Tunaopitia kwenye nyakati ngumu za kiuchumi na kimaisha, tutiane moyo!

Toka mwaka Jana mwishoni mambo yameenda kombo sema nina miti yangu mikalibea Kama 2,500 sema bado miaka mitatu ili nianze kuvuna. Nilikuwa nimeishapanada migomba Kama 400 Ila hyo mpaka nianze kuvuna bado miezi nane. Kujenga nimejenga ila nawaza kupata tena capital ya kupiga mishe mpaka nimalize miezi hyo minane ambapo Nina wakika wakupata mikungu ata 100 kila mwezi kwenye hyo Miche 400 niliyopanda ambayo ata nikiuza kwa ndizi moja 8,000/ in case the price is down naweza kujipatia 800,000/ kila mwezi uku nikiwa namuomba mungu miaka mitatu iende alaka nivute ata 25,000,000/ kwenye kamsitu kangu niliko kapanda kimasihara kwa pesa ya boom la chuo. Ila asikwambie mtu kufulia kubaya Ila ngoja tupambane kuanza upya maana bado January hii mpaka kuja kufika desemba kitaeleweka tu kwa nguvu za mungu.
 
Kimsingi huna shida wewe au hujui maana halisi ya shida ninayoiona kwako Ni changamoto tu
 
Pole sana . ...tukaze tu!
 
Nimesoma kwa umakini hadi nilipofika 'ujenzi haujaisha, nimepoteza 14m, nina gari ndogo' nikaona umeleta thread hii kuwachora wenye hali ngumu kiukweli.
Huyu mkuu anatuchanganya tu watu vichwa vishawaka moto.
Mi juzikati tu hata wiki haijaisha niliona kama dunia nzima imenielemea nikafanya mpango chapchap nikaenda kwa bro wangu na yeye kama alijua vile siku ile tulipiga story hadi sa nane usiku,akawa ananielezea maisha aliyopitia alivyostrugle mpaka kua hapo alipofikia na haya yote hakuwa kunambia hata siku moja.
Basi aliponipa ile story kesho nikamuaga mapemaa nikasema bado mapema sana kilichonileta huku acha nikamalizane nacho tu mwenyewe nikapambane kiume.

Haya maisha mkuu unaweza ukajiona una shida ila ukitana na watu wenye shida serious mbona we mwenyewe unanyooka.
 
pole sana mkuu my hubby and I tunapita kwenye situation kama yako inatakiwa tarehe 1feb tukamuone landlord ila Mungu ni mwaminifu atafanya njia pasipo na njia
Imani yako imekuponya, na iwe hivyo.
 
Pole sana mkuu, ila kwa pesa hiyo uliyopoteza shambani ungetumia nusu yake kununua nyanya na kufanya biashara naamini ungetoka vizuri tu.
Nakushauri ufyatue hiyo risasi yako ya mwisho ujilipue kwenye biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…