Tumemaliza rasmi ubishi wa nani zaidi kati ya Messi na Cr7

Tumemaliza rasmi ubishi wa nani zaidi kati ya Messi na Cr7

Messi yupo class ya peke yake, an exceptional player.

Halafu ndio wale wengine wajipange akina Pele, Maradona, Zidane, Ronaldinho, Ronaldo de lima, Christiano Ronaldo, Beckeunbauer, di Stefano, Platini nk
Kila moja kwa wakati wake.
Huwezi kuwalinganisha
 
Umeuliza Messi amefanya nini kingine tofauti na magoli aliyofunga. Nimekuletea takwimu kujibu swali lako, unaniita mshamba na kuniletea habari za Cuadrado.

Hapo ni nani mshamba kati ya mimi na wewe?
Mshamba wew ambaye unadai Messi ni mchezaji mkubwa afu unaleta rekodi za kitoto ambazo Ata wachezaji wakawaida wamezifika ndio nikakupa mfano wa Juan alifikia hiyo rekodi Yako ya assist tatu sjui mbili ili uelewe
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Tatizo la wabongo Kuna ugonjwa fulani unatusumbua.Yaan mtu akifunga goli au akicheza vizuri ,atapewa sifa zote kama vile hatujawahi kuona wachezaji wengine wazuri.Hata hapa nyumbani tu.Kuna mchezaji anaitwa Chama au Morrison wakicheza vizuri yaan sifa zinakuwa nyingi sana kuliko mchezaji mwenyewe.Utasikia hapa bongo haijawahi kutokea mchezaji Kama huyu.Yaan upumbavu mtupu.So far sijaona ubora wa Messi .Yaan ni Kama kubahatisha tu.Ukiwaona Croatia ni wazuri sana kuliko Messi na Argentina.Aidha kwa umri wangu nimeona Maradona akicheza mpira.Sioni Kama Messi anamfikia.Kama Messi ndio bora basi tumerudi nyuma sana.
 
Kama unadhan mpira rahisi kacheze,heshima kitu cha bure na LAPUGA apewe heshima yake
Ukiwauliza uyo Messi ukitoa Goli za penati za kupewa kafanya kitu Gani zaidi ya hapo watakwambia anapiga chenga sana uwanjani Messi imefika time anapiga chenga hadi anadondoka mwenyewe kitu alichobakinayo Messi Kwa Sasa ni uwezo wa kuficha mpira tu ila speed,Goal score ,assist kashuka sana kama Kuna mtu anajua mpira apa aje tumpe takwimu za Messi Toka 2004
 
Kuna tofauti kati ya kibarua saidia fundi na fundi mwenyewe cr7 ni kibarua aliejituma katika kazi, na messi always ni fundi
 
Kumbe we united ya Ferguson????lazima uweweseke na huyu kiumbe kwa kile alichowafanyia Wembley 2019 mpaka babu yenu akapatwa na degedege
2019 Ferguson alikua Manchester unaona ulivo mbovu kweny rekodi za mpira inawezekana Ata Messi umeanza kumtizama miaka ya 2020
 
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Ujinga wako wa kipumbavu umebase kwenye uchawa zaidi .Angalia mpira fanya interpretation sio uchawa.Tanzania tunapenda kusifia sifia tu .Hata ujinga tunasifia.Hili Taifa la watu wa ajabu sana.
 
Anaejua anajua tu,co lazima umkubali ww ucwe mjinga wa kiwango cha SGR
Ujinga wako wa kipumbavu umebase kwenye uchawa zaidi .Angalia mpira fanya interpretation sio uchawa.Tanzania tunapenda kusifia sifia tu .Hata ujinga tunasifia.Hili Taifa la watu wa ajabu sana.
 
Anaejua anajua tu,co lazima umkubali ww ucwe mjinga wa kiwango cha SGR
Jenga hoja sio matusi.Yaan matusi yako yanadhihirisha uwezo wako mdogo.Yaan siku hizi humu JF kuna vilaza tupu na watu waliofrustrate.Its a rare case to meet with unknown who can cement strong ideas and point.
 
Messi yupo class ya peke yake, an exceptional player.

Halafu ndio wale wengine wajipange akina Pele, Maradona, Zidane, Ronaldinho, Ronaldo de lima, Christiano Ronaldo, Beckeunbauer, di Stefano, Platini nk
Huwa siwaelewi mtu anayembeza Gaucho...ni ama hakuwahi mshuhudia kwa muda murefu kwa sababu ya changamoto za teknolojia muda ule, ama amemshuhudia wakati anaelekea ukingoni!

Gaucho alikuwa anacheza kwa passion, spirit na kutoa burudani kwa watazamaji kitu ambacho hao wengine hawana!
 
Kuwa mjinga co tuc,ni kutojua tu uhalisia wa mambo
Jenga hoja sio matusi.Yaan matusi yako yanadhihirisha uwezo wako mdogo.Yaan siku hizi humu JF kuna vilaza tupu na watu waliofrustrate.Its a rare case to meet with unknown who can cement strong ideas and point.
 
Lakini huwez kufanya huo Ulinganishaji ..
CR ni Messi + 3 Age.

CR at his Prime na Leon at his Prime ilikuwa haieleweki who is the be/t.

Lakin walikuwa wakipishanapishana katika ubora. Ni best players kwa miaka 15 iliyopita.

Ni jokes kumdharau CR kwa kiwango cha sasa. Umri umeshamchapa kaka
Hata vipaji vyao kuanza kudhihirika ilikuwa ni tofauti sana, Messi alianza kukiwasha akiwa na 19, akaweka Hat Trick dhidi ya Madrid ilokuwa na mastar kibao.

