Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Pre GE2025 Tundu Lissu: Abdul (mtoto wa Rais Samia) alitaka tukutane kwenye hoteli moja Masaki anihonge, nikamwambia njoo kwangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu Mtoto anayetembea na Mabulungutu kayatoa wapi?!
Wewe umesikiliza upande mmoja na unatoa hukumu. Lissu ni mwana siasa na kama kweli angweza kuweka mtego zaidi ya huu sababu alikuwa anajuwa kitakachotokea hakuweza hata ku record maongezi maana huwezi kumshutumu mtu tu kwa kauli ukija kupelekwa mahakamani ok thibitisha? Kwanini akatae kumtaja wa Chadema, wewe ukiona mpaka watu wanakuja na mtu wa chama chako kutaka kukuhonga basi ujuwe wanajuwa udhaifu wako kuwa umeshawahi kupokea.
 
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
LISSU kamsamehe huyo dogo sasa nawe nakushauri mwambie huyo dogo aende mahakamani kwa kuchafuliwa usimpangie LISSU cha kufanya akikosewa, mbona amewasamehe waliotaka kumtoa roho sembuse kumpa rushwa?
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Mshana Jr umeumbuka
 
Sina uhakika kama hizi tuhuma ni za ukweli na kama ni kweli kuna ulazima sasa kila mtu kwa imani yake kuliombea taifa letu na si kuleta ushabiki na mizaha.
 
Kweli rushwa za wakubwa zinapwlekwa nyumbani, tena ktk US Dollar Cash Money
 
Wewe umesikiliza upande mmoja na unatoa hukumu. Lissu ni mwana siasa na kama kweli angweza kuweka mtego zaidi ya huu sababu alikuwa anajuwa kitakachotokea hakuweza hata ku record maongezi maana huwezi kumshutumu mtu tu kwa kauli ukija kupelekwa mahakamani ok thibitisha? Kwanini akatae kumtaja wa Chadema, wewe ukiona mpaka watu wanakuja na mtu wa chama chako kutaka kukuhonga basi ujuwe wanajuwa udhaifu wako kuwa umeshawahi kupokea.
Hahahahaha, na huyo wa chama chake walioenda nae kwa lisu itakua ni mtu anayemmudu Lisu ,ama aliwahi kufanya nae ishu km hy...mtu na mtuwe..wakaenda na mtue
 
hongo huwa inasababu, daktari akjtibu, hakimu ushinde kesi, polisi uachiwe sasa yeye wamhonge kwa lipi? kama aliona ni hongo nayeye ni wakili kwanini hakutoa taarifa takukuru?
Mbona swali lako ni la kipuuzi sana kama hauna kichwa aisee!?
 
Bhc atakua mnafiki kwann asimtaje na wa chama chake tujue ni kweli?
Alaf kama alikua hazitaki kwann amuambie amletee kwake?
Siasa mchezo mchafu
Wewe acha upumbavu.
Appointment ilikuwa wakutane waongee jambo si appointment ya kupeana pesa ingawa alishaambiwa na mtu wa CHADEMA kuwa ni mshiko unakwenda kutoka.
Sasa angekataa appointment angemchana wapi kuwa hataki pesa chafu?
Lissu si kiongozi mkuu wa chama so akisema kuwa kuna kiongozi ndiye alikuwa mtu kati ni kweli kabisa labda ni chairman wake au kiongozi mwingine wa juu ndani chama chake hivyo anaweza kumweka kikaangoni mbele ya CHAIRMAN.
Huyo kiongozi bila shaka ni yule aliyehamia CCM juzi
 
Tundu hakuhongwa na hakukuwa na fedha za kumhonga. Hizo ni drama tu. Tundu alivyo na shida ya hela kwa maisha anayoishi kwa kuunga unga huko Belgium asingeweza kukataa hela kama zingekuwapo.
Ulikuwa beki tatu wake nini huko Ubelgiji? Hapo hata chai hujanywa unasema Lissu aliishi kwa kuunga unga 😃
 
