PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sheria ya jeshi la polisi inaruhusu askari kubeba silaha lakini kutumia hiyo silaha kuna mwongozo wake sio kila tukio lazima silaha itumike.
Kwa hiyo tume wamekubali kuwa vifo vilisababishwa na polisi?

Kwa amri kutoka kwa nani?

Maadam sasa imebainika idadi ya vifo; inajulikana idadi na utambulisho wa waliosababisha vifo hivyo?

Ni polisi toka vituo gani waliohusika na mauaji haya!
 
Dah! Uenda waliokufa ni wengi sana basi! Mungu awarehemu! Kama tume ya sanaa imetaja idadi iyo,bas ni zaidi
 
Hiyo ndiyo kazi ya tume aliyoiunda, kupunguza madhara yaliyosababishwa na Ccm kwa mauaji yaliyotokea ikiwa pamoja na kupunguza idado ya mauaji.
Jaji Warioba alisema idadi ya waliokufa ni zaidi ya watanzania waliouawa wakati wa vita vya kagera tuanze kuchambua kuanzia hapo.
 
Wanaume: 490
Wanawake: 28
Askari: 16
Watoto: 21 Kati yao,
Miaka 15-17 walikuwa 15.
Miaka 7-10 walikuwa 4.
Chini ya miaka 5 walikuwa 2.

Vifo vingi vikiwa vimetobolewa na kitu chenye ncha kali yaani walipigwa risasi. Zaidi ya watu 700 walitekwa na kupotea wengine hadi leo hawajulikani.

Wengi walipigwa risasi wakiwa majumbani, madukani, sebuleni nk, hii inaonyesha ni matumizi mabaya ya vyombo vya usalama kinyume na sheria za kimataifa.

Sheria ya jeshi la polisi inaruhusu askari kubeba silaha lakini kutumia hiyo silaha kuna mwongozo wake sio kila tukio lazima silaha itumike.

Kwa mujibu wa shahidi kutoka Mwanza tume iliambiwa askari polisi waliwapiga risasi vijana 13 waliokuwa kwenye kibanda cha kuonyesha mpira.
Damu hizi za raia wasiokuwa na hatia ipo siku zitakuja kumuokotesha makopo Samuya.
 
Report inasemaje kuhusu nani aliwaua na kwa amri ya nani? mauaji 500 lazima wauaji wanajulikana watuambie kesi ianze na majina ya waliopotea 700 wayaweke wazi
 
Askari 16 waliuwawa, jiulize nani aliyewauwa.

Halafu kuna wapuuzi walitegemea Samia apelekwa ICC wakati zilikuwa vurugu zenye nia ya kuipindua serikali.
Nguruwe kuwa na akili za kujuwa wapuuzi, hilo haiwezekani.

Wauaji wengi kama siyo wote walivaa kiraia. Nguruwe kama wewe huwezi kujuwa kuwa hao hao ndio waliosababisha vifo vya wenzao; hasa ukijuwa KMKM nao walikuwa miongoni mwao?

Huyo mfugaji wako haepuki
 
Labda kama nimesikia vibaya.
Ila sina shaka na masikio yangu.
Wakati anaorodhesha silaha walizokuwa nazo "wafanya ghasia"
Silaha za moto pia ilikuwemo.
Na amesema waliouwa walichomwa na visu na mikuki na mishale maana hivyo ndivyo vitu vyenye ncha kali maarufu hapa tanzania kwa kuulia watu. Risasi sio kitu chenye ncha kali hicho ni kitu chenye baruti. Kwa hiyo chande ameona watu hawakupigwa risasi. Sasa hao walio uliwa na vitu vyenye ncha kali sijui waliwafukua wapi kuwafanyia post-mortem.
 
Uchunguzi huo wa kitaalam ulifanyika wapi na lini?
Walipopelekwa 'mortuary' sababu ilikuwa ni ya kufanyiwa huo uchunguzi kubaini sababu ya vifo, au ilikuwa ni mahali pa kuweka maiti kabla ya kupelekwa kwenye kaburi la halaiki?

Lakini hata risasi ni "nchakali" inapoingilia mwilini kabla ya hiyo baruti!
 
Unarukia hili unadhani ndilo litakalomwokoa mhalifu Samia kuwajibishwa kwa uhalifu wake.
Nanyi nyote mtakuwemo humo kwa kadri ya ushiriki wenu.
Hao walioua askari 16 sio wahalifu?. Unapokuwepo ushahidi wa aina hiyo hao ICC wanakuwa hawana sababu ya kuingilia kesi isiyowahusu.
 
Ewaaaaaa! Baaaamh!

Ukombozi umekaribia. No reverse imeenda hiyo.

Hii ndio habari ICC walikuwa wanasubiri.

Wamejitia kitanzi

Yajayo yanafurahisha…

Subiri majibu ya BBC CNN watakavyojibu

Hii Wanasema nzi kafia kwenye kidonda.

Wamejifunga wenyewe.
Huu ni Upuuzi tu
 
Nguruwe kuwa na akili za kujuwa wapuuzi, hilo haiwezekani.

Wauaji wengi kama siyo wote walivaa kiraia. Nguruwe kama wewe huwezi kujuwa kuwa hao hao ndio waliosababisha vifo vya wenzao; hasa ukijuwa KMKM nao walikuwa miongoni mwao?

Huyo mfugaji wako haepuki
Mapinduzi yenu yalidhibitiwa vizuri sana, mnapokuja kujiliza kwamba raia wengi waliuliwa mnakumbushwa kwamba hata askari waliuliwa na waliowaua wakavaa nguo za kiaskari wakaingia mitaani.

Vijana wa kitanzania pekee hawawezi kuwa na ujasiri mkubwa kiasi hicho, uzuri ni kwamba mfumo haufanyi kazi kwa presha za nguruwe wenye donge na nongwa vichwani kama Kalamu.
 
Back
Top Bottom