Tumetoka mbali sana, tumshukuru Mungu. Wengi hawakujionea kwa macho

Kombolela, Ukuti au ule mchezo unaitwa center na ule mpira wa kuzunguka unaitwa sina ukimwi
Siku hizi watoto wanabong'oka aisee miaka ile ukiinama tu ushapigwa zamani sana.

Jumamosi unapotelea Mtoni ukirudi jioni
ushachoka sana na hapo bado fimbo zinakusubiri za kutosha.

Tulijifunza kuvua samaki na kuwapika huko huko...vitu vingi tulivyofanya utotoni leo ukubwani ndio fursa.

Uza sana mipira ya vitamba ya kushona hapo unapata pesa yako ya jeans Jumapili pake Sabasaba(Morogoro mjini kule kwa Walurguru).

Hahaha mara mwisho nilikodiwa kwenda kuchezea team ya jirani nimelipwa mia (Sio laki shilingi mia ile) nikafunga ikawa mimi na mechi.Kuja kuangalia matokeo ya shule nikala fimbo mbaya. Masela wote waliokuwa wanakuja kunikodi nao moto ukawaka makwao.

Leo hii hata mpira siujui...
Achana na ugomvi ule shule..wachana na karate tulizocheza kwenye vile vikundi.
 
Nakuja inbox
 
Acha uongo, Rungwe Oceanic ilikuwa ya Mwakitwange, haina uhusiano na huyo Hashim Rungwe wako! Msiongee uongo hapa watu wengi tunajua haya mambo!
...Ungemsahihisha TU Mkuu, bila Kejeli!
 
...Land Rover...!
 
Kila mkoa ulikuwa na chizi maarufu ambae alikuwa anahisiwa kuwa ni mtu wa usalama wa Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…