Tukubabali au tusikubali, Hayati Magufuli alikuwa mkombozi wetu

Tunahitaji jambazi aje apambane na majambazi ya mizoga.
 
Nanoi huyo anaejua kiingereza ukimtoa Nyerere na mkapa??
Kikwete alisoma hotuba same to Zumaridi wenu.
 
JPM mwacheni apumzike basi khaaaaaa....

Mnamtetea saaaaana,,, kama alifanya makubwa acheni watu wayaone....


Acha kupiga mayowe, waache watu waone wenyewe - Unknown
 
Mapato ya chama yalipaa kutoka milioni 50 hadi trion moja na nusu maana ccm walidhiodhi kitapeli,
Walikodisha vibanda kwa kwa laki nusu na kulipa ofisi za ccm elf25,
 
Sasa kama huyo tajiri alitesa ndipo akapata ni kwa nini nae asiteseke?ungejua wanayofanya katika ulimwengu wa roho!!!!
 
Alikuwa anakuja kuomba chakula kwako?
 
Umestaarabika yakhee!
Hakika walioathirika wanajulikana. Wezi, wavivu wa kazi,majangili wa rasilimali, wachimba migodi mafilisi,wakwepa kodi,wafanyakazi haramu na listi inaendelea...
Nina uhakika jamii yako imo kati ya hao juu.

Watu wake wa Hayati wamekuwa wanateseka kwa karne nyingi.

Weka akiba uzandiki wako na hasama zako.
Mtashindwa tu
 
Yawezekana hujaelewa somo.
Ni kwamba, JPM alifanikiwa kufanya makubwa yaliyoshindikana tangu enzi za Mwalimu.
Hapo nazungumzia JNHP, IKULU kuhamia Dodoma nk.

Lakini pia kabla yake vibaka walitapakaa kila kona, lakini alipoingia tu madarakani, vibaka wote walipotelea kusikojulikana.
JPM aliacha Mfuko wa mbolea ukiuzwa kwa sh 45000/50000 lakini sasa mfuko huo umepanda bei na sasa unauzwa kwa sh. 130,000 hadi 150,000. Si mbolea tu, hata vitu vingine vinapanda bei kila kukicha.
 
Jamani mbona hayo juu yalikuwa ni mlolongo mrefu wa malani(ilani) ya chama cha alichokuwa anawakilisha.
Mmnamsema kana kuwa hakuwa binadamu anayetenda makosa, huo ni ujambazi wa asili ya Ubinadamu.

Ridhaa aliyopata ilimfanya kiburi kupita kiasi. Wenyewe mnawajua waliompa ridhaa hiyo?
Kweli kuna mashetani duniani, chagueni upande, Lakini mkumbuke kila pande lina sehemu ya kufikia, Umilele.

Naionea huruma familia yake ya kwanza, mjane wake, watoto zake. Jaribuni kuwa na bakshishi ya maneno ya kubeza mfuu.
 
IKULU kuhamia Dodoma nk.
Hili Lina tija Gani? Yaani serikali kuhamia Dodoma ni mafanikio? Au ni gharama tu kwa raia maskini?

Hivi hiyo pesa ingepelekwa kwenye bajeti ya maendeleo ya kilimo ambayo huwa inatekelezwa chini ya 20% unadhani tungekuwa wapi sahivi kma sio uchumi wa kati juu??

Kuna mambo ya kumsifia ila sio kuhamia dodoma hiko means nothing.....

Afu unasema eti Bwawa La Nyerere limeshindIkana toka uhuru? Kwani kusambaza umeme wa gesi uliwezekana tangia uhuru? Maana kama shida ilikua ni umeme tu mbona hamtoi credit kwa Kinyerezi 1 and 2 ambayo ni Miradi ilianza na Jk?

Unafiki unawasaidia nini?
 
Mapato ya chama yalipaa kutoka milioni 50 hadi trion moja na nusu maana ccm walidhiodhi kitapeli,
Walikodisha vibanda kwa kwa laki nusu na kulipa ofisi za ccm elf25,
Acha unafiki!! Hizo Mali nyingi ziliporwa maana zamani ilikua chama kimoja sasa tokea vyama vingi vije ilipaswa hizo Mali zirudishwe kwa Umma maana walitumia pesa za walipakodi kujengea say viwanja vya mpira, Majengo n.k

So kabla ya kusema alibana mafisadi ndani ya CCM hata umiliki tu kuhamisha CCM ulikua wa kifisadi ilipaswa azirudishe kwa Raia na sio kuendelea kuhodhi kihuni.
 
Kwa hiyo mmekata tamaa baada ya mkombozi wenu kufariki?
Poleni sana.

Pia mkumbuke kuwa, Magufuli huyo huyo kwa watu wengine wengi alikuwa ni muuaji, mkatili, Dikteta, mfilisi na shetani.
Hujakosea, ni kweli alikuwa muuaji kwa wezi,majambazi, panya road na ndiomana alifanikiwa kuyapunguza,mkatili, dikteta kwa kusimamia sheria na kutocheka cheka na wazembe selikalini. mfilisi kwa matapeli na wezi waliofilisi nchi hii we ulitakaje?😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…