Tulizeni Mioyo Watanzania: Taifa liko Salama Mikononi mwa Mama Samia Suluhu Hassan
Wanajamvi kwanza nitoe pole kwenu nyote bila kujali itikadi za kisiasa au imani za dini. Poleni sana kwa kumpoteza raisi aliyekuwa ana uthubutu hasa kwenye kutekeleza miradi mikubwa. Hapa lazima munielewe maana baadhi yenu hamkawii kunitusi na kuniita MATAGA buku saba mzee wa Lumumba.

Kawaida hakuna binadamu mkamilifu , tukubaliane kwamba Mheshimiwa alikuwa na mapungufu Kama wanadamu wengine. Lakini pia alifanya Taifa hili lipige hatua kubwa mpaka kuingia uchumi wa kati. Kikwetu marehemu huwa hasemwi vibaya ni mwiko kabisa.

Tukirejea kwenye mada ni mda muafaka kwa watanzania na watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii, kufunga na kuomba ili Mwenyezi Mungu amtie nguvu Makamo wa raisi(Raisi mtarajiwa)

Kwanza aiongoze nchi katika misingi ya kuleta umoja wa kitaifa, maridhiano, kuaminiana, mshikamano na kupendana Kama enzi za Hayati Mwalimu.
Pili miradi mikakati ambayo ameiacha Hayati jemedari JPM aiendeleze maana ni kwa faida yetu na vizazi vyetu Kama watanzania.

Tatu awakumbuke watumishi waliopo serikalini na pia wastaafu ambao bado wanasota kupata mafao yao.

Nne aongeze ajira kwa vijana wetu
Ni hayo maombi yangu machache kwa siku ya leo wanajamii.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
 
Hata ingalikuwa ni kweli haya umtuhumuyo nayo ni Rais/ Mfalme gani kuwahi kutokea duniani ambaye hakuua?! Anzia kwa wa kwenye Misahafu sembuse hawa wa katiba za vyama na nchi, manabii na wafalme wakina Sauli na Daudi
Kwahiyo unahalalisha ubaya kwa ubaya? Kama fulani alifanya mabaya basi na mwingine kufanya ubaya kama ule ni sahihi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magufuli kaondoka dah, sawa yafuatayo si ajabu yakawa mandated:
1.Kuvaa barakoa
2.Social distancing
3.Lockdowns
4.Inayoitwa chanjo ya C-19, ambayo kiukweli sio chanjo, lakini ni bio-weapon.
5.C-19 IDs.
6.Relaxation ya sheria za Ushoga.
5.Ngada kama kawa.
6.Ujambazi kama kawa.
7.Wizi wa mali za umma na uonevu wa wananchi kama kawa.

Na sina shaka yeyote kwamba sasa hivi mabepari wanafanya kila mbinu kumuweka Mama Samia makwapani.
Itawezekana? Tusubiri.

Tusubiri.
 
Kuna mambo ya kusema na tutayasema zikipitiza hizi siku za maombolezo. Ninawasoma wote na naendelea kuthamini michango ya mawazo yenu.
 
Kwahiyo ukiandikiwa ndiyo na Wewe tena Msomi wa Sheria wa aina yake ndiyo asijiridhishe kwa Kuipitia Katiba ya nchi?

Yaani hata Mimi tu Layman nimeweza Kuipitia hiyo Katiba na Kuielewa iweje Yeye tena a high Profile Public Figure wa aina yake asilijue hili au kuwa na uhakika nalo kabla hajatangaza?

Namkubali mno Mama Samia Suluhu Hassan ( Makamu wa Rais ) ila kwa Kukosea tu Jambo Muhimu na la Kikatiba kama hili naanza Kuingiwa na Mashaka kuwa labda Msiba umemchanganya au yupo katika Kipindi cha Vitisho kutoka kwa Watu wenye Maslahi yao yaliyoratibiwa vyema na tunayemuomboleza hivi sasa.
inawezekana alikufa cku 5 nyuma kabla ya kutangaza
 
Yaani sasa hivi nawaza hali za watoto yatima wote walio katika madaraka sasa. Wale DCs, DASs, RASs, MPs bila ya kuwasahau wale waimba mapambio wasio na vyeo.
 
tumpe nafasi huyu mama, tusimchambe kabla hajateua baraza lake...akileta ushosti serekalini itakula kwake.
 
All in all mazingira ya kutangazia inaonekana ni haraka haraka..... na pia unaona hata wamesahau kwenye sheria ni siku ishirini na moja.
Muhimu tuombee taifa na tumuunge mkono kwa sababu alikuwa na vita kubwa sana.

Na toka wiki iliyopita walivyompangia aende Tanga walilenga kumuweka mbali kabisa yeye na Waziri Mkuu kwenye jambo hili. Halafu hakuna mtu mnafiki kama Mwigulu na ana tamaaa sana ya madaraka
Hata Ile stendi ya kutangazia katengeneza fundi Maiko.🙆🙆🙆
 
Tatizo mfumo bado ni ule ule na walio madarakani ni wale wale. Tusiweke juu matumaini yetu tusije kuumia baadae
 
Mungu ninaye mwamini mimi, BWANA YESU, amuwezeshe na kumfanya kuwa jasiri na hodari. Aepuke wakujipendekeza maana watamgharimu. Uzalendo uliojengwa na JPM muda alioitawala Tanzania nawaonea sana huruma warithi wake kama hawatafuata nyayo zake.
Sioni wa kuvaa viata vya Magu.Yaani kwa ujasiri kabisa kupambana na Shetani head on!Aisee ni ujasiri wa ajabu.I believe Shetani ametaka kuonyesha kwamba he is still in control in Tanzania na spiritually nadhani kasema ngoja niwaonyeshe kwamba mnachokitegemea kiko chini ya himaya yangu na nakibeba hicho hicho.

Nakumbuka bila kupepesa macho mabeberu wakisema hatutaki Rais mwingine kama Nkrumah na Nyerere!Hii inanifanya nitafakari sana kifo hiki.Is it natural because he has extremely powerful enemies.Have they by remote control switched of the electrical gadget he was using for his heart?What exactly happened.Nawaza sana kifo hiki.A hero has fallen.Wow!
 
Back
Top Bottom