Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mmmh, mkuu umeongea point,

Maana kila mgeni anayehamia kwake kajenga lazima avamiwe na majambazi, labda nyumba iwe mbovu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungeeleza zaidi jinsi walivyowekewa mtego na matukio yaliyofuata.
 
Nilikutana nao kisumu usiku wa SAA nane nikiwa naelekea kazini.nipata konekshni na Jamaa Fulani alikua engineer wa kplc yani Tanesco ya kenya.sa tulikua tunapelekaga UMEME vijijini kama REA(rural electrification authority).sa inabidi kuanza safari ya kutoka kisumu kwenda vijijini usiku wa SAA nane au Tisa ili SAA moja tii tuwe eneo la tukio tupige kazi.basi bana kama kawaida kazi ikatokea usiku tuamke tukapande ndinga,,nilikua na mshikaji wangu anakaa mtaa wa pili ananipitia tunasepa wote gari iliyobeba vitu vya kazi ilikua INA paki mbali kidogo na tunapoishi.sa mshikaji akanipigia simu toka nshafika nje tuende job usiku mmoja hivi.mi hapo nshavaa ovaloli langu Niko na ka bengi ile nafungua mlango wa geto napigwa telo kudadeki na Jamaa kama saba wana mitutu na matochi.nikapigwa kitako cha bunduki usoni nikalazwa chini kikakanyagwa na kugongeshwa vya kutosha.wakaingia chumbani wakachukua simu,nilikua na 3000ksh wakachukua.hahaha nilikua na perfume ya cool water nilinunua mwanza wakaiba nayo.washenzi mnoo hata sikua na kitu nilikua kavulana ka chuo kanakofanya kazi na kusoma tu.niliachana na kazi Hiyo usiku uleule.


Mungu sio Mzee mkumba nikawaza niishije Mara nikaanza kufundisha waZungu kiswahili nikapiga ela Zao mno.zile jambazi za kenya zilikua ninakanyaga na kunigongesha huku zinasema Pendukaaa,pendukaaa naangalia nani.yani penduka ndo pinduka,haya maneno mpaka leo hayajawai futika kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya kukamatwa kuna jamaa yangu ndio alionekana pesa ilitumwa kwake


Alikua na duka la simu mitaa ya dampo/ngokozi ndio mfadhili wao alikua

Ni jamaa tunaejua fika.
Duh dunia hii umdhaniae ndiye kumbe mmmm
 
Huyo hakuwa Sheikh, Alikuwa mganga mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]daaah nimecheka sana! Hii ndiyo comment bora kwenye huu uzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyu polisi si umuue,nitafute nikuelekeze sehemu wanayokodi bastola,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halalbadir...huwa haisemi uwongo...tatizo kumpata msomaji wa ukweli sasa...maana ina masharti maalum!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…