‘Tuma kwa namba hii’ wapatiwa muarubaini, mwisho wao umefika

Hakuna Mifumo thabiti ya Utambuzi wa Watu kwenye hizi nchi zetu za ki-Afrika. Suala hili limefanywa kwa makusudi na Watawala ili kuweza kujinufaisha binafsi wao wenyewe wakiwa madarakani. Mathalani, watawala wamejuwa wakivuruga makusudi mifumo ya utambuzi wa Watu katika nchi zai kwa nia ovu ya kutaka kuiba kura nyakati za Uchaguzi wa siasa, biashara haramu ya binadamu, magendo na uhalifu katika masuala ya utakatishaji fedha chafu, kufanikisha biashara zao za madawa madawa ya kulevya, na kufanikisha biashara haramu za Magenge ya Uhalifu. Mfano mzuri zaidi kwenye suala hili ni uendeshaji wa biashara ya haramu ya magenge ya Utekaji watu na kuomba "Kikombozi" kutoka kwa Wanandugu wa Mtekwaji inayofanywa na baadhi ya Watawala wahalifu nchini Nigeria kupitia kwa Magenge ya Wanamgambo wa Boko Haram.
NB: Nchi ya Nigeria ina idadi ya watu wapatao zaidi ya Milioni 200 ambao wanaishi nchini humo, lakini watu ambao wamesajiliwa rasmi kwenye database ya raia wakazi wa nchi hiyo hawafiki hata idadi ya watu Milioni 22 nchini kote. Aidha, hata SIM cards za simu zilizosajiliwa rasmi kwa utambulisho rasmi ulio halali hazifiki hata Milioni Kumi kwenye nchi hiyo yote kabisa.
That's why Nigeria kuna uhalifu mwingi Sana, na ni vigumu Sana kuwatambua wahalifu hao.
 
Ila huu ujinga unalelewa tu mkuu. Mfano, wangesema kila ambae nida yake imetumika katika namba asiyoijua basi awasilishe hiyo namba na wakala atafutwe ajibu tuhuma hizo lasivyo wakala husika anafungiwa usajili na kifungo juu basi michezo ingepungua kwa kiwango kikubwa.

Sema taifa letu na namna za viongozi wetu ni vichekesho.
 
Na wakisema Kila mtu ajisajili kwa namba yake ya nida hapo kutakuwa na watanzania wengi kukosa mawasiliano kwani bado kuna watu wengi nchi hii hawana namba za nida na sio kwa uzembe wao bali ni mifumo mibovu ya mamlaka ya vitambulisho nchini(nida)
 
Mimi Sa hivi nimetoka halotel nataka kufuta namba nisizotumia wameniambia system imegoma hadi mamba mpya ninayotumia itimize mwezi sa hadi hapo wangapi wqtakuw wametapeliwa
 
Mwarobaini # 1,watu wapunguze ujinga wawe kidogo una ufahamu
tunajuwa kuwa wajinga huwa hawaishi lakini basi huu ujinga upungue

Mwarobaini # 2,hawa mawakala wanaosajili mitaani labda waondolewe,watu wawe wanasajili kwa kwenda sehemu zao husika

Ova
 
Mimi nafikiri watu waache kuwasijilia laini watu wengine kwa sababu wengi wa hawa wanaosajiliwa laini akipoteza simu yeye afuatilii ili laini ifungwe anachofanya anatafuta mtu mwingine anamsajilia laini nyingine maisha yanaendelea sasa yule aliyeiba simu ile laini anayoikuta kwenye simu anaendelea kuitumia kutapeli watu au wengine wanaziuza kwa matapeli,hiyo ndiyo shida na ikidhibitiwa kwa watu kupewa elimu ya madhara ya kumsajilia mtu mwingine laini huenda tatizo likapungua.
 
Yaani hao jamaa huwa siwaelewi namba wanaipataje maana unaweza sajili laini leo kesho meseji inaingia hyo hela tuma kwenye namba hii..sasa unajiuliza laini inasiku moja huyu kajuaje?
 
Hakuna mwarobaini hapo.
Hawa hutumia cards zitokanazo na simu za wizi,kuokota na za marehemu wa ajali mbalimbali.
 
Huwezi kufanya hivyo kwa sababu watu wana clone namba za simu. Hujawahi kuambiwa wat wanapata messege toka namba yako wakiomba helana wewe hujatuma hizo mesjesi? Sasa huoni utafungia watu NIDA wasio na hatia? Kwa hiyo pendekezo lako ni null and void, asante hata hivyo kwa kujaribu
 
Kwanini usiangalie laini zako ulizosajili kupitia *106# ?

Maana kama kuna number ambayo huitambui na inaonekana umeisajili unaifunga ili isitumike kwenye utapeli.
 
Kongole. Umepiga pale pale.
 
Huu sio mwarobaini, ni namna ya kuwapa Police ulaji, Hili swala mamlaka wanaliweza Kimfumo, hawataki tu kutuliza vichwa
Ukiripoti polisi kuwa umeibiwa na hao jamaa, polisi wana namna ya kuwapata. Ila wanachofanya ni kuwatafuta na kugawana kilichotapeliwa.
Hata simu zinazoibwa, nyingi sana wanazipata, ila zile nzuri na za bei kubwa watasema hazijapatikana (wanazitumia wao-kasoro kama uliyepotelewa utakuwa ni kigogo au utatoa mpunga wa maana).

Polisi huita waandishi wa habari kuwaonesha simu nyingi walizokamata, lakini zinakuwa ni viswaswadu na itel za laki moja au mbili, kama ushahidi kuwa wanafanya kazi vizuri na ni waaminifu.

...Urefu wa kamba...
 
Hao wezi hawatumii line zilizosajiliwa kihalali,hao ni watu wanajua kucheza na mitandao,wanakuwa na line zaidi ya 500 ambazo Wala hazina hata usajili wa NIDA,wanakuwa wameziingiza kwenye system kwa utundu walio nao,nakuanza kuibia raia.
 
Kinachotusumbua ni rushwa tuu,laini hiyo hiyo Kuna makosa mtu akifanya anakamatwa fasta yaani huwezi kuchukua hata hatua.kwa teknolojia iliyopo Sasa hivi mtu akifanya utapeli anaweza kugundulika alipo.
 
Hao matapeli inatakiwa wakikamatwa wainamishwe tu kusiwe na mambo mengi.
 
Hao wezi hawatumii line zilizosajiliwa kihalali,hao ni watu wanajua kucheza na mitandao,wanakuwa na line zaidi ya 500 ambazo Wala hazina hata usajili wa NIDA,wanakuwa wameziingiza kwenye system kwa utundu walio nao,nakuanza kuibia raia.
Hii nayo ni mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…