joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 19,513
- 41,719
mda ni nini?
Acha kukalili, kuna watu kibao wanapanda na ni wafanyakazi wakawada, cha msingi ni kuwa na ni NIDHAMU YA MDA, sio kila kitu kulalamika tu. Zamani Stand ilikuwa maeneo ya Kisutu, ikahamia Ubungo walitokea wanaolalamika kama ww,ila baadae wakazoea hata hili la Mbezi watazoea tu,haijalishi unapenda ndege, treni au bus unacho takiwa kuwa na nidhamu ya mda.
Mkuu ni pabaya tu uchochoroni na mazingira machafu sana plus mrundikano wa mabasi mchanganyiko, hata stand ya katesh ni nzuri sana.Mbona Nairobi wanastendi yao ya muda mrefu?. Inaitwa machakos bus stand ya zamani sana miaka ya 1980s sema wameruhusu mabasi mengine kuwa na stendi zao
Kaza ulimi, sema "muda"muktadha unaotumika: ni neno la mkato linalomaanisha muda
Katika mawasiliano ya kila siku na maandishi yasiyo rasmi, "mda" hutumika kama neno dogo au la mkato la neno muda lenye maana ya wakati, saa, au kipindi fulani cha kufanya jambo.
Reference: Google kama hujaelewa nikupe link.
aisee angekuwa anajua nidhamu ya muda asingesapoti hii kitu ni kumsamehe bure tu. mana hajawaza yale malri+ wakaazi wanaotoka katika shughuli jioni + wanaoenda kupokea watu jam yake itakuwaje kutikea mjini kuingia na kutoka mbezi. ni aheri wangeacha tu hivi hivi kiukweli imepunguza misongamano na kuongeza vyanzo vya mapato na ajira kwa baadhi ya watu.Huwezi ukawa na nidhamu ya muda ukapanda Bus acha kudanganya watu.
Kupanda mabus ni watu wa kipato cha chini.
Mtu mwenye pesa hawezi tumia masaa zaidi ya 12 kutoka Dsm mpaka Arusha alafu useme ananidhamu ya muda
Nikaze mimi au wenye msamiati wao?Kaza ulimi, sema "muda"
aisee angekuwa anajua nidhamu ya muda asingesapoti hii kitu ni kumsamehe bure tu. mana hajawaza yale malri+ wakaazi wanaotoka katika shughuli jioni + wanaoenda kupokea watu jam yake itakuwaje kutikea mjini kuingia na kutoka mbezi. ni aheri wangeacha tu hivi hivi kiukweli imepunguza misongamano na kuongeza vyanzo vya mapato na ajira kwa baadhi ya watu.
Vipi option ya kuwa na shuttle, huwezi kuweka Stand binafsi kila mahali huo sio utaratibu. Tatizo kizazi cha kivivu, watu wanataka kushushwa nje ya nyumba.Yaani mtu atoke kigamboni ati anawahi Bus Mbezi Louis?
Tena watu wenyewe wengi wao ni pangu pakavu.
Huo ni usumbufu.
Wao waweke utaratibu kwamba magari lazima yaingie Mbezi Louis hasa yanayotokea Chalinze.
Hapo 50/50 kati ya serikali na raia wake.Ulimuelewa RC alivyosema? Lengo ni kuondoa mabus makubwa ndani ya mji.
Mkuu mabus makubwa yanayopita katikati ya mji ni KERO kubwa sana ,halafu yanakimbia sana ,yanasababisha ajali kila siku ,yakianzia huko nje ya MJI inaleta haueni.
Sisi tunayoyaona yanavyoleta VURUGU tunajua athari zake.
Kumtoa abiria kutoka huko temeke hadi Mbezi Magufuli siyo shida ,Dar zipo Route zote za kwenda Mbezi Magufuli....Usafiri kwasasa ni 24/7 ,kata tiketi ambapo muda utakuwa mzuri kwako...hauwezi kuchelewa bus...Pale mbezi magufuli zipo facilities za accomodation au unaweza ukaa waiting room vile vile kama hauwezi kuafford accomodation.
Kwasasa serikali ya Mkoa wa DSM inapaswa isimamie sheria na taratibu. Tuwe wakali kwenye hilo, hakuna kumchekea mtu.
Mapato ya serikali yanavuja.
Sasa dar Ina ukubwa Gani sehemu ya square kilometer 1700.Nonsense!...yaani jiji kubwa kama dar mnataka mabasi toka mikoa yote yafikie kwenye stand moja!?...jiji kubwa kama hilo linatakiwa liwe na stand kubwa kadhaa kulingana na mabasi yanapotoka
Kama unaweza kuwa na fremu za biashara na vituo vya mafuta kila mahali unaweza pia kuwa na stendi binafsi kila mahali.Vipi option ya kuwa na shuttle, huwezi kuweka Stand binafsi kila mahali huo sio utaratibu. Tatizo kizazi cha kivivu, watu wanataka kushushwa nje ya nyumba.
Wanaopanda ndege ni akina nani? Wewe una vichekesho sana.Wanaopanda ndege ni ma CEOs wa benki, mawaziri, matajiri, watalii na wafanyakazi wanaolipiwa nauli na Ofisi zao. Wote hao wanapelekwa airports na maviete ya serikali na Ofisi zao, range au taxi. Wanaopanda mabasi ni masikini na wanajitegemea wenyewe kwa kila kitu.
Acheni upumbavu wa kufananisha Airport na Stendi za mabasi, ni sawa na kufananisha Ikulu na Ofisi za Halmashauri za wilaya.
Nyie ndio mnaofanya wanaolazimisha stand ibaki Mbezi waonekane wana hoja. Maana hamna hoja ya maana mnazubgukazunguka tu.Kama unaweza kuwa na fremu za biashara na vituo vya mafuta kila mahali unaweza pia kuwa na stendi binafsi kila mahali.
Wanaopanda ndege ni walimu, wamachinga, bodaboda, wauza nyanya, mama ntilie na wamachingaWanaopanda ndege ni akina nani? Wewe una vichekesho sana.
Una vichekesho sana.Wanaopanda ndege ni walimu, wamachinga, bodaboda, wauza nyanya, mama ntilie na wamachinga
Kuna mtu anataka stendi ya Mbezi ihamishwe? Mimi naona watu wanataka stendi nyingine za ziada zaidi, sijaona mtu akisema stendi yenu pendwa ya Magufuli Mbezi ing'olewe ipelekwe kwingine.Nyie ndio mnaofanya wanaolazimisha stand ibaki Mbezi waonekane wana hoja. Maana hamna hoja ya maana mnazubgukazunguka tu.