Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

1635432823840.png
 
Ila mdundiko wazaram nimewavulia kofia,eti ukinttomba ukinnfilla sizai,nasema sizai
🤣🤣🤣ah ***** umenkumbusha huu wimbo aisee..huu wimbo huwa nikiukumbuka namkumbuka mother fulani alikuwa anaitwa mama Alfani enzi hizo sisi wadogo alikuwa na tako la haja basi kuna siku tunaenda mkoleni yeye ndio alikuwa mbele kabisa anaimbisha huu wimbo..."wee sizai tena hata ukint....ukinf...sizai tena" basi nikikumbuka kuhusu mdundiko wa zamani nakumbuka scene hii ya mama alfani
 
Yaani wengi watadhani ni as mulizi tu za Jomba Buji, lakini huku ndiko haswa tulikotoka

1. NGOMA YA MDUNDIKO
Zama zile MDUNDIKO ulipita mtaa kwa mtaa jijini, ni mwendo mpwitompwito, nyimbo, ngoma, matusi, mikatiko, yaani kivumbi na jasho, unatoka kwenu Buguruni unajikuta uko Kawe Mzimuni, na nauli huna.

2. JIWE LA FATUMA
Mmelala ndani mnasikia nje watu wanahesabu, moja, mbili taaaaaaaat. Kabla hawajamaliza kuhesabu mnaliona jiwe kubwa sana love naingia ndani, mlango umesambaratishwa, njemba za miraba minne kama Tisa, mapanga yameremetayo yenye makali kuwili yako standby kusambaratisha nyama za miili yenu, MNA music system wanabeba, TV set inaondoka, cheni na vidani vya dhahabu si Mali yenu tena.

Shukrani kwa Augustino Lyatonga Mrema

3. MAGARI KUFUNGWA KWA MAKUFULI NA MAKOMEO
MULTI LOCK kampuni ya ki Israel iliuza sana makufuli na makomeo ya kulinda magari yasiibwe. Mijitu iliiba magari kwa namna mbalimbali, ila kubwa zaidi ilikuwa kwa kutumia fungi Malaya. Multi-lock ikawa changamoto kwa kina Kaka Jambazi

4. KUIFIKIA BAADHI YA MIKOA ILIBIDI UTOKE NJE YA MDUNDIKO TANZANIA NDIPO UFIKE
Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mara, Kagera na Mwanza ilikuwa haifikiki kirahisi hata kidogo, ilibidi ukate passport ya muda ili uvuke Kenya na wakati mwingine Uganda ili uweze kwenda huko.

Scandinavia Express walipiga sana hela, pia kulikuwa na kampuni ya Akamba wakitoa huduma hizo.

5. YO!! RAP BONANZA
Miaka hiyo ya tisini mwanzoni kurap ndo ilikuwa mpango mzima kwa wajanja. Chris's Phabby, Ras Pomppy Dou na Wengine wengi waliokwenda kuonyesha umahiri wao

6. KUMBI ZA STAREHE
Zama zile muziki wa dansi ukiwa umeshika hatamu, kumbi zetu zilikuwa Bonga Bar, Lang'ata Social Hall, DDC, Ruvuma Mpaka Maputo, Amana Social Hall.
Disco kwa MBOWE.

7. CODRY NA RABA MTONI, SKIPA NA DENGRIZ

Wajanja walienda Greece kwa kuzamia meli walirudi na suruali zao za codry, dengdriz, skipa na raba mtoni.
Enzi hizo madukani vitu vilikuwa adimu mno.

8. MODEL ZA MAGARI

Zama zile kulikuwa na Datsun, Toyota Staut, Isuzu KB, Pajero ambayo ilikuwa inatajwa Hadi kuwa nantv inayoonyesha majeneza na watu wakienda kuzika pale inapokimbizwa Sana. Kulikuwa na gari inaitwa Morris, kulikuwa na Impala, Scania 111, Bedford, Isuzu NKR, Isuzu TX, Land Rover 109 kidume. Zama zile ilikuwa NI marufuku kwa Range Rover kupaki benki.
Na kipindi hicho humu bado kuna ambao walikuwa wanalala na dada zao maana walikuwa wadoogo madhara hawana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom