Kuna mambo hapa duniani hufanyika ni magumu na kila unapoyaelezea unaweza kuwa unatoa machozi na kulia, Lakini cha ajabu, yakisha kutendeka hayabadiriki tena hata ukivimba na kuvimba Kwa uchungu ukiekezea,
Kuendelea kuyakumbuka ni kujiumiza Kwani huwezi kuyabadirisha, una heri moyo wa kusamehe
Utu hupimwa Kwa uendelevu wa mtu kule aendako na siyo atokako
Ukiniuliza Mimi kuhusu Tundu Lissu Kwa sasa, nitasema, huyu Lissu ni mbaya kuliko anayemsema kuwa ni mbaya!!
Kwa maana ni wangapi ambao wamepatwa na ulemavu wa kusababishiwa lkn Bado walivaa ubinadamu wa kusamehe na kumwinulia Mungu sifa, na unajiuliza, kama ingetokea ndio amekufa siku hiyo, hii lawama angekuwa anaitupa wapi???
Swala lililopo ni kumshukuru Kwanza Mungu Kwa kubaki salama na kwamba Hadi sasa yupo, Swali lake ingelikuwa ni kumu, uliza huyu Mungu aliyeamua abaki, ni lipi anapaswa afanye, na Kwa nini aliamua yeye abaki mbali na kwamba mpango wa maadui zake ilikuwa kwamba afe!!!?
Kama Hana hata hiyo akili, basi yeye ndio mbaya kuliko maadui zake,