Nimeamua kuandika ili wananchi tujue ya kuwa hata baadhi ya watunga sheria na pia ni viongozi wa dini hawajui kinachoendelea duniani.
Huyu Mbunge (Askofu )wa jimbo la Kawe ETI anaona chanjo vaccine ya corona ni upuuzi.Labda hana kitu kinachoitwa BRAIN ana maji kichwani.Dunia nzima inagombania chanjo hiyo ya ugonjwa hatari wa corona. Tayari ukiachilia nchi zilizoendelea kama Uingereza tayari asilimia 99 ya watu wanaoishi washachanjwa,Nchi za Afrika kama Ghana,Kenya,Rwanda wanaendelea na zoezi hilo.
Huyu Mheshimiwa akatembelee hospitali za Dar tu akaone zilivyofurika.Wakati wa awamu ya tano tulikuwa tunaambiwa ni ugonjwa wa kushindwa kupumua
Sasa awamu ya sita kwa kufuata ushauri wa WHO sijui kama anajua kirefu chake imeamua kufuata kwa manufaa ya wananchi na wageni. India watu kwa mamia wanateketea vivyo hivyo Brazil, Afrika ya Kusini baada ya kuumizwa sana na hatua za kuuzuia ugonjwa huu sasa ni afadhali kwani tayari nao wanachanja. Wameshusha hadi grade 1.
Sisi tumesaidiwa sana na nchi jirani kufunga mipaka yake vingenevyo Askofu sijui angekimbilia wapi.Uchumi wetu umedondoka anajua hilo? Watalii hasa Warusi waliokuwa wanajazana Zanzibar wamekimbia wa Serengeti hawapo kabisa kisa washaambiwa Tanzania kuna Corona na serikali inaficha ukweli.wawekezaji nao hawaonekani kutokana na uoga wa corona na ukandamizaji wa kodi na utaifishaji wa mali.analijua hilo? Dada Mdee mpe Elimu kidogo Mh Askofu hapo Bungeni.
Tanzania sio kijiji.Mwenzio akinyolewa wewe tia maji.Tukiwasikiliza akina Askofu Gwajima Hakutakalika nchini.Serikali iache kusikiliza upuuzi wa akina Askofu Gwajima.
#Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
#Kazi iendelee.
Soma:
Askofu Gwajima: Ni ujinga kuruhusu Taifa zima kuwa 'experiment' kwa sababu tuna haraka ya Corona
Fact-check: Ukweli kuhusu upotoshaji wa Mbunge wa Kawe juu ya chanjo ya Covid-19
Ufuatao ni ukweli kuhusu kauli za upotoshaji juu ya chanjo ya corona zilizotolewa na Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima, Bungeni Mei 11, 2021
1.
MRA technology iliyotumika kutengeneza chanjo inaingia kwenye DNA na RNA ya binadamu na inatuma ujumbe miaka ijayo mtu azaliwe wa namna gani. Miaka 20 au 30 ijayo Watanzania wanaweza kuzaliwa hawawezi kufikiri vizuri
UKWELI
Teknolojia iliyotengeneza chanjo haiitwi MRA bali inaitwa "messenger RNA (mRNA)" ambayo haibadilishi chembe chembe za mwili wa binadamu wala kuingilia DNA ya binadamu. Utafiti wa wanasayansi umethibitisha kuwa mRNA hiyo huvunjikavunjika muda mfupi baada ya mtu kupigwa chanjo na haikai haikai kabisa mwilini.
2.
CDC (Centre of Disease and Control and Prevention) inaruhusu dawa kupitishwa Marekani pamoja na shirika jingine linaitwa FDA (Flag and Drug Authority). Chanjo zote hizi unazoziona hazijapitishwa na mashirika haya.
UKWELI
Usahihi ni kuwa kirefu cha CDC siyo "Centre of Disease and Control and Prevention" kama alivyodai Mbunge wa Kawe bali ni
Centers for Disease Control and Prevention na kazi ya CDC siyo kuruhusu matumizi ya dawa bali kutoa taarifa kuhusu magonjwa na kuyadhibiti.
