Utakuwa unatumia mama sana, hongera mkuu.
Hatuwezi kuweka bus stands kila mahali, achilia mbali private bus stands, itakuwa danguro lisilo na kiongozi.
Kuna options mbili tu ili kurahisisha usafiri wa mabus ndani ya jiji.
1. Kujenga zonal bus stands, kuwe na zones tatu, moja ya Magufuli, nyingine Temeke na ya tatu Bunju. Kwa namna hiyo wenye mabus wataamua, mengine yaondokee Temeke kuelekea Kaskazini(Moshi, arusha, Manyara, Tanga nk), Nyanda za Juu(Mbeya, Ruvuma nk), Kanda ya ziwa(Mwanza nk)huku kukiwa na routes za kawaida kuelekea Mtwara nk.
Same scenario iwe kwa Mwagufuli na Bunju, hii itarqhisisha usafiri wa ndani na wananchi watapunguziwa mzigo.
2. Wenye mabus waamriwe kuwa na shuttle bus, Ratco anafanya hivyo mda sana, wakishushwa Magufuli wanapanda shuttle kuelekea Temeke na viunga vyake, Bagamoyo Road na maeneo yake, katikati ya jiji nk.
Ila huwezi kuruhusu kila basi kuwa na stand yake, huo ni upumbavu na kukosa dirt kama jiji. Tutembee kudogo mataifa yaliyoendelea tujifunze jamani, sio kwenda kushangaa magorofa na njia 18 za barabara.