#COVID19 Tumpuuze Askofu Gwajima kuhusu Chanjo ya Corona

Moja ya hoja za hovyo kabisa. Wewe kama unaogopa kufa kwa Corona ni wewe nenda kachanjwe. Hoja alizotoa Bishop Gwajima zinamashiko, taifa haliwezi kufanyiwa majaribio aisee tumekuwa manyani sisi. Thubutu
Kama kuna mtu hapaswi kuwa kwenye vyeo vya kisiasa basi ni Askofu Gwajima. Huyu mtu ni toxic. Amewapumbaza waumini wake vibaya sana, huwa wanakaa na maiti hadi siku 3 wakiamini Gwajima atawafufua. Halafu anafanya biashara ya madawa ya kulevya.

Mwendazake ametuletea disaster kwa kuwaweka hawa bungeni
 
Tumpuuzeni Gwajima Ila hoja yake tuibebe...!

Kama wengi wenu mlivyo mpuuza Hayati JPM Kwenye maamzi mengi kuhusu Corona, Ila hoja ya kutokuilock nchi tuliibeba wote ndivyo tunapaswa kufanya Kwa Askofu Gwajima

Gwajima, ameshauri Jambo la maana mno hatuwezi kuipuuza hoja yake kisa alimtoa jimboni kipenzi chenu
 
Gwajima hana data ambazo ni authentic zaidi ya consipiracy theories tu zilizopo miaka yote.

USA wamechanja about 40% population na ni less than 60 people tu ndiyo walipata complications ambazo, kwanza ni kawaida kwa dawa yeyote kwa baadhi ya watu. Pili siyo permanent impairment.

Gwajima ni FALSE PROPHET, msimpe nafasi sana kwa kuwa anaweza kuwa brain wash kama alivyowafa waumini wake
 
Hivi hizo vaccination Watanzania mbona tumezitumia sana tu bila ya madhara yoyote? Chanjo ya ndui, polio, kifua kikuu, yellow fever n.k. na tunaendelea kutumia hizo chanjo hadi kesho kutwa. Angalia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika baadhi ya nchi za Ulaya na USA baada ya kutumia chanjo za Pfizer na Moderna ili kupambana na COVID-19 sasa idadi ya maambukizi na vifo imepungua mno hadi baadhi ya nchi kuanza kuondoa vizuizi mbali mbali vilivyowekwa vya COVID-19.
 
Askofu Gwajima amesema hapingi chanjo bali anatoa tahadhari kuhusu aina ya chanjo, teknolojia iliyotumika na muda uliotumika kutengeneza chanjo za covid ukilingsnisha na chanjo za magonjwa mengine ambazo zinachukua hadi miaka 8 kukamilika.

Pia aliongelea madhara ambayo tayari yameanza kujitokeza kwa baadhi ya chanjo Kama kuganda damu na kupunguza uwezo wa kupumua.

Pia ukumbuke chanjo hizi ziko kwenye majaribio na hazijathibitishwa na CDC na FDA kama chanjo rasmi, bali zimeruhusiwa kutumika kwa ajili ya dharura, kwa hiyo madhara yeyote yatayotokana na matumizi ya hizi chanjo kampuni zilizotengeneza hazitawajibika kwa lolote.

Kwa hiyo ndugu unapojibu hoja za Askofu Gwajima jaribu kujibu kisayansi Kama yeye alivyodadavua, siyo hizo ngojera zako ulizoandika.
 
Mawazo ya kijima.
Ndiyo maana watu kama nyinyi korona ndiyo inaanza na nyinyi hadi mtakwisha
Wewe akili hauna Corona imemuondoa Maalim seifu ila sioni humu kulisema hilo au nae alikuwa na mawazo ya kijima?
 
Una mdomo mrefuu..!
 
Nyinyi ndio wale mnaosema hata shoga akiwa kiongozi sawa tu
Lissu akitetea haki za mashoga kwamba ni jambo la faragha anaonekana ni msomi ila sasa ajabu Gwajima anashambuliwa na kuitwa mcheza porn, Mbowe anajulikana ambaye ni mlevi na malaya ila ukisema hayo unaambiwa ni mambo yake binafsi.