Jukumu la kuruhusu matumizi ya madawa Marekani liko chini ya FDA (Food and Drug Administration) na siyo "Flag and Drug Authority" aliyosema mbunge.
Hadi hivi sasa, FDA imeruhusu aina 3 ya chanjo zitumike Marekani, ambazo ni
Pfizer, Moderna na Johnson & Johnson
3.
Kuna kishirika kidogo kinaitwa Emergency Use Authorization ndiyo ambacho kimeidhinisha chanjo za dharura
UKWELI
Emergency Use Authorization siyo shirika wala kishirika, bali ni utaratibu au mfumo chini ya FDA ambao unaruhusu dawa au chanjo ambazo hazijapitia mchakato wa kawaida mrefu wa tathmini, ziweze kufanyiwa tathmini ya haraka na kuruhusiwa kutumika wakati wa majanga au dharura ya kitaifa na kimataifa kama Covid-19.
4.
EMA (European Medicines Agency) haijaruhusu chanjo yoyote itumike, bali chanjo hizo zimeruhusiwa na kishirika hicho kidogo cha Emergency Use Authorization
UKWELI
EMA ndiyo mamlaka pekee yenye uwezo wa kuruhusu dawa na chanjo zinazotumika Ulaya na siyo FDA au hicho kishirika hewa cha Emergency Use Authorization alichokisema mbunge.
Ukweli ni kuwa EMA hadi sasa imeruhusu aina 4 ya chanjo kutumika kwenye nchi za ulaya, ambazo ni
Johnson & Johnson, Pfizer/BioNTech, Moderna na AstraZeneca/Oxford
5.
Madhara ya chanjo ni pamoja na kushindwa kupumua, damu kuganda na kifo
UKWELI
Hakuna watengenezaji wa chanjo yoyote wanaosema kuwa moja ya madhara yake (side effects) ni kifo. Siyo WHO, CDC, FDA, EMA wala taasisi yoyote ile ya kisayansi na kitabibu iliyotoa tahadhari kuwa moja ya madhara ya chanjo ni kifo.
Chanjo za corona, kama ilivyo dawa au chanjo zozote nyingine duniani, zinaweza kuwa na madhara kwa baadhi ya watumiaji. Utafiti umeonesha kuwa hakuna kifo hata kimoja duniani ambacho kimehusishwa moja kwa moja na chanjo za corona. Asilimia kubwa ya madhara kwa waliopigwa chanjo ya corona ambayo imeonekana kutokea ni kwa baadhi ya watu kuumwa na kichwa kwa muda mfupi. Watafiti wamebaini kuwa faida za chanjo ni dhahiri.
Ikumbukwe kuwa hata dawa ya Aspirin nayo husababisha madhara kwa baadhi ya watu, ikiwemo kotoka damu.
Katika mataifa 54 ya Afrika, ni mataifa 5 tu ambayo bado hayajaanza kutumia chanjo ya corona, nayo ni
Chad, Burkina Faso, Burundi, Tanzania na Eritrea
Madagascar, ambapo tulituma ndege ya serikali na waziri wetu mwaka jana kwenda kufuata iliyoitwa "tiba ya asili" ya corona, sasa imeachana na mitishamba baada ya kubaini kuwa haifanyi kazi na kuingia rasmi kwenye matumizi ya chanjo.
Wahenga walisema:
"Uongo ukiachiwa uzungumzwe sana, huonekana ndio ukweli"
"Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako. Ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzetu"
Twende na wenzetu ulimwenguni, ikiwemo mataifa mengine karibu 50 ya Afrika ambayo yanatumia chanjo ya corona na tayari baadhi ya nchi hizo zimeanza kupata mafanikio ya kupunguza kasi ya maambukizi na idadi ya vifo.