Sawa kwakuatujadili bwana tajiri!!.
Ila unaonekana muda wako wa kumiliki kitu kinacho tumia mafuta ulikuwa bado sana umelazimisha ndio maana unawaza sana angalia usije pata pressure bure .
Yaani ununue gari utegemee mafuta akuchangie mwingine, kwahiyo asipo changia hautaenda kazini na gari lako? Au ndo wivu wa kiafrika tulio nao.
Mimi kama miezi minne iliyo pita nilihama kwenda kutafuta ridhiki mkoa x, kuna jamaa tunafanya shughuli pamoja, wakati nataka kurudi mkoa nilio na makazi kuangalia familia na yeye akasema anaenda huko huko anatafuta watu wa kumchangia mafuta.
Tukawa watu watatu tukasema sawa tutachangia mafuta, nauli ni 25,000 kwa bus ila tulipo fika kituo cha kuweka mafuta tukiwa tunampa 25,000 aligoma kuwa anataka 35,000, wote tukampa bila maneno kumbuka wote tunafanya shughuli sehemu moja.
Tulipofika njiani akaongeza abiria mwingine ambaye alitoa 20k tukabanana hivyo hivyo gari lenyewe ni Cc 1490.
Kwa mawazo yake alikuwa na akili kama yako kuwa hawa hawana magari.
Wiki mbili ziliyo pita mimi nilimpa lift siku ya ijumaa toka mkoa x na kurudi naye siku jumapili sehemu ya mihangaiko yetu ya kutafuta mkate, akabaki anajichekesha chekesha tu kuwa umeniokoa sana nilikuwa sina nauli mara sijui gari lake limefanyaje fanyaje, mimi nikiwa namchora tu, huku akiangali gari lina Cc zaidi ya 4000 ila ni diesel.