Sasa nashindwa hata kuelewa.
 

Mkuu uaskofu sio uhuni wa kunyonga mauno hapa naona hujautendea haki na ingefaa utumbe samahani, Corona ni ugonjwa unaofahamika kwa watu wote walioenda shule na wasio na elimu kama huyo kanjanja wako wanajua nini kifanyike lakini wachache wanajifanya wanajua kuliko hata shirika la Afya la Ulimwengu kumbe wamejaza takataka kichwani mwao wakiamini kuwa watanzania ni wajinga kiasi hicho wanachoamini
 
Unless sijamsikia vizuri ila alichosema ni kwamba HAPINGI chanjo maana kama ni kuchanjwa karibia wote humu tulishachanjwa kabla kuzuia homa ya manjano, surua, uti wa mgongo, tetekuwanga , pepopunda etc etc.

Alichosema ni kwamba tusiwe part ya majaribio na wataalamu wetu wazifanyie tafiti hizo chanjo 3-4 kuona ipi inayotufaa na yenye potentially minimal side effects. Kwani NIMR au wale maprof wa pale Muhimbili wapo pale kwa kazi ipi?

Gwajima hatumpendi ndio lakini chuki isitufanye vipofu na kupinga kila kitu anachosema. Kwenye hili yupo sahihi. Hatuwezi kuiga kizembe na kukimbilia kila kitu eti kwa kuwa Nchi nyingine zinafanya hivyo. Context zetu ni tofauti sana
 
Watu wanapaswa kujua kuwa pharmaceutical cartels wananguvu sana hapa duniani. Magonjwa mengi yanayoisumbua dunia ni genetically engineered na hawahawa jamaa. Haingii akilini Covid-19 ilijitokeza mwisho wa 2019 ndani ya mwaka mmoja chanjo imeshagunduliwa na mataifa yanashinikizwa kuitumia. Kuna nchi mbalimbali zikiwepo za Ulaya wamesitisha matumizi ya baadhi ya chanjo baada ya either Kugundua kuwa zinamadhara au hazifanyi kazi iliyokusudiwa.
 
Ndugu zangu tumtegemee Mungu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kwani anajadiliwa Mbowe au Lisu hapa?

Lazima ushindwe kuelewa kama umeshindwa kujikita kwenye mada.

Lisu ni mwanasiasa
Mbowe ni mwanasiasa

Gwajima ni mtumishi wa Mungu ambaye ameamua kuwa Malaya Malaya kingono na kisiasa kwanini tusiseme?
Mtumishi wa Mungu unaacha mke ndani unaenda kununua Malaya tena unajirecord kabisa huo si uwendawazimu?
 
Mbona umeandika bandiko kubwa ,la kumshutumu Gwajima.Lakin ndani hakuna hoja za msingi zaidi ya uchafu tupu.Gwajima amejenga hoja za msingi,ulitakiwa kuzijibu na kutuambia kama ni za uongo.Napata mashaka kwamba una ka NGO kako umekaandaa ili upige dili kupitia hizo chanjo.Jaribu kusoma majarida ,Journal mbalimbali ili ukishitumu MTU ,unatumia evidence. Sio uchafu tu wa kusikia.
 
Mbowe ni mfanyabiashara na Lissu ni mwanasheria, mkileta masuala binafsi ya mtu basi pia huwezi kukataa kuzungumzia masuala binafsi ya ulevi na umalaya wa Mbowe. Mgejikita kwa yale aliyoyaongea Gwajima ila badala yake mnazungumzia mambo yake ya faragha kitu ambacho hata wakili msomi Lissu huwa anakipinga.
 
Wewe na jiwe na huyo Gwajima akili zenu sawa na subirini lwang'oe mmoja mmoja
 
Hizo ni akili za ki lucifa yaani mnafurahia Tanzania ikitumbukia kwenye matatizo ya kama ya Kenya au India ndiyo mtafurahi maana mtakuwa mmepata damu za kafara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…