Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

[emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwaka 2004 mwezi wa 7 sumbawanga to mpanda saa 11 alfajiri maeneo ya mbele ya stalike tukiwa na basi kampuni ya,sumry high class enzi hizo.Barabara mbovu balaa mnatoka swanga saa 7 mchana lakini mpanda mnafika asubuhi au alfajiri.
Kuna jamaa alikuwa na mipesa yake wazee wa kazi walimlia tatget toka mbeya hadi tdma bila mafanikio wakaamua kuja naye swanga hadi kupanga guest moja naye bila mafanikio na ndipo waliamua kumlia target mpanda road stalike baada ya kujua jamaa yule alikuwa anaenda mpanda na zile pesa.
Sitaki kuzama sana maana shida tuliyoipata alfajiri ile haitosahaulika.Alikufa mmoja lakini pia baada ya kuondoka nyuma yetu kulikuwa na mkurugenzi wa mpanda naye akatekwa na gari yake kutumika na majambazi kubebea pesa na kukimbia nayo na kuitelekeza kambi za wakimbizi huko katumba.
Kwa ufupi kwa miaka niliyowahi kuishi mpanda ambayo sasa ni mkoa wa katavi nimeshuhudia ujambazi mwingi sana maeneo ya mpanda mjini, karema road na ikola ambao hadi wamewekewa ulinzi wa wanajeshi baada ya askari kuchemka maana wale wazee wa kazi walifikia kuandika hadi barua kuwaambia polisi lini wanafika kuiba.
Nadhani kwa sasa mpanda ya sasa ni tofauti na ile ya zamani maana mara nyingi tulilala maporini kwa ajili ya majambazi ambao wengi walitoka drc Congo huku wakiita tz kuwa ni dubai yao ya kubeba mali.
Pongezi kwenu wanajeshi wa kigango cha ikola mliwanyoosha sana,miaka ile ya 2004 kurudi nyuma hasa tukio la kasangantongwe.
Mungu bariki jeshi letu la tz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyo mr. wako ni mimi kabisa.
 
Kuna siku natoka mishe kuna kichochoro napita nimeongozana na jamaa mmoja, yeye mbele mie nyuma kama hatua kumi na tano hivi, kila mtu yupo mdogo mdogo.

Wakati safari inaendelea kuna njemba mbili zikanipita na salamu zikanisalimu kabisa, inakuaje nikajibu poa halafu zenyewe zikaendelea mbele,

Kufumba na kufumbua naona yule jamaa alie mbele anakabwa.

Kwanza nilistop halafu nikaanza kujiuliza mimi ni nani mpaka vibaka waniache wakamkabe aliye mbele? Nikaona hili ni zali la mentali, so nikapanga nigeuke fastaaa nianze kukimbia.

Nilipogeuka nikaona kuna washkaji watatu wanakuja nyuma yangu, hapo nikaona yeees nimepata kampani.

Nikaanza kuvimba sasa,
Hapo niko bize nawaambia wale wa mbele ‘oyaaaa nyie mafala hebu muacheni mwanangu huyoo kabla sijawaletea noma’(majamaa yapo bize yanampukutisha tu mchizi)
Mie; oyaa hamsikii? Ujue nikija hapo ntawaletea noma mpaka mkasimulie kwenu’’
Mara jamaa akajibu unavyoongea hakikisha mfuko wako uko vizuri,
Kisha likaendelea Oyaa mbona mnamchelewesha huyo ndezi.

Duuh niliposkia hivyo nageuka nyuma naona njemba zile za nyuma zina mapanga, duuuh! Ki moyo moyo nikasema yaani mie naona nyie wana kumbe ni timu moja, nikatulia wakachukua hela yote iliyokua kwenye pochi halafu wakasema twende kwa yule wa mbele

Basi bhana ile tunafika kwa jamaa anaekabwa pale mbele wale wakabaji wake wakasema huyu ndezi hana kitu tumemkuta na spana tu
Akala ubapa wa beka wakamuuliza mbona hatembei na hela?
Akaanza kulia anasema yeye ni mgeni hapa mjini.

Basi yakasema tupigane makofi mawili mawili kisha tusepe, jamaa likanipiga kindezi ndezi ila ilipofika zamu yangu nahisi alisikia uchungu kama ule niliosikia mimi nilipochukuliwa hela yangu,

Baada ya kuachiwa hakuna alieongea na mwenzake mpaka tunaachana, mie hapo kucheka natamani kulia natamani


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji38][emoji38]
 
[emoji38][emoji38]
 
Naomba niwe mlinzi wako binafsi kuanzia leo
 
[emoji1787][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji1787][emoji16][emoji1787]my ribs

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji81][emoji81][emoji81][emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…