Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa wanafanywaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.

Kwani ni kweli Lissu alikuwa msaliti katika mapambano ya serikali kuhusu Rasilimali zake na wakoloni?

Maana kweli ninachojua! Nchi yoyote huwa iko kinyume kabisa na wasaliti na huwa wanapelekewa moto kweli!
 
Duh

Kwani Yeye Tundu Lisu alikuwa anapinga nchi?
alikuwa anapinga UKANYABOYA wa Magufuli ambao KABUDI kaudhibitisha
1664915659087.jpg
 
Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa tunafanyaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.
Huyo Tundu Lissu, ninachomsifu huwa haogopi kutamka lolote!

Kama ni nyeupe atasema ni nyeupe. Full Stop
 
Back
Top Bottom