ukiachana na hizo fungus na UTI na magonjwa ya zinaa,,, mshauri pia awe na utaratibu wa kujisafisha mara kwa mara kwa maji mengi na kubadili pichu walau mara mbili au tatu kwa siku ikiwezekana.... kwani wadada wenzangu kwenye vibegi vyenu hua mnawekaga nini maana mimi lazima niwe nazo za ziada hata mbili za kubadili
Hapo kwenye usafi ndio penyewe haswaaa ila sasa nadhani mtoa huduma wa kituo cha afya anapaswa amwambie kwa mpenzi ataona kama anamzingua tu,
-Asichangie vyombo vya chooni na pia awe ana kawaida ya kuvisafisha kila wiki,
-Aoshe Uke kwa Maji mengi bila sabuni, wengi hutumia sabuni tena zile medicated soap au za kunukia akiamini ndio anasafisha kumbe anajiharibu,
- Aingize kidole na kutoa uchafu wote wa juu juu hapa napo ni mtihani maana wengi huambiwa wasiingize kidole uke unajisafisha wenyewe, ni kweli lakini unatoa uchafu kutoka ndani na kuuacha kwenye kingo mchache unatoka hadi kwenye chupi sasa ukiulimbikiza ndio mwanzo wa kuzalisha bakteria wabaya na kuanza kuwashwa,
- Akimaliza kufanya mapenzi ajisafishe kwa maji mengi na ahakikishe shahawa zote zimetoka kwa kujikamua, kuacha shahawa ndio mwanzo wa kuzalisha bakteria wabaya na kutengeneza miwasho na fangasi,
-Abadili chupi walau mara mbili kwa siku, asishinde na chupi moja siku nzima
-Avae chupi aina ya Cotton na sio Materials zingine
-Akikojoa anawe kwa maji na kujikausha kwa tissue sio kutumia tissue pekee ndio mwanzo wa kufuga uvundo au maji pekee bila kujikausha unatengeneza unyevu,
- Asitie viungo kwenye uke kama vipipi, shabu, mnato wa kisomali, vitunguu saumu, mafuta ya miski, n.k
MUHIMU: Wakitaka kufanya Mapenzi waogeshane kwanza, haya mambo ya kuparamiana na mijasho na uvundo mwisho wake ni kuanzishiana thread [emoji23][emoji23][emoji23]