Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Ndugu zangu,
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa tena siku ya leo.

Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa hapa nchini, na kushuhudia chaguzi mbali mbali zikifanyika, mwaka huu umetengeza rekodi yake ya kipekee kabisa. Chadema, kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini, kimeshawahi kuwa na wagombea wa uraisi mbali mbali: (1) Mh. Mbowe; (2) Dr. Slaa; (3) Mh. Lowasa ambao hawakuwa na makando kando ya wazi ya kushirikiana na mabeberu.

Mwaka huu naona mbengu nyingine kabisa ambayo haijawahi kuonekana tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa vyama vingi vya siasa hapa nchini. Aidha, naishukuru tume kwa kumpitisha Mh. Tundu Lissu kupeperusha bendera ya chama hiki , maana wangemkata wangempa umaarufu ambao hastahili kuupata. Tangu Mh. Tundu Lissu arudi nchini, tumeshuhudia nyendo zake nyingi tu, zenye kujaa jeuri nyingi sana, kumbe jeuri hizi zinatokana mkono wa beberu nyuma yake (Amsterdam et al.,) ambao wanajulikana kote duniani kwa kutengeneza machafuko hasa katika vipindi vya uchanguzi mkuu wa nchi husika. Kwa ushirika huu wa Mh. Tundu Lissu na mabeberu hawa, sifa ya yeye kuwa kibaraka inamfaa kabisa. Ndugu watanzania wenangu, kumbukeni kuwa kibaraka yoyote yule, huwa haangalii maslahi ya nchi, bali yuko pale kwa ajili ya kulinda maslahi yake na mabeberu wake waliomtuma.

Kwa mtazamo wangu, Mh. Tundu Lissu anajua kabisa hawezi kuwa raisi wa nchi hii, ila amerejea kwa ajili ya kuleta amsha amsha tu. Aidha, kuna jambo nataka niwaeleze na mlijue; Tanzania ni mojawapo ya nchi pendwa sana na Mungu, maadui wetu huwa wanajaribu kila njia ili kuleta vurugu, lakini huwa hawafanikiwi. Kwa mfano, katika kipindi cha makinikia, Mh. Tundu Lissu alipiga kelele sana kwenye jambo hili, lakini mwisho wake serikali na Barick walikaa kwenye meza moja na kuja na kampuni ya Twiga (30:70% shares respectively), kwenye kukamatwa kwa ndegu huyu alikuwa anashangilia sana. Kwenye Korona napo mtu huyu na watu wake walipiga kelele sana, ila watanzania wengine na Mh. Raisi tulikuwa tunamtegemea Mungu, na hatimaye tukaibuka washindi katika hili.

Siku zote ukiwa mnafiki kwa taifa lako huwezi kufanikiwa, katika uchaguzi huu hakuna cha kibaraka, beberu au mtoto wake na beberu ambaye atafanikiwa na nchi itabaki salama na amani tele, na tutazidi kumuomba tena Mungu mchana na usiku ili kuhakikisha kuwa Ikulu ya Chamwino na Magogoni haigeuzwa kuwa pango la waporaji. Ikulu ya nchi hii, lazima akae raisi ambaye ana nia ya dhati ya kupigania maslahi ya watanzania kwa kulinda maliasili zake. Mimi nina imani kubwa sana Mh. Magufuli anaeda kushinda kwa kishindo kikubwa sana, na kuendelea kuongoza tena kwa miaka 5.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu
 
Nyie ndio mlikosea, mlidhani mkimpiga risasi angekufa, matokeo yake ameenda kutibiwa na hao mabeberu akapona, ndio maana mnawachukia mabeberu.

Sijui wewe mjinga ulitaka Lissu awasifie kwa lipi?!
 
Hiyo chamwino igeuzwe pango la waporaji mara ngapi? kwani ile 1.5 T haikuporwa

Beberu sio rangi, beberu ni vitendo. yanayofanywa na nduguzo ni ubeberu pia
 
Badala ya kushuhudia mgombea dikteta uchwara we unashuhudia upuuzi.

Huyu uchwara alidhabi atadumu milele sasa mwisho wake umefika.
 
Tulia mama, hujaingia leba ushaaza kupiga makelele.
 
Tokea mlipokosa shabaha ya kumwua kwa Risasi 16 zilizopenya kwenye mwili wa Mwanadamu aitwaye Tundu Lissu, sasa mnatengeneza taarifa nyingi za kijinga na kuweweseka, si muda mrefu mtaanza kutajana mlioshiriki Mpango huu ovu.
 
Nyie ndio mlikosea, mlidhani mkimpiga risasi angekufa, matokeo yake ameenda kutibiwa na hao mabeberu akapona, ndio maana mnawachukia mabeberu.

