Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Naona hapa wengi wamekutana na vibaka tu Ila sio majambazi.Leo nimekutana na majambazi hapa Johannesburg South Africa kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.

Nimetoka Eastgate mall mida ya saa moja hivi nikaona ubahili kukodi Uber nikatembea kwenda home . Nimevuka mataa kuna gari (salon) imesimama baada ya taa nyekundu kuwaka ,mara kuna salon nyingine ikaja ikaizuia gari ya kwanza halafu watu watatu wakashuka na bunduki AK-47 kama sikosei.

Nilipigwa na butwaa halafu jamaa akaenda mlango wa nyuma wa upande wa abiria ,ile anafika tu kapigwa risasi akaanguka ,wale wawili waliobaki wakaanza kumimina risasi nyingi.Jamaa akajibu mwingine tena akaanguka chini.Muda huo nimekimbia kidogo halafu nimelala chini,najiburuza kama Rambo vile, jamaa wa tatu aliyekua amebaki akaenda kujificha nyuma ya gari huku wakiendelea kurushiana risasi na jamaa wa kwenye gari

Nimejiburuta umbali mrefu kweli nikainuka huku nikipiga mbio nyingi sana kwenda home.Risasi zisikie tu kwenye movie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mdogo wangu pamoja na rafiki yake wallikua wanakaa kwenye nyumba ya bro ilikua nyumba mpya. Usiku wa manane jamaa wa mapanga shaa wakaanza kuvunja mlango. Basi madogo kushtuka usingizini wakaanza kupiga kelele kuita majirani wakidhani majamaa yatakimbia. Cha ajabu majamaa hayaongei chochote yanaendelea tu kuvunja kimya kimya tena bila story. Madogo kuona makelele hayasaidii wakabadili style wakaanza kuchimba biti na kutukana matusi ya nguoni...'waseng nyie ingieni tuwaonyeshe kazi, mnadhan sisi tunakaa kiboya humu..ingieni tuwafumue marind...'. Wale majamaa wala wao hawaongei wanaendelea tu kuvunja bila story na mtu. Madogo mle ndani wakaona hawa jamaa mbona hawatishiki...ikabidi waanze kupiga maombi na kukemea pepo kwa sauti kuu na wakinena kwa lugha. Basi yale majamaa yakafanikiwa kuvunja yakaingia...yakawanasa vibao afu yakasepa na vitu kidogo na simu maana nyumba haikuwa na kitu na madogo walikua wanaenda tu kulala..
 
Hahaha nimcheka hapo eti ingieni tuwaonyeshe kazi mnadhan tunakaa kiboyaboya tu
 
Huko SA kuna utu wowote uliobaki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sauzi Kuna wizi Sana wa magari, ngoja nitakuwekea link ya video

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda jamaa ako anaconnection na hao watu, Kwanini ajiamini hivyo..
 
we ni jilani yangu,bila kusahau ile ya mabatini,mangi alichezwa na machele,
 
Mwaka 2012 kipindi icho ndo nachipukia usichana niliendaga coco wananchi
Tuliporwa sikuhiyo vibaya mno..pale katikati ya maisha cluba na coco nilivamiwa na vibaka machalii tu kama kumi na zaidi
Nilivyowaona wananijia nikatimua mbio nilikua nmebeba kihandbag cha nainai kina mnyororo mkubwa kilivutwa ule mnyororo ukanichana shingo
Nilijikuta kawe .
Nilipata mikasa sikuiyo mana nilikua sina mbuni nafikaje Om kwa mguu.
Tangu siku ile nmejifunza mambo mengi sana maishani
Sijawahi kwenda kwenye kusanyiko la watu wengi tukiachana na sherehe & kanisani
Beach sijawahi kukanyaga hadi leo ahilia mbali naishi Dsm yani nafanya tu kuyaona maji yale nikipita posta etc nikienda mahala natamani kubeba mabodyguard

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh sasa walipata faida gn kuiba simu ya elfu 70? Hivi yule Mama angekubali ile laki 1 inamaana wangemuachia au wangempora? [emoji51]
Sio kwamba wale walikuwa washafanya yao sasa wakawa wanarudi, na pengine maza nae labda aliibiwa humo humo na vibaka wengine.
Mtu mwenye chuma hawezi kuiba simu kirahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tandika walikua na hii tabia sana[emoji23] mtu unashikwa bega unaambiwa dada zile simpo utanipa sh ngapi
Akati izo simpo mtu kazivaa anatembea hana hili wala lile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…