwa chombo kilichogonga kingine kwa nyuma kikiwa kwenye mwendo
Mmiliki wa chombo kilichogonga angelipa fidia kwa abiria wake na waathirika wa chombo kingine kilichoharibika.
Faini ya TZS milioni 50 ingelipwa na mwenye chombo kilichogonga.

2. Viwango vya Fidia kwa Waathirika wa Ajali

Ninapendekeza viwango vifuatavyo vya fidia

1). Kwa Vifo: Familia ya aliyefariki ingepokea fidia ya TZS milioni 250 hadi 500.

2). Kwa Ulemavu wa Kudumu: Mwathirika angepokea fidia ya TZS milioni 150 hadi 200, kulingana na athari za ulemavu wake kwa maisha ya baadaye.

3). Kwa Majeraha ya Kawaida: Mwathirika angepokea fidia ya TZS milioni 50 hadi 100, kutegemea gharama za matibabu na muda wa kupona.

3. Faini ya Kupata Ajali

Kwa kuwa ajali husababisha madhara makubwa kwa jamii na miundombinu:

Faini ya Lazima: Kila anayepata ajali angelipa TZS milioni 50, bila kujali hali ya ajali (iwe imeua au la, chombo kimeharibika au la).

4. Mfumo wa Bima ya Lazima

Ili kuhakikisha fidia na faini zinalipwa ipasavyo:

1). Kila mmiliki wa chombo angetakiwa kuwa na bima ya dhima kubwa inayoweza kufidia madhara makubwa ya kifedha.

2). Wamiliki wasio na bima inayokidhi viwango wangetozwa faini kubwa au magari yao kufungiwa.

5. Hatua za Nyongeza za Kuzuia Ajali

Ili mfumo huu ufanye kazi kwa ufanisi, hatua zifuatazo zingepaswa kuzingatiwa:

1). Ukaguzi wa Magari: Serikali ingefanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyombo vyote vya usafiri kuhakikisha vinakidhi viwango vya usalama.

2). Elimu ya Usalama Barabarani: Madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wangeelimishwa kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani.

3). Adhabu Kali kwa Wakiukaji: Madereva na wamiliki wanaopatikana na hatia ya uzembe wanhepatiwa adhabu kali kama kufungiwa leseni au kifungo cha muda.

6. Faida za Mfumo Huu

1). Kuongeza Nidhamu na Uwajibikaji:
Wamiliki wa vyombo vya usafiri wangehakikisha vyombo vyao ni salama, na madereva wangekuwa makini zaidi barabarani.

2). Kupunguza Ajali kwa 100%: Kwa gharama kubwa ya fidia na faini, ajali zingepungua kwa kiwango kikubwa.

3). Kuimarisha Usalama wa Jamii: Barabara zingekuwa salama kwa kila mtumiaji wa barabara.

Kwa kutumia mfumo huu, tungepelekea kuondoka kwa uzembe barabarani, huku tukihakikisha kila anayehusika anawajibika kwa matendo yake. Tungeanza kutekeleza mfumo huu, hakika ajali za barabarani zingekuwa historia ndani ya muda mfupi!
Ndg watu wanahukumiwa kunyongwa mpaka kufa na bado wanaua, adhabu haiwezi kuwa suluhisho. Labda ubovu wa miundo mbinu unachangia sana. Barababara kuu km za Mbeya-Dar, Dar-Arusha- Namanga, Morogoro-Mwanza zote hizo na zile za Dar-Lindi-Mtwara, Mtwara Songea, Songea-Njombe-Mbeya zilitakiwa ziwe njia 4 siku nyingi. Huwezi kuta magari yanagongana hovyo maana katikati ya njia 2 2 kuna gema kubwa. Umaskini ni adui mkubwa wa binadamu
 
Yangu haijaongelea speed, Wala inflexibility, inaongelea adherence to rules and regulations kwenye risk area, mfano, sehemu hairuhusu kuovertake, jinga Moja lina-overtake, hairuhusu certain speed, some fools wana speed up. Hairuhusu change of lanes. Etc, ajali za kuparamiana (utuamiaji mbaya wa road lanes) na kugongana ndio nyingi Tanzania, Wala sio kuacha njia (Barabara).
Okay
 
Habari za jioni ndugu na marafiki,
Poleni sana kwa wote mnao endelea kuathirika na ajali zinazo endelea kutokea barabarani.

