Tukubabali au tusikubali, Hayati Magufuli alikuwa mkombozi wetu

Je sasa Uhuru wa vyombo vya habari umeongeza nini kwenye pato la wananchi?
je, kuminya uhuru wa vyombo vya habari kuliongeza nini kwenye pato la wananchi? Wananchi kupata habari ni moja ya haki za msingi za taifa lolote.Jiulize bila tv, redio, magazeti maisha yangekuwaje?
 
UU! Umekushibisha uhuru huo,uhuru unaousemea unanisaidia Nini Mimi ninayeumia na mfumuko wa bei za vitu madukani
Kwaiyo magufuli angeenda kuizuia russia isiivamie ukraine? maana icho ndio kilichopandisha bei ya vitu?
 
Kama alikukomboa wewe na Sasa unasugua juu ya mawe basi pole Sana endelea kuomboleza,zamu kwa zamu.
 
Mumfanyie tajiri lolote bila woga hii imekuwa Banana Republic.
Nchi inapaswa kuongozwa kwa katiba, sheria na taratibu na Mtanzania ana haki ya kustawi katika nchi yake kwa juhudi zake akizingatia hayo.
Tuondoleeni roho zenu mbaya nyeusi.
Alikomesha mambo yote ya blaaa blaaa, sasa yamerudi kwa kasi. Ninapenda hii "tajiri kufanyiwa lolote bila woga" sasa mguse tajiri unuke.
 
#3 eti mama anataka nidhamu ya moyoni sio ya woga....
Hahaha! Kabla JPM watu tulikuwa tunaingia kazini(hospitali) na mkoba umejaa dripu, ganzi, mabomba ya sindano, dawa na kadi za wajawazito na kuuza mchana kweupe, ni JPM era nilishuhudia dawa maarufu "pawasefu" ikiletwa kwenye kiti ya MSD ngazi ya zahanati!(nidhamu ya moyoni hiyo) sasa hivi taratiiibu wameanza tena nimeona wajawazito wanatumia photocopy za kadi za kliniki nikawaza "neema" umerudi kwa manesi wenzangu ila bahati mbaya nilishaondoka huko nipo zangu mgodini Ikumbayaga tunatorosha tu dhahabi bila tozo....mitano tena kwa SSH!
 
Mimi mwenyewe nilifurahi sana. alijifanya anajua,kumbe mbwiga tuu
 
Alikuwa Rais mwenye akili nyingi kuwahi kutokea.

Yani Rais ambae hadanganyiki hovyohovyo.
Rasi anaejiamini, rais anae fuatilia maagizoyake, rais anae fanya ziara za kushtukiza,ambae mbali na taarifa anazopewa na wasaidiziwake yeye mwenyewe anauwezo wa kuzichambua na kupata ukweli.

Kikubwa zaidi hakuwa muoga, na hakutaka kuyumbishwa na matajiri na mabeberu.

Aliweza kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati bila kupanda ndege kwenda ulaya.

Ndio maana watanzania wote walimuamini sana sana sana.

Viongozi acheni kumpiga vijembe magu, pigeni kazi tuwapime kwa jinsi mnavyo tuhudumia, acheni wivu.
 
Kila nafsi itakiri ni swala la muda tu.RiP Jembe
We ngoja tu, tutaelewana tu. Uzuri ni kwamba, kila wakijaribu kupindisha ukweli juu ya JPM, baada ya siku mbili tatu wanaumbuka.

Wameshasahau kipindi ambapo magari na Mabenki yalipokuwa yakitekwa na kuporwa mchana kweupe.
 
Umesahau mengine,
Kujenga Ikulu Dodoma huo ni ujambazi, kudhibiti ajali za kijinga kijinga huo ni ujambazi, kutokomeza vibaka waliokuwa wametapakaa mitaani huo ni ujambazi, kuiingiza Nchi katika uchumi wa kati huo ni ujambazi, kuleta nidhamu ya watumishi wa umma huo ni ujambazi nk.
 
Yawezekana ulikuwa bado hujazaliwa, wakati wa huyo jk ndipo umeme ulipokuwa unakatika karibu kila dakika kadhaa, lakini hali hiyo ya kipuuzi ilidhibitiwa na JPM.
Sasa hali inarudi kule kule.
 
Daaah ni kweli mkuu,ukiangalia jinsi mambo yanavoenda, magufuli alikua jembe

Ila tufanyaje sasa?tunajifanya kupinga tu kwa roho ngumu ili tuonekane wagumu ila kwa sasa tunapigwa kila kona

πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜€
 
Kwaiyo magufuli angeenda kuizuia russia isiivamie ukraine? maana icho ndio kilichopandisha bei ya vitu?
Muda mwingine tuwe tunafikiri mambo kiyakinifu.
Vita vya Russia na Ukraine vimeanza juzi hapa wakati huo bei za vitu zilikuwa zimeshapanda tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…