Mfukuzeni basi Lissu kama mnaweza muone. Mbowe apumzike kwa heshina na Lissu aambiwe arudishe fomu ya makamu acnukue ya m/kiti. Makamu achukue Heche au Lema. Mnyika amesusa ukatibu kwa sababu Mbowe anafuja pesa za chama huku anaona, Mnyika ni smart hataki kusema tu. Mrema aondoke pale au kama anaweza agombee na yeye vyeo ndani ya chama vya kupigiwa kura. Mkimfukuza Lissu atawataja washenga wa Abdul ndani ya chama Kwa umma.. Na Sijui kwa nini hakumwambia Msigwa au CCM wamemkataza Msigwa kwa kuwa nae kapokea pesa zao?
Rubbish! Kweli chadema chama kubwa. Mnabwabwaja all day and night. Na wala hakuna mtu wa Chadema anabwabwaja kuhusu CCM! Jitafakari
 
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akizungumza kwenye kipindi cha Medani za Siasa, Star TV, leo Agosti 17, 2024, amesema Mtoto wa Rais Samia aliyemtaja kwa jina la Abdul alitaka kumhonga pesa Novemba 2023.

Tundu Lissu amesema Abdul hakutaja kiwango cha pesa, na alitaka aende usiku kwenye mojawapo ya hoteli zilizopo Masaki ili apatiwe pesa hizo lakini alikataa, akasema aje nyumbani kwake Tegeta. Lissu amesema Abdul alitumia watu wa chama chake kumfikishia ujumbe huo.

Amefafanua zaidi kuwa kijana huyo alikuja nyumbani kwake, na baada ya kutaka kumpa pesa alizikataa akasema anataka kupewa pesa zenye risiti, siyo hizo za gizani. Kwenye mazungumzo hayo walikuwepo watu wanne, na walinzi wa Abdul wakiwepo nje ya nyumba yake.

Kwa mujibu wake, yeye alizikataa pesa hizo na kumwambia aende akamwambie Rais amlipe stahiki zake kwa mujibu wa sheria na siyo kumhonga, na alimpatia nyaraka zote zinazohusiana na madai yake.

Baada ya hapo hawakuwahi tena kuwasiliana.

Lissu amekataa kumtaja kiongozi wa CHADEMA aliyeambatana na Abdul.

Pia soma
Most likely huyo kiongozi wa CHADEMA anaweza kuwa Msigw.

Kwa kuwa, hamtaji na kwa ,kuwa Lissu aliwahi kusema CHADEMA siyo mama yake na ukisikiliza maneno ya Nchimbi kuhusu Lissu basi iko siku Lissu atahama hasa ikiwa atashindwa uchaguzi mafasi ya makamu mwenyekiti na pia ikiwa atashindwa kuteuliwq kuwa,mgombea urais 2025.

Usimuamini mwanasiasa mithili ya dini
 
Kama huu ugawaji wa fedha ni kweli, hela hizo ni Kodi kwa ajili ya maendeleo ya Nchi. Hivyo ni muda sasa Watanzania kuungana kuhoji suala hili. Je kuna biashara gani kwenye Uongozi wa Nchi yetu? Huu Uongozi wa kununua ni kwa maslahi ya nani?
 
Najiuliza maswali, kama Lissu alijua nia ilikuwa kumuhonga, lakini alitakiwa aende hotelini, kwa nini asingekataa moja kwa moja, lakini akatoa plan B ya kufuatwa nyumbani? Mwenye nia ya kupambana na rushwa angekataa moja kwa moja, iwe nyumbani au hotelini. Au aliomba dau kubwa, lilipogoma akaona awahi mapema kusema kabla upande wa pili haujasema? Hao akina Abdul hawakuwa na vinasa sauti au kamera za siri?

Lissu anasema hotelini angepigwa picha....!!!! Alitaka apewe sehemu ya gizani, au kificho ndio maana akachagua nyumbani?

Ndani ya CDM kuna watu wana access na uongozi wa kitaifa, na huwa wanawaunga na viongozi wa CCM ili wapate fedha? Ni akina nani hao? Wangapi mpaka wako chadema, na ni viongozi wa kitaifa na wameshapewa?

Ndio mnataka tuandamane?
 
Back
Top Bottom