PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mimi nafahamu watu watatu walioliwa Geita
 
Nafikiri wao wameweka idadi ya taarifa walizokusanya, kuna sehemu mbele kasema upo uwezekano idadi ikaongezeka kutokana na tume yao kukosa taarifa. Hawa wamefanya kazi sehemu ndogo sana ya tatizo, hawajafikia watu hata asilimia 1 ya Watanzania wote. Inshort hii Tume hamna ilichofanya
 
Nilijua kutakuwa na huu upuuzi. Vifo 518 really?
Mkuu, mwenyekiti aliweka disclaimer kwamba hivyo ni vile tu walivyovithibitisha wao ila wale waliokufa majumbani na kuzikwa huko huko, ama walikufa na miili haikupatikana ama walikufa siku za mbeleni kutokana na majeraha ya tarehe 29 hawakuwa accounted. Hivyo wanaweza kuwa wamekufa maelfu ila sample yao imethibitisha 500+ nadhani ni jibu la kisiasa tu kuepuka mkono wa mabeberu
 
Kwan hujasikia wamesema kuna baadhi waandamanaji walikuwa na silaha za moto.
Walisema? Wewe ulishaona picha ya muandamanaji akiwa na silaha, hata mmoja? Hivyo vilipuzi wanazungumzia viberiti au? Wao wanasema wameua watu 518 hao police 12 waliouawa ni akina nani na familia zao zipo wapi? Zaidi ya familia elfu 7 walijitokeza kuwa wapendwa wao hawajaonekana tangu hiyo siku ya uchaguzi......Wapo wapi? Waache kudanganya watanzania.......Watu wengi wamepoteza ndugu, rafiki yangu aliyepo Arusha amepoteza rafiki zake zaidi ya 25. Hii ni dhambi wanayofanya hii tume ya mchongo. Watusaidie kitu kimoja, watu waliopoteza wapendwa wao wajitokeze.....waache kutuchezea.
 
Na wao watakwambia kama kuna Askari unayemfahamu aliyeua muandamaji mtaje. Kingine ripoti haijataja waandamaji Mkuu,imesema wafanya Ghasia au Vurugu
Kasema maandamano yaligeuka kuwa vurugu.

Askari wanajulikana wengine walikuwa na uniform na force no zao.
 
Kama kuna watu wanasema kuna zaidi ya hao, hasa wanaharakati uchwara, ambao walikuwa na miezi zaidi ya 6 kuweka hata mtandao ambao watu wanakuja kuandika majina ya ndugu na jamaa waliopotea kipindi cha tarehe 29 mpaka 31, kwanini wameshindwa kufanya hivyo?
Badala ya kulalamika hio idadi ni ya uwongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…