Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Zamani mashoga hawakuwa wengi kutokana na lifestyle iliyotukuza...hapa mtaa ninaokaa sio ushuani wala nini lakini nina miaka mingi sana sijasikia watoto wakicheza kombolela au hata ukutiukuti
 
Zamani mashoga hawakuwa wengi kutokana na lifestyle iliyotukuza...hapa mtaa ninaokaa sio ushuani wala nini lakini nina miaka mingi sana sijasikia watoto wakicheza kombolela au hata ukutiukuti

Kombolela, Ukuti au ule mchezo unaitwa center na ule mpira wa kuzunguka unaitwa sina ukimwi
 
Nani anawakumbuka hawa?

FB_IMG_1635426857416.jpg
 
1.Nyama kwenye pick up ikipelekwa buchani huku na wanunuzi wakiwa wamepanda juu wakiikanyaga hiyo nyama.
2.watu wakivuta sigara ndani ya basi.huku basi likiwa limewekewa ashtray kabisa.hakuna abiria anaelalamika.
 
Yaani wengi watadhani ni as mulizi tu za Jomba Buji, lakini huku ndiko haswa tulikotoka

1. NGOMA YA MDUNDIKO
Zama zile MDUNDIKO ulipita mtaa kwa mtaa jijini, ni mwendo mpwitompwito, nyimbo, ngoma, matusi, mikatiko, yaani kivumbi na jasho, unatoka kwenu Buguruni unajikuta uko Kawe Mzimuni, na nauli huna.

2. JIWE LA FATUMA
Mmelala ndani mnasikia nje watu wanahesabu, moja, mbili taaaaaaaat. Kabla hawajamaliza kuhesabu mnaliona jiwe kubwa sana love naingia ndani, mlango umesambaratishwa, njemba za miraba minne kama Tisa, mapanga yameremetayo yenye makali kuwili yako standby kusambaratisha nyama za miili yenu, MNA music system wanabeba, TV set inaondoka, cheni na vidani vya dhahabu si Mali yenu tena.

Shukrani kwa Augustino Lyatonga Mrema

3. MAGARI KUFUNGWA KWA MAKUFULI NA MAKOMEO
MULTI LOCK kampuni ya ki Israel iliuza sana makufuli na makomeo ya kulinda magari yasiibwe. Mijitu iliiba magari kwa namna mbalimbali, ila kubwa zaidi ilikuwa kwa kutumia fungi Malaya. Multi-lock ikawa changamoto kwa kina Kaka Jambazi

4. KUIFIKIA BAADHI YA MIKOA ILIBIDI UTOKE NJE YA MDUNDIKO TANZANIA NDIPO UFIKE
Mikoa ya kanda ya ziwa hasa Mara, Kagera na Mwanza ilikuwa haifikiki kirahisi hata kidogo, ilibidi ukate passport ya muda ili uvuke Kenya na wakati mwingine Uganda ili uweze kwenda huko.

Scandinavia Express walipiga sana hela, pia kulikuwa na kampuni ya Akamba wakitoa huduma hizo.

5. YO!! RAP BONANZA
Miaka hiyo ya tisini mwanzoni kurap ndo ilikuwa mpango mzima kwa wajanja. Chris's Phabby, Ras Pomppy Dou na Wengine wengi waliokwenda kuonyesha umahiri wao

6. KUMBI ZA STAREHE
Zama zile muziki wa dansi ukiwa umeshika hatamu, kumbi zetu zilikuwa Bonga Bar, Lang'ata Social Hall, DDC, Ruvuma Mpaka Maputo, Amana Social Hall.
Disco kwa MBOWE.

7. CODRY NA RABA MTONI, SKIPA NA DENGRIZ


Wajanja walienda Greece kwa kuzamia meli walirudi na suruali zao za codry, dengdriz, skipa na raba mtoni.
Enzi hizo madukani vitu vilikuwa adimu mno.
Hili la Jiwe la Fatuma ndiyo lina nikela mpaka leo....hivi wale jamaa waliokuwa wanafanya wizi wa namna hii kiumri sasa hivi ni watakuwa wamezeeka sana ingawa ujuzi wanao bado .....
Sasa kwanini mseme kijiji bila wazee ni fujo ?
Mimi ndiyo maana wazee wasikuhizi siwaamini maana ndiyo walikuwa Mataikun ya enzi hizo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
1.Nyama kwenye pick up ikipelekwa buchani huku na wanunuzi wakiwa wamepanda juu wakiikanyaga hiyo nyama.
2.watu wakivuta sigara ndani ya basi.huku basi likiwa limewekewa ashtray kabisa.hakuna abiria anaelalamika.
nilikuwa namaindi kimyakimya mtu kwenye pickup kakaa juu ya nyama asee
 
Back
Top Bottom