Tumeshawaambia msisafiri na familia nzima katika gari moja ila hamsikii

Tumeshawaambia msisafiri na familia nzima katika gari moja ila hamsikii

Kusafiri pamoja hakuna tatizo kabisa.Tatizo ni ubovu wa barabara,uzoefu mdogo wa kuendesha gari masaa mengi na uzembe wa baadhi wa madereva barabarani hasa hawa wa magari makubwa kama Lori na mabasi.Mtu kama hujazoea kuendesha gari masaa mengi Mfano utoke dar Hadi mwanza Bora utafute dereva mwenye akili timamu mwenye uzoefu na kufuata Sheria za usalama barabarani
Walau madereva wawili....wife anaendesha hadi Chalinze akichoka unachukua hadi kipande fulani.


Tatizo lingine mkuu ni hawa jamaa hawajawahi kuendeshs safari ndefu safari zao ni za ndani ya Dar na muda mwingi wanaendeshwa.
 
Walau madereva wawili....wife anaendesha hadi Chalinze akichoka unachukua hadi kipande fulani.


Tatizo lingine mkuu ni hawa jamaa hawajawahi kuendeshs safari ndefu safari zao ni za ndani ya Dar na muda mwingi wanaendeshwa.
Sahihi kabisa.tatizo kubwa ni uzoefu wa safari ndefu.
 
Watz ni watu wajinga Sana .

Tulishawaambia kuwa wasisafiri na gari moja Kama familia nzima.

Baba
Mama
Watoto

Hawa wote unawakuta wanapanda gari moja na ikitokea ajari wanafariki wote.


Tumewawapa Sana onyo na masomo na upo Uzi upo umu JF.
Kutosafiri kwenye gari moja, nayo inautata. Yaani tunapoenda kijijini, ndio tupande magari tofauti. Ila tukiwa hapa mjini, mfano tunaenda ibadani, kwenye mkutano, tunaweza kupanda gari moja?
Anyway, Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awajalie majeruhi nafuu ya haraka.

Risk factors za ajali za Bongo, ni pamoja kutumia chombo cha usafiri kwenye barabara zetu, regardless unaendesha, unaendeshwa, mko wengi au mko wachache. Uwezekano wa kupata ajali kwenye nchi hii ni mkubwa kuliko familia hiyo hiyo ingekuwa inasafiri kwenye gari moja ndani ya Canada au UK au USA.
 
Asafiri na mtu mzoefu wa safari ndefu, aendeshe say dar hadi mkata then mwingine ashike hadi mombo, toka mombo hadi same...then mwingine amalizoe safari. Kwa mtu wa kujifunza safari moja inatosha kabisa.
Upo sahihi lakini uzoefu unapatikana kwa kujaribu tena mara kwa Mara kwa mtazamo wangu ukishajua basic za kuendesha gari na kufuata sheria za usalama barabarani basi possibility ya kufika salama ni kubwa.
 
Kwa mujibu wa imanu yangu hakuna aliyewahi kumuona Mungu,wewe pia unaweza kuamini unachoamini.
Kama hujawahi kumwona unathibitishaje kuwa huwa anapanga. Hizi stori za alipangalo Mungu huwezi kukwepa ni jitihada za binadamu kukwepa kuwajibika kwa makosa yake. Ajali zinazotokea nyingi zinasababishwa na uzembe wa watumiaji wa barabara na vyombo vya moto...
 
Mipango yote anapanga Maulana. Akiamua utangulie kwenye haki hata ajali ndogo kwa macho utaitika wito tu, akiamua usiitike siku hiyo unatoka mzima kwenye ajali inayogeuza gari jipya kuwa chuma chakavu....

RIP Nko Bwana ahimidiwe.
Siyo mipango yote
 
Marehemu hasemwi ila nimejisikia vibaya sana. Watoto wamefunga shule tokea mwezi wa 12 mwanzoni, kwann wasitangulie na mama yao?
Mkuu kuna vibe kubwa Sana kutembea na familia ingawa kuna risks kubwa....nami pia nimesafiri na familia tuombeane Tu turudi salama
 
Watz ni watu wajinga Sana .

Tulishawaambia kuwa wasisafiri na gari moja Kama familia nzima.

Baba
Mama
Watoto

Hawa wote unawakuta wanapanda gari moja na ikitokea ajari wanafariki wote.


Tumewawapa Sana onyo na masomo na upo Uzi upo umu JF.
Huu ni uposhaji. Laiti ungejua idadi ya familia zinazosafiri kwa pamoja usingeandika haya. Kwa taarifa yako karibu kila gari la binafsi linalosafiri kwenda holidays kama hii limebeba watu wa familia moja. Hii ni bahati mbaya tu au sahihi niseme ni uzembe uliofanywa dereva/madereva.
 
Mwenyezi Mungu akipanga lake huwezi kulikwepa hata iweje,kikubwa tuwaombee heri huko waendako na tuwape pole wafiwa na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa.
Pia tuendelee kukumbushana kuishi vyema hapa duniani tusifanyiane husuda na roho mbaya bali tuishi kwa kutendeana vyema kwani maisha ya duniani ni mafupi sana.
Hakuna Mungu anayepanga ajali.

Hebu acheni hizi mentality za kijinga.

Hii Tanzania watu wanakufa sanasana kutokana na ujinga, uzembe na umaskini.
 
Msiba ungekua mdogo.
kaka haya mambo hayaendi hivyo, Unaweza kukataa kupanda gari na familia yako, ukawaambia wapande gari nyingine, huko ndio wakaenda kufa. Unakuwa umewapeleka kwenye kifo.
Nje ya mada, nina milion saba bro, niongeze mpaka ngapi nipate gari Hybrid nzuri hapa TZ?
 
Marehemu hasemwi ila nimejisikia vibaya sana. Watoto wamefunga shule tokea mwezi wa 12 mwanzoni, kwann wasitangulie na mama yao?
Mkuu sidhani kama amefanya vibaya. Ni vizuri kusafiri na familia yako hasa kipindi hiki. Nmemwambia mwanzisha thread kuwa idadi ya family zinazosafiri kwenye gari moja kipindi kama hiki ni nyingi mno. Karibu kila gari linakuwa limebeba familia au ndugu wa karibu. Tunasafiri kwenda kwenye misiba tukiwa watu wengi zaidi kwenye gari moja, pengine familia hata 5. Kwa kifupi tukio la familia moja kufariki wote kwenye ajali ni adimu kulinganisha na idadi ya wanaosafiri. Muhimu ni kila dereva kuwa makini na kuzingatia sheria hasa kuchunga mwendokasi. Tukiwa na mawazo kama haya tunaweza tunajikuta tunasema familia moja isilale nyumba moja kwa sababu moto ukitokea wanaweza kuteketea wote.
 
Back
Top Bottom