Tumetoka mbali: Mada maalum ya matukio ya zamani

Hili ni kanisa walilolichoma makoloni huko Meru 1951.
Maaskari wa kikoloni walichoma nyumba za Wameru, mifugo na vyakula stoo. Wakachoma kanisa na kuamisha watu Kwa nguvu.

Mama mmoja alikuwa anajifungua, wakakataa kumpa nafasi ya kujifungua, akaenda msituni na akafia huko.

Kitabu Cha Kirilo Japhet Ayo 1966.
 
MWADUI ILIKUWA ZAIDI YA MGODI.

Kwa waliokulia au kusoma shule katika mgodi wa Williamson Mwadui watakubaliana na mimi kuwa mwadui ilikuwa zaidi ya Mgodi. Hii picha ilipigwa October 1974

Vijana wa mwadui Primary School Brass Band kutoka kulia wa kwanza ni Magani Machege ( morgan machege) , Kizito Albert Mbunda ( Zito Albert Mbunda) huyo dada Balandya Mwl. Kasoyaga, Benedictor Julius( Betto Julius Pacheco, aliefuata jina limesahaulika , mwisho Head Master Mwl. Mchaina.

Hayo majina kwenye blaketi ni majina ya kimuziki kwani vijana hao walikuja kutamba kwenye tasnia ya muziki na bendi mbalimbali nchini walianzia Safari Trippers ya Marijani Rajabu, Ottu/Juwata Jazz Band, Maquis Du Zaire. Morgan Machege alipiga muziki hadi kenya na Orchestra Le Mangelepa (wana sindano ya moto) huyo dada alibakia Polisi Brass Band mpaka alipostaafu. Watatu hao wote hatunao wameshatangulia mbele ya haki.

Kwa wapenzi wa msiki wa ndansi hayo majina siyo mageni, je ulikuwa unatambua kuwa hawa watu walitokea mwadui?

Njile Nkuba Sitta 0788 199 994
 
Ni kweli kuwa Charles Dundas alishawahi kuishi tengeru?
Hapana, si kweli kuwa Charles Dundas alishawahi kuishi Tengeru.
Sir Charles Dundas, ambaye alikuwa mtawala wa kikoloni wa Uingereza, aliishi na kufanya kazi zake kwa karibu zaidi katika maeneo ya Moshi na Kilimanjaro.
Alihudumu kama Kamishna wa Wilaya (District Commissioner) wa eneo la Moshi katika miaka ya 1920.
 
Mama Randi wangu. Na mimi.
Tumetoka mbali. Miaka 18; bila ugomvi wala mabishano. Allah Baarickllana!!
Zahir Ally Zoro
 
Shukrani kwa response
 
Mji Mkongwe wa Zanzibar enzi za zamani .
 
Mitaani Mji Mkongwe wa Zanzibar katika miaka ya 1970s .
 
Mpango Wa Jeshi La Tanzania Kuikomboa Uganda 14 September 1972 Na Ndege Ya DC-9 Documentary History #reels #reelsviralシ #Uganda #aviation #tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…