Tunahitaji mjadala mpana wa kitaifa juu ya timu ya watu inayounda 'Mamlaka za Uteuzi' nchini

Kama unataka kila unayepingana nawe afungiwe basi atafungiwa kia mtu humu.

Kwa hiyo mtu akianzisha mada kulaani teuzi zilikzokaa kikanda utataka afungiwe?

Kama mtu akianzisha mada kuhoji teuzi zilizokaa kikabila utataka afungiwe?

Kama mtu akianzisha mada kuhoji teuzi zinazobagua wanawake utataka afungiwe?

Kama hayo yote huwa hamuoni tatizo kwenye mada zinazoyahusu, kwa nini buwa hampendi mada zinazohoji teuzi zilizokaa kidini? —Au mnanufaika na mfumo wa aina hii kwa hiyo hampendi uhojiwe?
 
Hizo DINI nyengine hazina athari. Lakini Ukristo na Uislamu ni Kama Simba na Yanga.
 
Hizi takwimu za Pemba, Bagamoyo na Tanga tu
 
Wakristu wa Zanzibar hawafiki hata asilimia moja. Ndio maana hawalalamiki. Kwasababu wanapewa kikubwa kuliko wanachostahili.
 
Mwacheni mama achape kazi usimpangie cha kufanya au mnataka siku akasirike naye aropoke "mimi sipangiwi" msilete mambo ya udini na ukabila mama anaangalia uwezo wa mtu sio dini wala kabila.

Mbona huko katika uongozi mmejaa wakristo na waislam ila taifa tupo wengine ni Budha lakini hatujawai lalamika.
 
Najua hata wewe unaujua wingi wa wakristo, kwa huku Tanganyika hata bila kumuuliza huyo Mganga njaa Chahari, Wakristo ni wengi.Kule visiwani waislam ni wengi kuliko wakristo sikatai.Ila tunapozungumzia Tanzania (Tanganyika + Zanzibar) ndo tutahitaji hiyo sensa unayoizungumzia.

Hiyo sensa ya 1954 unayoizungumzia wewe, haiwezi kutoa uhalisia wa maisha ya Sasa kwasababu ilikuwa ni kabla ya uhuru, na kipindi kile dini ya kiarabu(Islamic) ilikuwa imetawala sana tofauti na wakati huu.
 
So, are you saying that a Muslim president is prejudiced against Muslims?
 
kwamba mlifikiri akiwa rais basi atapendelea upande fulani?
nadhani mna miss concept ya urais.
ni taasisi na hafanyi maamuzi mwenyewe.. majina yanapita vetting.. ambayo ime comprise mashirika ya ulinzi, na ya kiraia.
kama vetting cometee hamuitaki. andamana wafute
 
Nimekuelewa vizuri hadi natamani mleta uzi akuelewe pia. Kwa kuongezea ,katika distribution let's say ya wenye PhD wakiwa categorized kwa dini je hizo PhD na uzoefu zinakidhi nafasi husika???Maana swala la dini ni very minor compared to technical experience and expertise in the required field , sijui kama mleta uzi amezingatia hayo!

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
 
Hao 20 percent Muslims bado kuna watu wanamuona mama mdini.

Walitaka Muslim ikiwezekana wawe 1 percent I guess.

Hii nchi ngumu sana
Hapa mdini ni wewe. Bila shaka hata wateuliwa waislamu 60% hautaridhika.

Mbona mpaka sasa teuzi zinazolalamikiwa na kupigwa mawe sana ni za Phillip, Dotto, Lameck na huyu Thobias aliyetenguliwa. Wanaoshambulia ni wamisheni na waislamu na hamna mtu anayesema wakina Fatma wanawakosoa kwa sababu sio waislamu!

Mnakotaka kutupeleka siko.

Amandla...
 
Nafikiri ili hii hoja iwe na mashiko
Uje na analysis ya kuthibitisha hio imbalance
Mfano uteuzi wa jana tuweke column ya dini afu tutafute ratio

Vinginevyo hizi zinabaki kuwa ni hisia
 
Ukitaka kulijua hilo vizuri anzia CHEKECHEA KABSA baadae njoo sekondari, baadae njoo vyuo vikuu then chukuo orodha ya wagombea wa nyazifa mbalimbali hasa ubunge na udiwani kupitia ccm kwa kila jimbo au kata nadhani utapata jibu sahihi. Labda kama ungesema ipo haja ya kufanya juhuudi za makusudi kabsa kupendelea upande flani kwani inaonekana dhaili unataka kumeza upande mwingine, lkn kumshutumu MTEUZI kuwa anapendelea upande mwingine unamwonea bure, na hii iko hivyo hata kabla ya uhuru, ukitaka kujua hilo chukua takwimu za watumishi wa serikali kabla ya uhuru na uanze kuwachambua then lete mrejesho.
 
Mbona Zanzibar husemi waislamu wamependelewa mana ndo wamejaa huko?.
Ushasikia mkristo analaumu?.
 
Mimi nadhani watu wazingatie deliverables.

Kumpa mtu kazi kwa sababu ya dini yake ni udini, kumnyima mtu kazi kwa sababu ya dini yake pia ni udini.

Mtu akianza kuchukua pesa za shirika au wizara kwenda kufanya mambo ya kidini, hapo ndio tuanze kumletea shida. Hata Magu, kuteua watu wa kanda yake haikuwa shida. Tatizo ni alipoanza kupelekea vitu kwao ambavyo namna pekee vinaweza kwenda ni kwasababu yeye ni Rais. Hapo ndio tabu ipo.

Kumuambia Rais balance dini, mimi nawaza how do you do that practically? Maana ukiwaambia wasaidizi nipeni composition fulani ya kidini, tayari unakuwa umeleta udini.
 
So what ,tumekubali kwamba Zanzibar na tanganyika ni taifa moja so nao wajiandae ipo siku mkiristu atakua mkuu wa nchi TOKA bara na mikoa yote itakua nusu KWA nusu Kama ambavyo tz kwamba bila ukabila ,dini jinsia kiongozi twampenda
Wakristu wa Zanzibar hawafiki hata asilimia moja. Ndio maana hawalalamiki. Kwasababu wanapewa kikubwa kuliko wanachostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…