Uchaguzi 2020 Tundu Lissu afanya mdahalo na Waandishi wa habari atoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali. Apangua hoja ya kutumika na mabeberu

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu afanya mdahalo na Waandishi wa habari atoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali. Apangua hoja ya kutumika na mabeberu

Sasa hapo ndipo ninapotofautiana na Lissu. Ubeberu ni real, na asitufanye kwamba hatuoni uhuni wa mashirika makubwa ya kibeberu yanayojikita katika nchi maskini yakitake advantage ya mifumo mibovu ya usimamizi wa raslimali ya serikali za nchi maskini.

Pili, kauli za style ya Lissu anayeizungumzia nchi yake kama isiyojiweza na inayetegemea serikali za magharibi ili tuishi ni kauli za kipumbavu mtu yeyote huru na anayejiamini na anayoipenda nchi yake hawezi kuiunga mkono. Kwamba sisi hatuwezi kujitegemea? Huku kujidharau abaki nako yeye, sisi tunaweza na tunajiweza inferiority complex aliyo nayo yeye ni yake mwenyewe.
Huyu angekuwa kiongozi wa nchi kipindi kile cha corona,tungeisoma namba,anaonyesha hawezi kuwa na maamuzi bila backup kutoka nchi za wazungu.huyu hafai hata kidogo.nasikitika tu ndoto yake haitaweza kutimia.
 
Dunia ni kijiji mkuu nchi zinategemeana ndio maana viongozi wako wengi huenda kutibiwa Apolo India hata Dreamliner haikutengenezwa Chato Geita imetoka kwa mabeberu.
Hivi una habari kuwa mpaka inafika 2018, asilimia zaidi ya sabini ya kalamu za kuandikia huko Canada zilikuwa zinatoka nchini China? Hapo sijazungumzia upande wa Marekani. Lakini je hali hiyo inaiondolea Canada uhuru wake na kujitegemea!? Bahati mbaya sitashangaa ukisema usiilinganishe Canada na Tanzania..!!!!
 
"Tofauti ya Mrema, Slaa na Lowassa ni 'organization' wakati wa nyuma hakukuwa na 'organization' ila sasa tunayo, tunaweza kuweka mawakala nchi nzima"- @TunduALissu

#“Kutakua na Uhuru kamili wa vyombo vya Habari, katiba yetu haina neno ISIPOKUA, kutakua na Uhuru wa maoni, kutakua na Uhuru wa kutafuta habari, kumekua na ukiukwaji mkubwa wa Uhuru wa Habari, miaka mitano ya Magufuli imekua migumu kwa vyombo vya Habari”.@TunduALissu #Mwanza.

“Kumbe wakati mwingine polisi wanafanya kazi zao kwa weledi lkn wanakuwa victimized wanapokataa maagizo toka juu”. Tundu Lissu.

"Kuna vitu havihitaji utoe pesa ili upate pesa, kuna sehemu unahitaji akili tu"- @TunduALissu.

"Serikali yangu itakuwa na 'complete freedom' ili ku-stimulate uchumi mzima, ukishusha vifaa vya ujenzi watu wataweza kujenga nyumba zilizo bora"- Lissu.
===

Katika Mdahalo huo waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wameuliza maswali mbalimbali ikiwamo namna gani atakavyouondoa ukoloni mambo leo? Umuhimu wa watu wengi kujaa kwenye mikutano, na auala la yeye kutumika na mabeberu.

Aidha alipoulizwa kuhusu serikali yake itapambana vipi kuundoa ukoloni mamboleo Lissu amefafanua kuwa suala la ukoloni mambo leo ni dhana iliyokuwa inabebwa zaidi na viongozi ambao walikuwa wanatawala kwa kufuata mfumo wa kijamaa ila kwa wakati huu dhana hii haipo tena maana hawa tunaowaita wakoloni mambo leo ndio ambao wamekuwa wakitusaidia na tukiwategemea katika kufadhili miradi mbalimbali.

Ameongeza kuwa hao tunaowaita mabeberu ndio wanatusaidia katika kila kitu hata katika vyombo vya usalama kama Polisi n.k. Pia wanatusaidia katika usafiri kama wa ndege na helikopta na wanatusaidia katika kutoa hela za miradi mikubwa mikubwa. Ameeleza kuwa ikitokea watu hao wametuzuia kidogo tu, tumekwisha. Hivyo amesisitiza kuwa watu waache kudanganyika na neno mabeberu na ukoloni mambo leo tutengeneze mahusiano mema na Dunia, kwa sababu dunia haitutegemei sisi isipokuwa sisi tunaitegemea dunia.