Hili jambo limelilazimu kukaa chini namimi nitoe mapendekezo yangu ili tuweze kutokomeza ajali zinazo endelea kumaliza ndugu na marafiki zetu.

Lakini kabla ya yote nimeona kwanza nilete pendekezo hili hapa jukwaani ili tuone jinsi ambavyo linaweza kufaa au kutofaa.

Kwanza kabisa naomba kuwasilisha kwamba ajali za barabarani huwa hazitokei kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya uzembe, kutokufuata sheria, na ukosefu wa tahadhari. Vyombo vya usafiri kama magari, mabasi, bodaboda, bajaji, na malori vinaweza kufananishwa na zana hatari kama visu, mapanga, au bunduki. Vyote vinahitaji uangalifu mkubwa ili visisababishe madhara.

Ili kumaliza ajali hizi, naomba kupendekeza mfumo huu madhubuti wa uwajibikaji unaolenga kuhakikisha kila mmiliki wa chombo cha usafiri anawajibika kwa matendo yake, huku akifuata sheria za usalama kwa umakini wa hali ya juu.

1. Uwajibikaji wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri
Mmiliki wa chombo cha usafiri alipaswa kubeba jukumu moja kwa moja kwa ajali yoyote inayosababishwa na chombo chake.

Aina za Uwajibikaji
1). Kwa mtu aliye gongwa na chombo
Mwathirika angelipwa fidia kulingana na viwango vilivyoainishwa (vifo, ulemavu wa kudumu, au majeraha).
Mmiliki wa chombo angelipa faini ya TZS milioni 50 kwa kusababisha ajali hiyo.

2). Kwa vyombo vilivyogongana
Kila mmiliki wa chombo angelipa fidia kwa abiria wake.
Kila mmiliki angelipa faini ya TZS milioni 50 kwa kushiriki katika ajali hiyo.

3). Kwa chombo kilichogonga kingine kikiwa kimesimama
Mmiliki wa chombo kilichogonga angelipa fidia kwa abiria wake na kwa mwathirika wa chombo kilichokuwa kimesimama.
Pia atalipa faini ya TZS milioni 50 kwa uzembe wake.

4). Kwa chombo kilichogonga kingine kwa nyuma kikiwa kwenye mwendo
Mmiliki wa chombo kilichogonga angelipa fidia kwa abiria wake na waathirika wa chombo kingine kilichoharibika.
Faini ya TZS milioni 50 ingelipwa na mwenye chombo kilichogonga.

2. Viwango vya Fidia kwa Waathirika wa Ajali

Ninapendekeza viwango vifuatavyo vya fidia

1). Kwa Vifo: Familia ya aliyefariki ingepokea fidia ya TZS milioni 250 hadi 500.

2). Kwa Ulemavu wa Kudumu: Mwathirika angepokea fidia ya TZS milioni 150 hadi 200, kulingana na athari za ulemavu wake kwa maisha ya baadaye.

3). Kwa Majeraha ya Kawaida: Mwathirika angepokea fidia ya TZS milioni 50 hadi 100, kutegemea gharama za matibabu na muda wa kupona.

3. Faini ya Kupata Ajali

Kwa kuwa ajali husababisha madhara makubwa kwa jamii na miundombinu:

Faini ya Lazima: Kila anayepata ajali angelipa TZS milioni 50, bila kujali hali ya ajali (iwe imeua au la, chombo kimeharibika au la).

