Wasambaa wametisha sana ๐ฅ
Udongo mwekunduuMAJI MAJI YA SONGEA : JUU (KUSHOTO) NI Golikipa Shaibu Kambangwa, David Mjanja, Omar Kapilima, Godfrey Kikumbizi, James Mhagama, Steven Mapunda "Garrincha" John Alex Lwena, Kelvin Haule (RIP) na Golikipa Doyi Moke (RIP). . . CHINI (KUSHOTO) NI Fortunatus Dello Ntumba, Omar Hussein, Willy Martin, Said Mshamu, Samson Paul, Hamisi Ngwena na Amri Said "Stam"View attachment 3596337
Duh ni zamani sana miaka ya 60๐Wengi wetu tunalijua hili duka wakati linaitwa Tanzania Elimu Supplies.Lilikuwa katikati ya iliyokuwa Salamander hotel na Posta ya zamani.
Duka lilikuwa kubwa la stationery na wenyewe walikuwa the Kanti brothers.
Ghafla katika miaka ya sitini hawa ndugu na familia zao walipewa masaa 48 waondoke nchini.
Sababu zilizozagaa mtaani ni kwamba wakishirikiana na ubalozi fulani walikuwa wanaingiza bidhaa bila kulipa kodi.
Sababu ingine ambayo ilishika kasi
Kawawa aliingia kwenye hili duka akitaka kununua pen aina ya Parker ambayo ni expensive.Kukatokea mzozo haijulikani kama Kawawa alitaka kuichukua bure au wenye duka walileta dharau.
Kilichofuata wahindi waliwekwa ndani na kesho yake na familia zao wakapakiwa kwenye ndege kuelekea Uingereza.
Duka likawa la umma Tanzania Elimu Supplies.View attachment 3601850
KWA NINI TUZIKE HISTORIA YA TANGANYIKA?
Baada ya kuanzishwa TANU, Rais wa TANU wa wakati huo, Julius Nyerere alizunguka katika eneo lote la Tanganyika kuwaomba watawala wa maeneo mbalimbali wajiunge na Shirikisho la Tanganyika. Unajua kwa nini Nyerere alifanya hivyo?
Eneo lote la Tanganyika lilikuwa ni nchi moja chini ya Wajerumani. Ila baada ya Wajerumani kushindwa na Waingereza katika Vita Kuu ya I ya Dunia mwaka 1919, eneo lote hili liliwekwa chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa kwa masharti kwamba Watanganyika watakapofika wakati wa kujitawala wapewa nchi yao. Hivyo, Uingereza ilipewa kuwa mwangalizi tu.
Hivyo masharti ya kupata uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni lazima uwe uhuru wa nchi moja kwa taifa zima la Tanganyika. Ndio sababu Mangi Marealle wa Moshi alipokwenda kule Umoja wa kudai Uhuru wa Wachagga (Kilimanjaro) pekee alikataliwa pamoja na ukweli kuwa Kilimanjaro ilikuwa na sifa zote za kuwa nchi inayojitawala.
Lakini pia, kama baadhi ya maeneo yangekataa na kusema kuwa hayakuwa tayari kwa uhuru, Uingereza isingetoa uhuru kwa Tanganyika. Hii ndio sababu iliyomfanya Julius Nyerere kupita kila eneo kushawishi machifu (watawala wa makabila) mbalimbali kuweka mamlaka yao kwa TANU. Ndio maana baada ya uhuru watoto wengi wa machifu walipewa nafasi serikalini kwa sababu ilikuwa sehemu ya makubaliano kati ya Nyerere (TANU) na baba zao ya kuwa watoto wao watapewa uchifu katika maeneo mengine.
Milki (tawala) zote mbili za Chifu Mwamakula, Utawala wa Mwaya chini ya Chifu Mwakalukwa Mwamakula na Utawala wa Kajunjemele chini ya Chifu Korosso Mwamakula tulitoa mamlaka yetu kwa TANU chini ya Rais Julius Nyerere.
Nyerere alichukua sahihi za machifu wote na kuziwasilisha kwa watawala wa Kiingereza na pia Umoja wa Mataifa kuwa Watanganyika kwa umoja wao wako tayari kujitawala. Hiyo ndiyo njia iliyotumika kudai Uhuru wa Tanganyika bila ya kumwaga damu kama Kenya na kwingineko.
Leo nilikuwa naangalia sarafu tatu za shilingi ya Tanzania: sarafu ya shilingi mia moja, sarafu ya shilingi mia mbili na pia sarafu ya shilingi mia tano. Nilibaini kuwa sarafu hizo kuna iliyo na picha ya Julius Nyerere na pia kuna iliyo na picha ya Sheikh Abeid Amani Karume.
