Mkuu sio malezi mabaya, mfano upo kwangu....... miaka ya 1997/98 huko nilikuwa mbali na wazazi na hicho ndio kipindi ambacho nilikuwa najaribu kufanya kila kitu, nikaanza kupiga nondo kwenye hizi gym za kiswahili, mwili ukakubali nikaanza kunyoa kama mwamba Mike Tyson (namkubali sana huyo dingi) maisha yakaendelea lakini niliogopa kuvuta bangi tu.
Nikapata demu ka binti ka kiswahili mitaa ya Igogo Mwanza, kakaiteka sana akili yangu, ka Mwanaidi kakanifundisha hata kula kiboga .......piga sana samvu la kopo........kajinga haka ndio kakanishawishi nichore huu upuuzi.....siku nimerudi nyumbani bi mkubwa akaona huu uchafu, hakuangalia eti nimekuwa baunsa [emoji1787][emoji1787], hakuangalia kwamba eti amenikumbuka siku nyingi hatujaonana, alinipa masaa matatu niwe nimeyafuta ndio tusalimiane.
Haikuwa mpaka masaa matatu yalipokamilika.......bi mkubwa alinivaa huku ananivurumishia makonde mazito mazito ya uzani wa juu sana (bi mkubwa wangu alikuwa mbabe sana na ana mbavu nene haswa) nilipigika kiukweli sio siri, ili ni takribani dakika 45 za mfueni hevi uliounganisha vipigo vya aina tofauti tafouti.......
Nimalizie tu kwa kukwambia mtoa mada sio wote wenye tatoo wameendekezwa kwenye malezi yao.