Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Yaani wengi watadhani ni as mulizi tu za Jomba Buji, lakini huku ndiko haswa tulikotoka

1. NGOMA YA MDUNDIKO
Zama zile MDUNDIKO ulipita mtaa kwa mtaa jijini, ni mwendo mpwitompwito, nyimbo, ngoma, matusi, mikatiko, yaani kivumbi na jasho, unatoka kwenu Buguruni unajikuta uko Kawe Mzimuni, na nauli huna.

2. JIWE LA FATUMA
Mmelala ndani mnasikia nje watu wanahesabu, moja, mbili taaaaaaaat. Kabla hawajamaliza kuhesabu mnaliona jiwe kubwa sana love naingia ndani, mlango umesambaratishwa, njemba za miraba minne kama Tisa, mapanga yameremetayo yenye makali kuwili yako standby kusambaratisha nyama za miili yenu, MNA music system wanabeba, TV set inaondoka, cheni na vidani vya dhahabu si Mali yenu tena.

Shukrani kwa Augustino Lyatonga Mrema

3. MAGARI KUFUNGWA KWA MAKUFULI NA MAKOMEO
MULTI LOCK kampuni ya ki Israel iliuza sana makufuli na makomeo ya kulinda magari yasiibwe. Mijitu iliiba magari kwa namna mbalimbali, ila kubwa zaidi ilikuwa kwa kutumia fungi Malaya. Multi-lock ikawa changamoto kwa kina Kaka Jambazi

4. KUIFIKIA BAADHI YA MIKOA ILIBIDI UTOKE NJE YA TANZANIA NDIPO UFIKE
Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mara, Kagera na Mwanza ilikuwa haifikiki kirahisi hata kidogo, ilibidi ukate passport ya muda ili uvuke Kenya na wakati mwingine Uganda ili uweze kwenda huko.

Scandinavia Express walipiga sana hela, pia kulikuwa na kampuni ya Akamba wakitoa huduma hizo.

5. YO!! RAP BONANZA
Miaka hiyo ya tisini mwanzoni kurap ndo ilikuwa mpango mzima kwa wajanja. Chris's Phabby, Ras Pomppy Dou na Wengine wengi waliokwenda kuonyesha umahiri wao

6. KUMBI ZA STAREHE
Zama zile muziki wa dansi ukiwa umeshika hatamu, kumbi zetu zilikuwa Bonga Bar, Lang'ata Social Hall, DDC, Ruvuma Mpaka Maputo, Amana Social Hall.
Disco kwa MBOWE.

7. CODRY NA RABA MTONI, SKIPA NA DENGRIZ

Wajanja walienda Greece kwa kuzamia meli walirudi na suruali zao za codry, dengdriz, skipa na raba mtoni.
Enzi hizo madukani vitu vilikuwa adimu mno.

8. MODEL ZA MAGARI
Zama zile kulikuwa na Datsun, Toyota Staut, Isuzu KB, Pajero ambayo ilikuwa inatajwa Hadi kuwa nantv inayoonyesha majeneza na watu wakienda kuzika pale inapokimbizwa Sana. Kulikuwa na gari inaitwa Morris, kulikuwa na Impala, Scania 111, Bedford, Isuzu NKR, Isuzu TX, Land Rover 109 kidume. Zama zile ilikuwa NI marufuku kwa Range Rover kupaki benki.
 
Acha tu tulitembea na mdundiko kutoka Tandale mpaka Buguruni tuliporudi home tulichezea stiki na mzee mpaka mjumbe aliingilia kati ndo ikawa pona yetu

FB_IMG_1635421777703.jpg
 
Nikiwa na mama yangu, niliwahi kupita Nairobi katika safari ya kutoka Dar kwenda Mwanza. Wakati huo nikiwa kinda.

Yaani kusafiri sehemu moja kwenda nyingine ndani ya nchi moja ni mpaka upite nchi jirani. Ni mojawapo ya vipindi vigumu tumewahi kuvipitia kama nchi.
 
AHAAAAAAAAAAAA, UMENIKUNA SAANA LEO, MUZIKI WA DANSI, DDC KARIAKOO, MAGOMENI KONDOA , EQUATOR BAR MTONI PALE, UWANJA WA NDANI WA TAIFA, KIGONGO BAR BUGURUNI, HIYO NI SIKINDE BWANA USIPIME. YANGA AU SIMBA ISHINDA MDUNDIKO TOKA UWANJANI HADI MAKAO MAKUU, KURUDI UTAJUA MWENYEWE. MAMA NITILIE NI JIONI SAA MOJA MOJA SAANA UNAUZIWA MAHARAGE
 
Hakuna simu wala nini, nakumbuka niliwahi kwenda Pale Tanga FFU tunaiba simu ya kukoroga zile nampigia Mpenzi wangu(make now) alikua anafanya kazi Ofisi ya Kanisa Hahahahaha.

Appointment ilikua Appointment haswaaaaa mkiachana Leo mkipata mkutane Jumamosi SAA nane mchana eneo Fulani basi lazima iwe hivyo; hakuna kuliwa nauli!
 
Back
Top Bottom