Tunaojihisi kuchoka na kitu fulani tufarijiane

Mkuu yaani mimi ndoo nichoka zaidi yako ila pole tutafika tu mungu yupo pamoja nasi .dunia ina hii ni ngumu inatunyanyasa mpaka akili analock
Inaumiza sana
 
Pole sana ,kuna haja ya kumuona mwanasaiokolojia haraka.

Kama watu ambavyo wanapiga promotion za pombe na sigara wangetumoa pia kwa matangazo ya umuhimu wa afya njema ya akili mambo yangependeza sana.
 
Pole sana ,kuna haja ya kumuona mwanasaiokolojia haraka.

Kama watu ambavyo wanapiga promotion za pombe na sigara wangetumoa pia kwa matangazo ya umuhimu wa afya njema ya akili mambo yangependeza sana.
Nimewaza Ivo pia
 
Pole sana ,kuna haja ya kumuona mwanasaiokolojia haraka.

Kama watu ambavyo wanapiga promotion za pombe na sigara wangetumoa pia kwa matangazo ya umuhimu wa afya njema ya akili mambo yangependeza sana.
Ngoja niende wanipe ushauri zaidi huenda nikakaa sawa
 
to yeye tunaweza kukuambia maneno mengi sana na kwa urefu sana lakini mimi naomba ni kumbie neno fupi tu nalo ni nyakati hazidumu.
Baada ya hilo tazamia kesho ilio njema tazamia asubuhi ilio njema, ila jua tu kesho njema huandaliwa na leo, na leo iliandaliwa na jana, kama jana ilikua mbaya basi usitarajie leo nzuri kadhalika kesho nzuri pia . Ila jua tuu wakati haudumu iwe mbaya ya mzuri haudumu, usikatishwe tamaa ya maisha kwa wakati mgumu wa leo ambao haudumu hali wewe unadumu.

Wakati unazaliwa wewe ili kua ni wewe kati ya maelfu kama sio mamilioni lakini wewe ukawa mshindi na ndio hivyo tupo nawe leo hii, hivyo fanya ufanyavyo lakini dili sana na kesho kwa kupitia leo, I wish ninge ki pm lakini itoshe tu kwa hilo.
Pole lakini.
 
 

Attachments

  • VID-20220110-WA0000.mp4
    4.4 MB
Barikiwa sana,nilishaanza kupona mkuu .Asante sana
 
Poleh sana jmn

Labda unapata wito wa kufanya biashara na sio ualimu
Au tafuta private kuna ahueni labda

Kuna kipindi niliichoka sana kazi flani..nilifanya mchakato nikabadili
No regrets am very happy saivi
 
Piga moyo konde ukubwa jalala usichoke Kuna watu hawana hata hio kazi ya kuamka mapema lakini hawajachoka kupambana
 
158-U Mwendo Gani Nyumbani?
How Far From Home (SDAH439)
Doh ni E♭

U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha, macheo karibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.

Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.

Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

Siyo mbali na nyumbani! fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi.
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.

Wimbo huo, ukawe faraja kwako.
 
Daah pole sana dada ila haupo pekee yako me muda natoka kwenye shughuli ya boss inayoniingizia kipato uwa nakuwa depressed sana bila sababu unakuta nahisi njaa ila sitaman kula chochote nachukia maisha kiujumla ila nashukuru Mungu nimeanza maombi ambayo yananisaidia kidogo kuniondolea hii hali plus music napendelea zaidi kuzirudia nyimbo hzi mbili,
Darasa ft Ben Paul-SIKATI TAMAA
Madee ft TundaMan-PESA
 
Kati ya nyimbo nazipenda sana hii ni moja wapo uwa natamani kila jmosi kabla sijatoka church niusikie nyingine ni,
3.Mungu atukuzwe
14.Nitembee nawe
80-Tupe moto wa uhai
85-Salama tumepita
131-Baba anilinda
143-Naamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…