4. Mfumo wa Bima ya Lazima

Ili kuhakikisha fidia na faini zinalipwa ipasavyo:

1). Kila mmiliki wa chombo angetakiwa kuwa na bima ya dhima kubwa inayoweza kufidia madhara makubwa ya kifedha.

2). Wamiliki wasio na bima inayokidhi viwango wangetozwa faini kubwa au magari yao kufungiwa.

5. Hatua za Nyongeza za Kuzuia Ajali

Ili mfumo huu ufanye kazi kwa ufanisi, hatua zifuatazo zingepaswa kuzingatiwa:

1). Ukaguzi wa Magari: Serikali ingefanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa vyombo vyote vya usafiri kuhakikisha vinakidhi viwango vya usalama.

2). Elimu ya Usalama Barabarani: Madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri wangeelimishwa kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani.

3). Adhabu Kali kwa Wakiukaji: Madereva na wamiliki wanaopatikana na hatia ya uzembe wanhepatiwa adhabu kali kama kufungiwa leseni au kifungo cha muda.

6. Faida za Mfumo Huu

1). Kuongeza Nidhamu na Uwajibikaji:
Wamiliki wa vyombo vya usafiri wangehakikisha vyombo vyao ni salama, na madereva wangekuwa makini zaidi barabarani.

2). Kupunguza Ajali kwa 100%: Kwa gharama kubwa ya fidia na faini, ajali zingepungua kwa kiwango kikubwa.

3). Kuimarisha Usalama wa Jamii: Barabara zingekuwa salama kwa kila mtumiaji wa barabara.

Kwa kutumia mfumo huu, tungepelekea kuondoka kwa uzembe barabarani, huku tukihakikisha kila anayehusika anawajibika kwa matendo yake. Tungeanza kutekeleza mfumo huu, hakika ajali za barabarani zingekuwa historia ndani ya muda mfupi!
 
Nina IST ya milion 10 nilipe milioni 50 naitolea wapi?
Meneja kwanmna hiyo ajari zitatengenezwa na zitakua nyingi sanaa.

Meneja Hebu pitia tena andiko lako
 
Kwa faini hizo ,na Hali ya uchumi ya watanzania wengi,magereza yatajaa tu ,kuzimudu hizo gharama ni wachache.
Kweli kabisa. Pia mtoa mada angezungumzia kuhusu hali mbaya ya barabara zetu ambazo pia ni finyu, aina za barabara k.m. lami, changarawe n.k. Uwepo wa madaraja na hali ya madaraja hayo. Kwa ufupi kuna mambo mengi ambayo huweza kuwa chanzo cha ajali katika barabara zetu na si madereva tu. Serikali inalo jukumu la kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabarani ipo katika hali nzuri. Hizo faini za milioni 50 kwa madereva zitapelekea barabara hizo kuwa za mabilionea ambao wana uwezo wa kulipa kiasi hicho cha pesa.
 
Nina IST ya milion 10 nilipe milioni 50 naitolea wapi?
Meneja kwanmna hiyo ajari zitatengenezwa na zitakua nyingi sanaa.

Meneja Hebu pitia tena andiko lako
Sheria ikiwa ndani uwezo wa kulipa sidhani kama inaweza kuzuia ajali.
 
Kweli kabisa. Pia mtoa mada angezungumzia kuhusu hali mbaya ya barabara zetu ambazo pia ni finyu, aina za barabara k.m. lami, changarawe n.k. Uwepo wa madaraja na hali ya madaraja hayo. Kwa ufupi kuna mambo mengi ambayo huweza kuwa chanzo cha ajali katika barabara zetu na si madereva tu. Serikali inalo jukumu la kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabarani ipo katika hali nzuri. Hizo faini za milioni 50 kwa madereva zitapelekea barabara hizo kuwa za mabilionea ambao wana uwezo wa kulipa kiasi hicho cha pesa.
Yaani inamaana ya kwamba kama mtu hawezi kulipa b
 
Back
Top Bottom