KERO Tunashukuru HESLB kuongeza muda, lakini button ya Application bado haionekani kwenye mfumo

KERO Tunashukuru HESLB kuongeza muda, lakini button ya Application bado haionekani kwenye mfumo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwanza, napenda kuishukuru sana JamiiForums kwa kutupazia sauti sisi waombaji wa mikopo ya HESLB. 🙏🏽 Post yenu ya tarehe 14 Septemba ilisaidia suala hili kuwafikia wahusika, na hatimaye HESLB ikaongeza siku nne za maombi. Tunawashukuru sana kwa hatua hiyo.

Hata hivyo, bado kuna changamoto kubwa. Leo, tarehe 16 Septemba, licha ya kuongezwa muda, mfumo wa OLAMS bado haujarejea katika hali ya kawaida. Kitufe (button) kilichokuwa kwenye dashboard, ambacho mwombaji alikuwa akikitumia kuingia moja kwa moja kwenye application, bado hakipo. Tunapoingia kwenye akaunti zetu, hatuwezi kuendelea na maombi.

Kwa hiyo, tunaomba tena HESLB irejeshe kitufe hicho na kutuwezesha kupata access ya maombi. Tumeongezewa siku nne, na tunaomba muda huo uwe na maana kwa kuhakikisha waombaji waliokwama kutokana na changamoto ya mfumo wanapata fursa ya kukamilisha maombi yao.

Muda unaendelea kuyoyoma, na sisi ambao tumekwama kutokana na mfumo bado hatujui hatima yetu. Tunaomba HESLB ichukue hatua haraka. 🙏🏽

1789618841833.png
 
Badala ya kelele za wadau kufika hapa tangu mfumo wa kuomba mkopo HESLB kusumbua tangu ijumaa ilihali deadline ilikuwa tarehe 14, bodi hiyo imeamua kuongeza muda tuu hadi tarehe 18 kwa wanaoendeleza ombi tuu ili kutupiga changalamacho badala ya kurekebisha mfumo na kuongeza muda.

Hali hii inatukera kwani hatuwezi kufanya chochote na tulishalipia hadi gharama za kuomba na pesa wamechukua. Pia no ya huduma kwa wateja hata hazipatikani ni gelesha.
 
Back
Top Bottom