Ronaldo akiwa na 19 hata haifahamiki kama atakuwa kuja mtu wa namna gani. Achana na Messi, Messi kile ni kipaji halisi cha mpira.
 
06eaf094060456abe34cd4e17ddc6fe1.jpg

Lionel Messi bado anaendelea kuvunja rekodi tangu afanikiwe kutwaa Kombe la Dunia kupitia Kikosi cha Timu ya Taifa ya Argentina.

Fowadi huyo wa Pari Saint-Germain na Argentina sio tu kwamba ndiye mwanasoka anayezungumziwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa lakini pia picha yake akinyanyua taji la Kombe la Dunia imeweka rekodi ya kipekee huko Instagram.

Picha ya Messi kwenye ukurasa wake wa Instagram akinyanyua taji hilo ilikuwa imevutia watu 69,901,173 hadi kufikia Desemba 21, 2022 saa 2 usiku.

Chapisho hilo pia lilikuwa na maoni 1,890,993 huku mashabiki wengi wakimpongeza nyota huyo wa soka kwa kuweka rekodi ya kipekee.

Mataji ambayo Messi ameshinda katika maisha yake ya soka

Bingwa wa Kombe la Dunia: Argentina, 2022

Bingwa wa Copa America: Argentina, 2021

Bingwa wa Olimpiki: Argentina, 2008

Mabao mengi kwa Argentina: 98

Mechi nyingi zaidi za Argentina: 172

Mpira wa Dhahabu wa Kombe la Dunia: Argentina, 2014, 2022

Mchezaji Bora wa Copa America: Argentina, 2015, 2021

Mchezaji Bora wa Kiume wa Muongo wa Dunia: 2011-2020

Mchezaji mdogo zaidi kufunga katika mechi ya Kombe la Dunia

Tuzo nyingi za Mwanasoka Bora wa Mechi katika Kombe la Dunia: 11

Mechi nyingi za Kombe la Dunia akiwa nahodha: 19

Ballons d’Or Nyingi zaidi katika historia: 7 (2021, 2019, 2015, 2012, 2011, 2010, 2009)

Tuzo nyingi zaidi za Mchezaji Bora wa Mechi ya Kombe la Dunia: 10 (2010, 2014, 2018, 2022)

Mshindi wa Kiatu cha Dhahabu cha Ulaya: 6 (2010, 2012, 2013, 2017, 2018, 2019)

Mshindi mara 10 wa La Liga: Barcelona

Mshindi Mara 4 wa UEFA Champions League: Barcelona

Mshindi Mara 1 League 1: Paris Saint-Germain

Mabao ya pili kwa Ligi ya Mabingwa: 129

Mabao mengi zaidi katika historia ya La Liga: 474

Mshindi Mara 15 Mfululizo wa tuzo za FIFA za XI Bora Duniani: 2007-2021

Magoli ya Klabu: 695

Assist za Klabu: 332

Magoli Timu ya Taifa - 98

Career assists, club: 55
 
Maoni yanaweza kutofautiana katika mjadala wa "Mchezaji bora wa muda wote" (G.O.A.T), lakini itakuvutia kujua kuwa Messi sasa ameshinda zaidi ya miamba ya soka Pele na Maradona walivyowahi kushinda!

Lionel Messi amemaliza ukame wa makombe ya soka, na kushinda mataji yote ya klabu na makubwa ya nchi.

Ukimlinganisha na Pele. Licha ya kushinda rekodi ya mataji 3 ya Kombe la Dunia, Pele hakuwahi kushinda Copa America. 'O Rei' ('The King') alicheza Copa America moja pekee mwaka wa 1959. Alifunga 8 katika michezo 6, lakini akashindwa katika fainali na vijana mahiri wa kiArgentina.

Ukimlinganisha na Maradona. Diego Maradona pia hakuwahi kushinda Copa America. Aliiwakilisha Argentina katika Copa ya 1979 na akatupwa nje, akakosa katika mashindano ya 1983 kutokana na jeraha, akarejea 1987 na 1989 na akatupwa nje. Alifeli majaribio ya kutumia dawa za kulevya mwaka 1991 na akasimamishwa kuitumikia timu yake ya taifa, kabla ya Argentina kushinda Copa mwaka huo. Maradona hata alipokuwa ameenda kucheza barani Ulaya, licha ya kuwa bora lakini hajawahi kushinda kombe kubwa zaidi kwa vilabu ambalo ni Ligi ya Mabingwa.

Kuhusu Cristiano Ronaldo, kinyota kitawekwa kwenye jina lake kila wakati kwenye mjadala wa Mchezaji wa muda wote (GOAT) kwa sababu bado hajashinda Kombe la Dunia ambalo ni kombe kubwa sana katika soka.

Jumapili ya 18/12/2022, Messi alimaliza soka. Sasa ameshinda kila ubingwa kwa klabu na nchi, jambo ambalo washindani wenzake katika mzani wa "GOAT" hawawezi kujivunia.

Hii inaacha maswali ya mtu kujiuliza, "Ni nini kingine kinachoweza kuulizwa kwa Messi ambacho hana?"

Mafanikio yake binafsi pia ni kitu kinachomuongezea nguvu katika mjadala huu. Kwa kuzitaja chache ni
~ Kashinda Baron Dior nyingi zaidi ya wote (7).
~ Golden ball nyingi zaidi ya washindani wake.
~ Mchezaji wa kwanza kuchukua mchezaji bora wa kombe la dunia mara mbili.
~ Play maker award mara 6.

Kwa vigezo hivyo, Messi atasalia kuwa mchezaji bora wa kizazi kilichopita, hiki cha sasa na kinachokuja.

Credit: Ritchie Mdugo (Fb)
FB_IMG_1671729578483.jpg
 
Back
Top Bottom