Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndg.Lissu atuwekee CCTV FOOTAGE ya yaliyotokea... pale nyumbani kwake anayo....Takukuru ipi ? Ya Nchi gani zaidi ya hii credit ya Leo? Perfect timing dunia yote ikisikia? Acha upumbavu.
Hapana, hapa ni Tanzania.Hii italeta tafrani kubwa sana
Ndg.Lissu atuwekee ushahidi wa CCTV FOOTAGE...
Humjui huyo,hongo ingekua inatosha asingesema.Humjui Lisu. Fuatilia maisha yake kama utasikia aliwahi hata kuhisiwa kula hongo.
Ya mama akeHuyu Mtoto anayetembea na Mabulungutu kayatoa wapi?!
""Yataleta Tafrani" wapi huko mkuu, 'Yoda"?Hii italeta tafrani kubwa sana
Unasahau vipi mama aliishi Dubai wiki kadhaa akiuza mali za Tanganyika?Huyu Mtoto anayetembea na Mabulungutu kayatoa wapi?!
Umebadilika sana. Sitashangaa iwapo ulisha tembelewa na Abdul!Tundu hakuhongwa na hakukuwa na fedha za kumhonga. Hizo ni drama tu. Tundu alivyo na shida ya hela kwa maisha anayoishi kwa kuunga unga huko Belgium asingeweza kukataa hela kama zingekuwapo.
Nitakuwa mtu wa mwisho kumuamini Lissu,huyu mnyampaa anaweza kufanya chochote kwa ajili ya popularity.Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.
Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.
Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.
Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.
Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.
Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.
Pia soma
TAKUKURU ipi? Hii au nyingine?hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
He who alleges must prove, ni fundamental principle ya evidence law..hata Abduli anaweza kutaja aliowahonga ili tuwazomee.
..tuhuma zote hizi kwanini Abduli hatafutwi ili aeleze upande wake?
..Abduli anatoa wapi viroba vya pesa za kuhonga wapinzani?
Mbona untaka kunitawala kimawazo niwe kama wewe? Uhuru wa maoni una maana gani kama wote tutakuwa na fokra moja?Umebadilika sana. Sitashangaa iwapo ulisha tembelewa na Abdul!
'Objectivity' niliyo dhani wakati mwingine, yote imeyeyushwa?
Unafikiri hatawataja? Anasubiri muda muafaka kufanya hivyo. Mtashangaa.Kwanini Tundu asitaje waliohongwa? You can't make an informed conclusion by pieces of information!! Ametuacha na maswali mengi kuliko majibu
TAKUKURU wamkamte Abdul aliyetumwa, acha utani.hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
Kama kweli anapinga rushwa na kaweza kumtaja upande mmoja ni kwanini amfiche wa Chadema? umechukizwa na jambo usitaje nusu nusu wataje tu maana hakuna siri tena.Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.