Sijui wewe mjinga ulitaka Lissu awasifie kwa lipi?!
Umemaliza hujasaza hata mboga buddy
 
Kwa mara ya kwanza tangu uasisi wa vyama vingi 1992, nchi yetu inakaribia kumpata Mgombea wa Upinzani ambaye ni Mpinzani HALISI, ila mimi nitamwita mwana SERA MBADALA HALISI.

Bado massa mawili tu kufika saa 10 kamili tu kama kutakuwa hakuna pingamizi lolote, maombi yenu yanahitajika.
 
Ndugu zangu,
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa tena siku ya leo.

Tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa hapa nchini, na kushuhudia chaguzi mbali mbali zikifanyika, mwaka huu umetengeza rekodi yake ya kipekee kabisa. Chadema, kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini, kimeshawahi kuwa na wagombea wa uraisi mbali mbali: (1) Mh. Mbowe; (2) Dr. Slaa; (3) Mh. Lowasa ambao hawakuwa na makando kando ya wazi ya kushirikiana na mabeberu.

Mwaka huu naona mbengu nyingine kabisa ambayo haijawahi kuonekana tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa vyama vingi vya siasa hapa nchini. Aidha, naishukuru tume kwa kumpitisha Mh. Tundu Lissu kupeperusha bendera ya chama hiki , maana wangemkata wangempa umaarufu ambao hastahili kuupata. Tangu Mh. Tundu Lissu arudi nchini, tumeshuhudia nyendo zake nyingi tu, zenye kujaa jeuri nyingi sana, kumbe jeuri hizi zinatokana mkono wa beberu nyuma yake (Amsterdam et al.,) ambao wanajulikana kote duniani kwa kutengeneza machafuko hasa katika vipindi vya uchanguzi mkuu wa nchi husika. Kwa ushirika huu wa Mh. Tundu Lissu na mabeberu hawa, sifa ya yeye kuwa kibaraka inamfaa kabisa. Ndugu watanzania wenangu, kumbukeni kuwa kibaraka yoyote yule, huwa haangalii maslahi ya nchi, bali yuko pale kwa ajili ya kulinda maslahi yake na mabeberu wake waliomtuma.

Kwa mtazamo wangu, Mh. Tundu Lissu anajua kabisa hawezi kuwa raisi wa nchi hii, ila amerejea kwa ajili ya kuleta amsha amsha tu. Aidha, kuna jambo nataka niwaeleze na mlijue; Tanzania ni mojawapo ya nchi pendwa sana na Mungu, maadui wetu huwa wanajaribu kila njia ili kuleta vurugu, lakini huwa hawafanikiwi. Kwa mfano, katika kipindi cha makinikia, Mh. Tundu Lissu alipiga kelele sana kwenye jambo hili, lakini mwisho wake serikali na Barick walikaa kwenye meza moja na kuja na kampuni ya Twiga (30:70% shares respectively), kwenye kukamatwa kwa ndegu huyu alikuwa anashangilia sana. Kwenye Korona napo mtu huyu na watu wake walipiga kelele sana, ila watanzania wengine na Mh. Raisi tulikuwa tunamtegemea Mungu, na hatimaye tukaibuka washindi katika hili.

Siku zote ukiwa mnafiki kwa taifa lako huwezi kufanikiwa, katika uchaguzi huu hakuna cha kibaraka, beberu au mtoto wake na beberu ambaye atafanikiwa na nchi itabaki salama na amani tele, na tutazidi kumuomba tena Mungu mchana na usiku ili kuhakikisha kuwa Ikulu ya Chamwino na Magogoni haigeuzwa kuwa pango la waporaji. Ikulu ya nchi hii, lazima akae raisi ambaye ana nia ya dhati ya kupigania maslahi ya watanzania kwa kulinda maliasili zake. Mimi nina imani kubwa sana Mh. Magufuli anaeda kushinda kwa kishindo kikubwa sana, na kuendelea kuongoza tena kwa miaka 5.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu

Ukiona mtu anasherehekea nchi yake inapopatwa na shida au hata kufanya juhudi za wazi kuitumbukiza nchi yake kwenye shida, ujue huyo mtu hafai hata kuwa kiongozi wa kitongoji!
 
Nadhani kumaliza mizozo na sintofahamu serikali na Jeshi la polisi wangelitoa msimamo wa kilichomkuta ile siku na kama wanafahamika sheria ichukue mkondo wake ili haya maizauza ya ubaya yamalizwe. Tanzania ni yetu sote na haki ya kuishi ni ya Mungu pekee.
 
Back
Top Bottom