Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 24,314
- 38,919
Daah kilimo cha kuwasikiliza motivational speaker.......hapana,Pole sana ndugu ila kwa hizo assets ulizo nazo hasa gari.....ifanye uber tu au uza......na naona bora wewe unapakuanzia kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daah kilimo cha kuwasikiliza motivational speaker.......hapana,Pole sana ndugu ila kwa hizo assets ulizo nazo hasa gari.....ifanye uber tu au uza......na naona bora wewe unapakuanzia kabisa
Kiingereza chote hichi umekosa kuwa na hela?kweli kiingereza bila hela ni sawa nakupiga kelele . alisema langa
Sent using Jamii Forums mobile app
Eti shida ni mashindano 😀 😀 😀 😀 😀Ninyi ndo miongoni mwa wa bongo mtu anamweleza hali yake ya kimaisha halafu yeye anamwambia Hiyo ya kwako mbona cha mtoto? utafikiri shida ni mashindano
Pole sana . ...tukaze tu!Toka mwaka Jana mwishoni mambo yameenda kombo sema nina miti yangu mikalibea Kama 2,500 sema bado miaka mitatu ili nianze kuvuna. Nilikuwa nimeishapanada migomba Kama 400 Ila hyo mpaka nianze kuvuna bado miezi nane. Kujenga nimejenga ila nawaza kupata tena capital ya kupiga mishe mpaka nimalize miezi hyo minane ambapo Nina wakika wakupata mikungu ata 100 kila mwezi kwenye hyo Miche 400 niliyopanda ambayo ata nikiuza kwa ndizi moja 8,000/ in case the price is down naweza kujipatia 800,000/ kila mwezi uku nikiwa namuomba mungu miaka mitatu iende alaka nivute ata 25,000,000/ kwenye kamsitu kangu niliko kapanda kimasihara kwa pesa ya boom la chuo. Ila asikwambie mtu kufulia kubaya Ila ngoja tupambane kuanza upya maana bado January hii mpaka kuja kufika desemba kitaeleweka tu kwa nguvu za mungu.
Amen! Amen! Amen!Maisha ni safari ndefu,kuna ups and downs,cha msingi ni kutokata tamaa,mlango mmoja ukifungwa tegemea mlango mwingine kufunguka..maandiko yako wazi"sitakupungukia wala kukuacha kabisa".
Sent using Jamii Forums mobile app
PoaKimsingi huna shida wewe au hujui maana halisi ya shida ninayoiona kwako Ni changamoto tu
Ninyi ndo miongoni mwa wa bongo mtu anamweleza hali yake ya kimaisha halafu yeye anamwambia Hiyo ya kwako mbona cha mtoto? utafikiri shida ni mashindano
Mkuu hii cha mtoto ilizingukaga ya mapapai[emoji1787]
Huyu mkuu anatuchanganya tu watu vichwa vishawaka moto.Nimesoma kwa umakini hadi nilipofika 'ujenzi haujaisha, nimepoteza 14m, nina gari ndogo' nikaona umeleta thread hii kuwachora wenye hali ngumu kiukweli.
Jamaa anatania watuMtu anamiliki tecno na mapumbu mawili, ww unamiliki gari na nyumba hata kama haijakamilika bado unasema hali ni ngumu my friend are you serious
Sent using Jamii Forums mobile app
Imani yako imekuponya, na iwe hivyo.pole sana mkuu my hubby and I tunapita kwenye situation kama yako inatakiwa tarehe 1feb tukamuone landlord ila Mungu ni mwaminifu atafanya njia pasipo na njia
Pole sana mkuu, ila kwa pesa hiyo uliyopoteza shambani ungetumia nusu yake kununua nyanya na kufanya biashara naamini ungetoka vizuri tu.Hali (situations) zinaniambia nimekwishafeli, naona km situations zinanipa both public and private insults.
Real insults and I have no power to argue. Nimebaki nainamisha kichwa chini tu na kusikilizia jinsi hali inavyouma.
Mambo yanakwama mbele ya uso wangu, mbele ya macho yangu naona. Nashuhudia mwenyewe. Roho inaniuma, nalia ndani kwa ndani kama wanaume waliavyo. I smile but don't mean it, I laugh but don't mean it. Naumia. Kilio cha wanaume.
Nakwama kuanzisha projects zangu ndogo ndogo tu. PESA sina. Nimefilisika kila kitu. Uzuri sina madeni yanayonikaba shingo, lakini kodi ya pango February kesho kutwa, sijui nitalipa nini. Oohh God simama na mimi, and make me strong forever.
Maisha ya kutafuta pesa natakiwa kuanza from 0 yaani zero, with nothing on hands.
Kweli life, are you unfair like this? Are you fighting against me? Nisamehe. You are always bigger than me, forever and ever. This punishment is bigger than me, am a little bit young and old I can't handle this intense. It's huge, very huge!
Cha ajabu Akili (brain), Moyo Mkuu (big heart) na Nafsi (Self) zinaniambia big NO sijafeli. Then, nasikia furaha kwa ndani. Lakini situations halisi zinaondoa furaha yangu ghafla. Naona sina pesa, naona siwezi hata kuanzisha ki mradi kidogo tu. Sina pesa mimi.
Kwa miezi ya mwishoni mwa mwaka jana nilipoteza shambani zaidi ya sh 14,521,000 kwenye nyanya huko Dakawa Morogoro. Hizi ndio situations zenyewe. Situations zenyewe ni hali halisi, najawa hofu kuu. Naanza kupoteza confidence, japo inside myself najiona nipo strong but weak.
Ujenzi umesimama rasmi. Nimekwama pesa. It's now very official. Wapi rafiki zangu wa karibu? Wanalia hali ngumu. Dah! Mwamba nimekamatika na mdororo wa kiuchumi. Oh God, shusha malaika wako uniokoe, wewe ndiye tumaini langu pekee.
Nina asset gani mkononi? Nina gari dogo nzuri tu. It's my last option. Hii ndio risasi yangu ya mwisho. Sitaki kuifyatua bila target, lakini naona hali halisi ikinishinda nguvu. Mungu ingilia Kati wewe ndo umebaki tumaini langu la mwisho. Nakusihi Mungu Mkuu. Sitaki kupoteza hii risasi ya mwisho. Naomba mwanga wako nipo gizani.
Nikipata mil 2 ndani ya miezi 3 naweza kurudisha labda na riba kidogo, let say 2.3ml. Wapi pesa hii hupatikana? In short hakuna. Zinapatikana kwa riba kubwa sana, ambayo sitaweza kuilipa. Otherwise atokee mtu mwema Mungu kamshukia asaidie. Ila ki kawaida kawaida hell no pesa hizo mtu hupati bila riba kubwa.
All shall pass. Kweli? Sijui.
Ma chief wa JF najua kuna wengi labda washawahi kuwakuta ya namna hii. Naomba tushauriane, nyie mlitokaje jamani? Kodi za nyumba mlilipaje? Heshima ya kumiliki pesa tena mliipataje? Mlirudi vipi kwenye form kama awali?
Tutiane Moyo na ushauri, tusaidiane tafadhali, hali ni tete sana.
Mungu Mkuu.