PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Tume hii imeongopa mengi lakini Wacha tuangalie idadi ya Watanganyika waliouliwa kuanzia oktoba 29 hadi November 5

Kipindi chote hicho Risasi, marungu na ukatili vilitawala

Hivi kweli Dar waliuliwa watu 182?😭
Ni uongo wa asubuhi
Hii tume kweli ilifika maneno ya Kimara? Tabata? Goba? Magomeni? Nk

Kwamba Mwanza waliuliwa watu 90 tu? 😭 Ni uongo
Vijana 17 pale Mji mwema walipigwa risasi wakiwa wanatazama mpira.
Watoto wa academy pale Isamilo 15 walipigwa risasi wakiwa hostel

Vijana wengi Kisesa, Kishiri, Nyegezi ni wengi mno acheni siasa za kijinga

Arusha ati walikufa watu 53?

Vipi Songwe hawakuuliwa watu hakuna idadi ya Songwe

Vipi Geita na KATORO hamjatoa figure Yao?

Vipi Watu wa Kahama waliuliwa wangapi?

Vipi Watu wa Musoma, Tarime, na Bunda? Waliuliwa wangapi

Vipi Watu wa Songwe,. Njombe, Chunya na Mbivu? Waliuliwa wangapi

Vipi Watanganyika wenzetu wa Dodoma waliuliwa wangapi?

Vipi Watanganyika wa Pwani, Kibaha, Vikundu walikufa wangapi?

Tume imefanya uhaini na ilaaniwe
View attachment 3577951
Mimi nafahamu watu watatu walioliwa Geita
 
Nafikiri wao wameweka idadi ya taarifa walizokusanya, kuna sehemu mbele kasema upo uwezekano idadi ikaongezeka kutokana na tume yao kukosa taarifa. Hawa wamefanya kazi sehemu ndogo sana ya tatizo, hawajafikia watu hata asilimia 1 ya Watanzania wote. Inshort hii Tume hamna ilichofanya
 
Nilijua kutakuwa na huu upuuzi. Vifo 518 really?
Mkuu, mwenyekiti aliweka disclaimer kwamba hivyo ni vile tu walivyovithibitisha wao ila wale waliokufa majumbani na kuzikwa huko huko, ama walikufa na miili haikupatikana ama walikufa siku za mbeleni kutokana na majeraha ya tarehe 29 hawakuwa accounted. Hivyo wanaweza kuwa wamekufa maelfu ila sample yao imethibitisha 500+ nadhani ni jibu la kisiasa tu kuepuka mkono wa mabeberu
 
TBC UKWELI NA UWAZI

HGlXo-7WkAE0EjX.jpeg
 
Kwan hujasikia wamesema kuna baadhi waandamanaji walikuwa na silaha za moto.
Walisema? Wewe ulishaona picha ya muandamanaji akiwa na silaha, hata mmoja? Hivyo vilipuzi wanazungumzia viberiti au? Wao wanasema wameua watu 518 hao police 12 waliouawa ni akina nani na familia zao zipo wapi? Zaidi ya familia elfu 7 walijitokeza kuwa wapendwa wao hawajaonekana tangu hiyo siku ya uchaguzi......Wapo wapi? Waache kudanganya watanzania.......Watu wengi wamepoteza ndugu, rafiki yangu aliyepo Arusha amepoteza rafiki zake zaidi ya 25. Hii ni dhambi wanayofanya hii tume ya mchongo. Watusaidie kitu kimoja, watu waliopoteza wapendwa wao wajitokeze.....waache kutuchezea.
 
Na wao watakwambia kama kuna Askari unayemfahamu aliyeua muandamaji mtaje. Kingine ripoti haijataja waandamaji Mkuu,imesema wafanya Ghasia au Vurugu
Kasema maandamano yaligeuka kuwa vurugu.

Askari wanajulikana wengine walikuwa na uniform na force no zao.
 
Kama kuna watu wanasema kuna zaidi ya hao, hasa wanaharakati uchwara, ambao walikuwa na miezi zaidi ya 6 kuweka hata mtandao ambao watu wanakuja kuandika majina ya ndugu na jamaa waliopotea kipindi cha tarehe 29 mpaka 31, kwanini wameshindwa kufanya hivyo?
Badala ya kulalamika hio idadi ni ya uwongo?
 
Back
Top Bottom