Tukiwaambia Hizo Simu Zenu za 1-5m ni Mitajji Mnatuita Motivational Speakers!

Tukiwaambia Hizo Simu Zenu za 1-5m ni Mitajji Mnatuita Motivational Speakers!

Hayo ma-BMW na Mercedes Benz unayoandikaga humu ni mtaji wa kilimo. Mwaka huu kaulize January kipeto cha viazi chips kimeuzwa bei gani.

Mtaji 2.5 or below kwa ekari, kipeto kimoja kimeuzwa hadi 100k majuzi tu hapo. Ekari moja unatoa vipeto zaidi ya 70 hadi 90 ukilima kwa kuzingatia. Kuna mtu kila ekari katoa 8.3M alilima ekari 15.

Kwa vile umeshauri wenye simu za bei wauze waagize vitu China, nami nakushauri uza gari moja la gharama kisha nunua Passo hiyo nyingine tia shambani.
Umetumia siraha kali sana mkuu,kumshambulia adui 😀😀
 
Iko hivi 2025 yote kila mwezi au miezi miwili nilikuwa naagiza mzigo mdogo China. Hii ni kama side business ambayo wateja wangu kwa uhitaji wao walinishauri niwaletee hivi vitu.
Mzigo wa mwisho nilitumia 1.8m kununua na mzigo kunifikia. Mzigo ulikuwa na items kama 185. Huu mzigo wote niliuza na kupata around 6.5m. China vitu bei rahisi sana. Na sio lazima uende.
Sada hapo unaweza kuona ka mtaji ka chini ya 2m kanazalisha 6.5m. Hivi iPhone bei gani?
Uzi tayari.
Cc Chivundu
Kuambiana kupo kusikilizana ndo hakuna
 
Kumbe hii kampuni ilishakufa!
Ilipata misukosuko muda fulani, hata sabotage ilihusika mambo ya ushindani wa kibiashara. Ilipoteza customer base kubwa nadhani trust wanairudisha kwa shida.

Kwa sasa Silent Ocean na GNM wanasikika kwa wingi. Kuna Wachina wanaibuka na kutoweka kina Win Win Cargo, hao Wachina wenzao ndio wanaanza kuwaweka kwenye mstari wanapitisha mizigo huko kwa kampuni ambazo wabongo wanyonge ndio wapo front.
 
Nina ekari zinanitosha. By the way sijashauri mtu auze simu yake. Kwanza wenye iPhone za maana humu wanahesabika.
Wewe huna hela ...watu wenye hela hawana hata muda wa ku brag humu...unachukua mzigo wa milioni tu kelele kibao hadi mimate..wanaochukua mizigo ya bilioni 3 hawana hata muda ..unazungumzia iphone? Watu wanatembelea gari za bilion unaongelea iphone ya maana?
 
Duuh watu mna stress sana.
 
Kampuni ilifirisika na pia nahisi ilifanyiwa figisu kiasi chake. Kampuni watumishi wengi ni Wakinga, ofisini ni mwendo wa Kamwene! Kamwene!

Mapembelo walikuwa wanasifika kwa kuwahisha loose cargo, ambazo Silent Ocean huwa wanachelewesha wao ni wazuri kwa makontena full. Na pia Mapembelo walikuwa wanagandamiza vizuri bale za nguo, nguo nyingi zinakuja kwenye bale moja na walikuwa bei chini kidogo kwa bei dhidi ya Silent Ocean. Soko la nguo Kariakoo limetekwa na Wakinga, ukichangia na kujuana wakajazana Mapembelo kuagiza. Na waagizaji wengine wa aina nyingine na mizigo mingine. Kampuni ilipokufa mizigo iliibiwa, au ikapotea, au kulikuwepo na madeni bandarini mizigo ikakamatwa. Yote kwa pamoja yanawezekana.
Duuh...naijua Mapembelo ila sikujua kama haipo tena! Ni ya mkinga yes,na wakinga walichangia sana kumsapoti ndugu yao! Hizo zitakuwa figisu za silent ocean for sure
 
Hayo ma-BMW na Mercedes Benz unayoandikaga humu ni mtaji wa kilimo. Mwaka huu kaulize January kipeto cha viazi chips kimeuzwa bei gani.

Mtaji 2.5 or below kwa ekari, kipeto kimoja kimeuzwa hadi 100k majuzi tu hapo. Ekari moja unatoa vipeto zaidi ya 70 hadi 90 ukilima kwa kuzingatia. Kuna mtu kila ekari katoa 8.3M alilima ekari 15.

Kwa vile umeshauri wenye simu za bei wauze waagize vitu China, nami nakushauri uza gari moja la gharama kisha nunua Passo hiyo nyingine tia shambani.
Alhamdullah mmefikiana sasa hapo nimeshukuru maana niliambia Negative

RRONDO
 
Back
Top Bottom