Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Humjui Lisu. Fuatilia maisha yake kama utasikia aliwahi hata kuhisiwa kula hongo.
Humjui huyo,hongo ingekua inatosha asingesema.
Kakataa dau dogo,na waliopeleka wakampotezea ndio maana anaropoka leo.
 
Hii italeta tafrani kubwa sana
""Yataleta Tafrani" wapi huko mkuu, 'Yoda"?

Mbona nchi hii siku hizi mambo ya aina hii hayamstuwi mtu tena?
Kwanza kuna watu wengi wanao mshangaa na kumdharau Tundu Lissu, kwa kutotumia fursa hiyo!

CCM imewafanya waTanzania watu wasio amini tena utu wa mtu, kwamba unanunuliwa tu wakati wowote na wenye uwezo na kumfanya mtu huyo chochote wapendacho kumfanyia.

Hii imekuwa 'disgrace' kubwa kwa nchi yetu. Hatuna hadhi tena. kama waTanzania.

Kama huelewi, huo mfano wa Abdul ndio mfano sahihi kabisa wanavyo wachukulia waTanzania sasa hivi. Kila mmoja wetu anayo bei inayomstahili.

Si unaona watu wanavyo pigana vibega kwenye hizi teuzi za kila wiki? Na mahali pa kushangilia ni hapa hapa JF. Tunaita "MKEKA", sijui maana yake ni nini!

"'Self esteem' tuliyo wahi kuwa nayo huko siku za nyuma, yote imefutwa na CCM.
 
Tundu hakuhongwa na hakukuwa na fedha za kumhonga. Hizo ni drama tu. Tundu alivyo na shida ya hela kwa maisha anayoishi kwa kuunga unga huko Belgium asingeweza kukataa hela kama zingekuwapo.
Umebadilika sana. Sitashangaa iwapo ulisha tembelewa na Abdul!
'Objectivity' niliyo dhani wakati mwingine, yote imeyeyushwa?
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Nitakuwa mtu wa mwisho kumuamini Lissu,huyu mnyampaa anaweza kufanya chochote kwa ajili ya popularity.
Huyo abdul ni mjinga kiasi gani kufanya jambo kizembe hivyo!
Kingine,Siasa sio mchezo wa WATOTO WADOGO.NA ndio maana sio Kila Raia ni Mwanasiasa.
Siasa ni uhuni wa kimafia,kila mbinu ni halal!
Jiulize wewe mwenyewe kwa nini walikufuata wewe na si Godbless kama Reputation yako haina UTATA!
Lissu ni Msaliti aliyekuwa irrelevant.
 
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
TAKUKURU ipi? Hii au nyingine?
 
Lissu Kama kamtaja Abdu kwanini asimtaje kiongozi wa chama chake. Dr. Slaa alitaka mafisadi wa ccm yeye kigugumizi Cha Nini.
 
..hata Abduli anaweza kutaja aliowahonga ili tuwazomee.

..tuhuma zote hizi kwanini Abduli hatafutwi ili aeleze upande wake?

..Abduli anatoa wapi viroba vya pesa za kuhonga wapinzani?
He who alleges must prove, ni fundamental principle ya evidence law
 
Umebadilika sana. Sitashangaa iwapo ulisha tembelewa na Abdul!
'Objectivity' niliyo dhani wakati mwingine, yote imeyeyushwa?
Mbona untaka kunitawala kimawazo niwe kama wewe? Uhuru wa maoni una maana gani kama wote tutakuwa na fokra moja?
 
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
TAKUKURU wamkamte Abdul aliyetumwa, acha utani.
 
Kama ulichoandika hapo ni cha kweli basi raisi anapaswa ajiuzulu na mwanae achunguzwe kwa kashifa ya rushwa
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Kama kweli anapinga rushwa na kaweza kumtaja upande mmoja ni kwanini amfiche wa Chadema? umechukizwa na jambo usitaje nusu nusu wataje tu maana hakuna siri tena.
 
Mfukuzeni basi Lissu kama mnaweza muone. Mbowe apumzike kwa heshina na Lissu aambiwe arudishe fomu ya makamu acnukue ya m/kiti. Makamu achukue Heche au Lema. Mnyika amesusa ukatibu kwa sababu Mbowe anafuja pesa za chama huku anaona, Mnyika ni smart hataki kusema tu. Mrema aondoke pale au kama anaweza agombee na yeye vyeo ndani ya chama vya kupigiwa kura. Mkimfukuza Lissu atawataja washenga wa Abdul ndani ya chama Kwa umma.. Na Sijui kwa nini hakumwambia Msigwa au CCM wamemkataza Msigwa kwa kuwa nae kapokea pesa zao?
 
Back
Top Bottom