Kilichonishangaza ni kuwa Julius Nyerere yeye kuelezwa kuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania wakati Karume kaelezwa kuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar. Historia yetu imefukiwa chini ya ardhi mchana kweupe. Sijajua unyama huo wa kuifukia na kuizika historia yetu ulifanywa kwa makusudi au ilikuwa ni 'umbumbumbu' wetu.
Kwa sababu ya kufukiwa kwa historia hiyo, leo kuna watu wananyanyapaliwa kwa wao kutaja majina ya Tanganyika na Zanzibar. Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza kaelezea katika ukurasa wake jinsi alivyotukanwa kwa kutumia historia hiyo.
Lakini pia ni makosa makubwa kuufuta kabisa utambulisho na historia ya nchi iliyo kwenye muungano au shirikisho. Historia inaonyesha kuwa mashirikisho mengi duniani zikiwemo nchi za muungano viliparaganyika na watu wa nchi zilizokuwa katika muungano, mashirikisho au umoja wakarudia mipaka yao na pia historia zao. Mifano hiyo ni kama Muungano wa Nchi za Kisovieti (USSR au Urusi), Muungano wa Nchi za Yugoslavia, Muungano wa Nchi za Sudan, Muungano wa Nchi Ethiopia, nk.
Wakati muungano wa nchi za Yugoslavia ukiwa katika hali kusambaratika kulitokea mapigano makali sana kwa sababu maeneo mengine pia yalikuwa na utata wa kihistoria na mipaka. Ni vizuri historia ya Tanganyika isiharibiwe, lakini pia ni vizuri historia na mipaka ya nchi ambazo ziliunda shirikisho la Tanganyika visiharibiwe.
Lakini pia, wakati Uganda walipoandika katiba yao kwa upya na kuitambua mipaka ya asili na tawala za asili, haukuwa shida kutambua pia mipaka ya tawala za Baganda, Banyoro, nk. Muungano ulio imara ni ule ambao kila mmoja anajua asili na historia yake. Lakini leo sehemu moja ya huu Muungano wa Tanzania hawaijui kabisa historia yao wakati sehemu nyingine wanaijua na wanafufua kila kitu cha kwao!
Kuyanyamazia haya ni kuahirisha matatizo ili kuyaacha yawe makubwa zaidi. Mzazi mwema na aliye na hekima ni yule anayehakikisha ya kuwa matatizo ya wakati wake anayatatua yote ili asiwarishishe watoto wake matatizo yake.
Leo tumefika mahali viongozi kutoka upande mmoja wa Muungano wanaongea hadharani kuwa ajira zote zilizo katika upande wa nchi yao ziwe kwa ajili wazawa wa sehemu ile tu wakati ajira za upande mwingine hutolewa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi. Wakati upande mmoja wa Muungano wanajuana hadi kifamilia lakini upande mwingine wanaijua historia ya Chifu Mkwawa wa Wahehe, Mtemi Mirambo wa Tabora na Kinjikitile Ngware wa Ngarambe tu.
Historia nyingine za tawala zetu zimefukiwa kiasi kwamba watoto wetu wakiambiwa juu watemi na machifu wa Tanganyika wanafikiri kuwa unawaambia kuhusu waganga wa jadi, wachawi, wapiga ramli na waaguzi. Wenzetu huko Ulaya wametunza historia za watawala wao wa tangu kabla ya Yesu, lakini sisi huku tunaifukia historia ya miaka 60 iliyopita. Je, huu ni ustaarabu gani wa kuua historia? Lakini huu ni uongozi gani wa kufukia misingi ya historia iliyounda nchi yetu?
Lakini kulikuwa na dhambi gani kuweka sarafu moja itaje Rais wa Kwanza wa Tanganyika? Na huo si ndio ukweli wenyewe? Tunamdanganya nani kwa maslahi ya nani? Je, tunamridhisha nani kwa maslahi ya nani hasa? Kuyafumbia masuala madogo haya kunajenga hisia, chuki na wivu wa vuguvugu la kujikomboa upande ambao unaona kuwa historia yake inafukiwa na vuguvugu hilo linaweza kuwa na athari mbaya sana kwa muungano wetu. Kile kitu ambacho tunafikiri tunakilinda, tutajikuta tunakibomoa kwa mikono yetu wetu kama yule mwanamke mpumbavu wa kwenye Biblia (Mithali 14:1).
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 9 Juni 2026; Saa 8:00 usiku wa mananeView attachment 3604458
Shukrani sana kaka mshana kwa kuendelea kutukumbusha.KWA NINI TUZIKE HISTORIA YA TANGANYIKA?