Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Wakato nasoma ile likizo narudi dar kutoka mbeya..
Nikapanda magari ya wafanyabiashara wanaoemda kufunga mizingo yanaondoka mbeya saa10 jioni na kufika dar asubuhi saa11..kabla hatujaingia morogoro kuna tulikuta jamaa wamemwaga ulezi na maganda ya ndizi gari ili sleep sana watu konda akasema ficheni mali zetu tunatekwa..
Mbele kidogo wametandaza sijui ni mbao zile zinamisumali dereva alijaribu kutaka kurudi nyuma ikapigwa shaba kwenye tairi na taa moja ya mbele,gari ikasimama dakika o zinatoka njemba porini zimeshiba wamevaa mask wameshika bunduki,wakatoa amri kila mtu atoke kwenye gari akiwa na boxer kwa wanaume na wamama watoke na chupi na sidiria tu huku majambazi wengine wamelizunguka gari wengine wameshaingia kwenye gari..hapo dereva ameshakula kichapo cha mbwa mwizi kwanini alitaka kurudisha gari nyuma.
Unavyotoka nguo unaacha kwenye gari unasachiwa kwenye boxer na wamama wanasachiwa kwenye matiti na kwenye chupi ukishasachiwa tu unapigwa mkanda wa mgongoni ulale chini,
Kuna mshua mwingine alitaka kuwavimbia alikua na bastora wakamuwahi aisee alipigwa sana hadi kuvunjwa mkono wake jamaa wana roho mbaya sana
Baada ya lile zoezi kuna majambazi wengine wakawa wanapakia vile vitu kwenye gari lao wengine wanapekua kwenye siti za gari wanazichana chana na visu kama mtua!eficha pesa au simu kwenye siti ya gari..tumelala pale tunakuja kumashwa na madereva wengine wapita njia majambazi wameshaondoka. Tukaenda police kutoa taarifa wachache walipata msaada wa makoti na vikoi wengine tulishuka pale kidongo chekundu tukiwa na boxer na wamama wengine wakiwa na chupi wafanyabiashara wa pale kidongo chekundu walitununulia nguo na kutupa nauli.
Kwa hesabu za haraka hili tukio walilifanya halikuzidi dakika15
 
Kaka Galadudu,,hii ya 2007 km chai vile[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo yule mzee alibahatisha hakuibiwa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Walimsalula kila kitu maana mchoro wote ulishachorwa kila kitu na walikua wanajua huyo mzee analala chumba namba ngapi so hakuna ambaye alipona labda yule dada wa chumba cha mwisho aliyekutwa na pichu tu ndio alipona kama alikua na mali
 
Wandugu njooni uku mtilike tufurahishe nafsi.

Me sina tukio lolote, huwa sitembei usiku sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Axee juz kati tu tumetok na mwana kupga masanga city cetre igoma,mishale ya ngoma nane tunarud mageton,tukakuna na vicheche ka kumi iv,ss mwnzangu yy kashiba kidogo ana li mwli,kaanz kutisha kuwa wote napasua vichwa,jamaa wakasita kidogo,cha kuja kustahajabisha akataka kuokota jiwe huku keshawaambia atapasua vichwa kwa risasi,tulikimbizwa,nashukuru Mungu miguu yangu haijawah nisaliti
 
hii imenichekesha sana yaani kibaka ana confidence ya kufa mtu ei "oyo nisubiri"
 
usiku kwenye watu wengi hauwezi kuyakumbuka haya, ukibisha utapigwa sanaa.
Kweli kabisa mkuu mimi enzi za ukuaji nilikua napiga sana zoezi la capoeira almaarufu paranawe ila ilikuwa for a self defense tu sasa kaka yangu mkubwa akawa anachanganya na makareti sijui judo akajiona mtamu balaa, siku hiyo katoka kazini usiku anatembea mdogo mdogo mara watu hawa hapa wamemuweka mtu kati wana panga zimenolewa jamaa si akajikuta shababi kupambana na hao wahuni, kilichomkuta tulipigiwa simu na wasamaria wema tukamuangalie ndugu yetu yupo mahututi hospitali, tangu siku hiyo jamaa anakuambia akikutana na watu wakamtaiti kama hana ujanja ananyanyua mikono juu tu wachukue wanavyovitaka wasepe
 
Mwaka 2005 mida ya saa tisa usiku natoka kwenye promotion ya safari lager miaka iyo,bia za mafungu,mtu tano hizi hapa,wakaanza mtama,nikala teke,nilikuwa najiweza nikarusha ngumi nakumpasua mmoja,wakaokota mawe ,speed nikatoka maana mawe sio,njombe hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikawaje???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akapewa kichapo na hela akatoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…