Tumejipanga kusikia mengi...but our focus remain
Bila shaka.
Lakini kuna mengi pia ya mama kuyazingatia.
Nakupa machache:
1.Sera ya madini.
Ni lazima serikali isimamie sera mpya ya madini iloweka na iruhusu wawekezaji zaidi wa kigeni kwa makubaliano kwamba hawasafirishi nje makinikia na wawekeze maeneo yanozunguka migodi.
Kuwekeza kwa maana kwamba hawaachi mashimo na umaskini kwenye maeneo hayo.
Pia kuwekeza huko kutawainua wananchi ili nao wajisikie nao ni sehemu ya "Gold Rush" kama ya Ikumbayaga.
Pia JWTZ iendelee na ulinzi wa mgodi wa Mererani Arusha na kudhibiti utoroshaji wa madini ya tanzanite.
2. Sera ya utalii.
Wawekezaji wa utalii walipe kodi kulingana na kipato chao na mashine zile za TRA zitumike ipasavyo. Vijana waongoza watalii nao wawe sehemu ya wajasiriamali na hiyo iwe na ajira rasmi kwa vijana ila watambulike kwa TIN number zao.
3. Mikataba ya uwekezaji kwenye maeneo ya teknolojia na sayansi ipewe kipaumbele kwa makampuni ya nje aqmbayo ya uwezo na utaalam na vifaa ambavyo sisi Tanzania hatunavyo. Lakini kwenye hili fedha wanazolipwa watumishi wa kampuni hizo wakiwa hapa Tanzania zikatwe kodi kabla ya kwenda kwenye akaunti zao huko nje.
4. Kila mtanzania mwenye kuingiza kipato halali alipe kodi. Kodi ndo msingi wa maendeleo ya kila nchi. Kodi ndo hutumika kujenga miundombinu kama barabara, shule na mahospitali.
Serikali yaweza kusema kuanzia sasa kila mtoto anaezaliwa kumbukumbu zake ziwekwe kwenye kanzidata.
Kila kata, manispaaa na wilaya ziwe na kanzidata za wakazi wake na kila nyumba ilipe kodi ya maendeleo. Hizi kodi ndizo zinasaidia kusafisha na kupendezesha miji, barabara za mitaa na usambazaji wa huduma muhimu kama maji.
5. Kuimarisha mahusiano na Kenya na Rwanda ambao ni majirani zetu wazuri. Kenya ni mabepari ambao wamekuwa huko nyuma wakifanya biashara zao bila kuingiliwa. Tuwape ushirikiano khasa kwenye suala la EPA ambalo wao tayari wanashikiana na nchi za Ulaya.
Kuhusu Rwanda, ni katika kuhakikisha biashara kati yetu na wao inayohusu bandari ya Dar na mipakani inaimarishwa kwa kuwekeana viwango rafiki vya kodi ili kuvutia zaidi biashara zao na za kwentu kwao.
Hayo ni machache lakini kuna mengi ntaleta kwa kadri serikali itavyokwenda na "trajectory" ya mtangulizi wa mama Samia.