Sambamba na hilo, Tundu Lissu ameeleza nchi hii imeharibu uhusiano na nchi nyingine ndani ya miaka mitano iliyopita. Hivyo, wakipata ridhaa ya kuiongoza nchi watahakikisha wanajenga mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuleta maendeleo nchini.

Aidha, akijibu swali kwamba serikali yake itapata wapi pesa za fidia kuwalipa wakazi waliobomolewa nyumba zao, Tundu Lissu amefafanua kuwa kwa sheria ya nchi inasema kuwa pale serikali inapokosea au kubomoa nyumba za watu kimakosa inweza kushitakiwa na kulipa fidia. Hivyo, ukikosewa kwa namna yoyote ile na serikali unastahili kulipwa fidia. Hivyo, kwa namna yoyote Tundu Lissu amesema wakipata nafasi ya kuingia madarakani watatafuta namna ya kuwalipa fidia. Amesisitiza kuwa japo itakuwa bili kubwa ya kulipa fidia lakini itawalazimu watafute pesa hiyo ya kulipa watu fidia.

Aidha, kuhusu suala la watu kujaa kwenye mikutano, Lissu anasema kuwa katika siasa mtaji ni watu, ili kubaini kuwa Mwanasiasa ana nguvu kiasi gani kisiasa lazima uangalie anaungwa na watu kiasi gani. Ameweka bayana kuwa Chadema ya mwaka huu imejipanga zaidi na wana matawi mengi na kutengeneza Organization ya Chama inaitwa Chadema ni Mshindi.

Ama kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, Tundu Lissu amesema kuwa serikali ya Chadema itavipa uhuru vyombo vyote vya habari na wataondoa vikwazo vyote mamlaka kama TCRA zitatumika kusajili tu vyombo na sio kuingilia maudhui yao.
Kama anasema atafanya mahusiano na nchi zingine ili kuleta maendeleo kweni sasa hatuna maendeleo kwenye utawala wa JPM?

Huyu ni muhaini tu na mpenda madaraka kwa sifa, MUNGU hawezi kumfanya kua Rais hata siku moja
 
Sasa hapo ndipo ninapotofautiana na Lissu. Ubeberu ni real, na asitufanye kwamba hatuoni uhuni wa mashirika makubwa ya kibeberu yanayojikita katika nchi maskini yakitake advantage ya mifumo mibovu ya usimamizi wa raslimali ya serikali za nchi maskini.

Pili, kauli za style ya Lissu anayeizungumzia nchi yake kama isiyojiweza na inayetegemea serikali za magharibi ili tuishi ni kauli za kipumbavu mtu yeyote huru na anayejiamini na anayoipenda nchi yake hawezi kuiunga mkono. Kwamba sisi hatuwezi kujitegemea? Huku kujidharau abaki nako yeye, sisi tunaweza na tunajiweza inferiority complex aliyo nayo yeye ni yake mwenyewe.

Una Samsung/Iphone ya mabeberu, Server inayokuwezesha kupost ipo Marekani halafu mdomo mrefuuu unajitegemea.
 
Pumba tupu! Mpaka leo hajui kama nchi nyingi Afrika tulipewa uhuru wa kisiasa na kijamii na sio wa kiuchumi! MWAMBIENI HUYO MGONJWA WENU KUNA VITU VYA BURE LAKINI SIO PESA.HATA UKIKUBALI USHOGA UKAPEWA HIZO PESA JUA TAYARI BIASHARA UMEKWISHA IFANYA NA VITA YA SASA INAYOPIGANA DUNIA NI VITA VYA KIUCHUMI( hakuna pesa za bure).
Halafu eti ni mgombea wa urais!!🤣🤣🤣🤣 TL uraisi ni kiatu cha wakubwa hakuna ataethubutu kukuvisha wewe. JPM NEXT LEVEL.

MAGUFULI4LIFE.
 
Wewe ni mnufaika binafsi wa uwepo wa Magufuli, hujali shida wanazopata wananchi maskini wàsiojua kesho watakula nini. Nyie endeleeni kusifia uwanja wa ndege Chato kwa sababu ukienda likizo toka hapo Wizara ya Mambo ya nje ulipopachikwa na baba yako unapanda ndege kwa amri ya baba yako.
Huo Uwanja utatumika tu na baba na wanawe waliopachikwa akiwa madarakani tu baada ya kustaafu/kustaafishwa hakuna ndege itatua au kuruka hapo litabaki gofu kama lile la Mobutu. Museveni hata Kenyatta wanaotumia Uwanja huo kuja kumwona baba hawatakuja tena hata kama watakuwa bado wako madarakani maana baba atakuwa mchungaji wa ng'ombe. Miaka 50 ijayo wakati Burigi National Park itakuwa na Wanyama wengi kuifanya kivutio kwa watalii, Uwanja wa kimataifa utakuwa machungio ya mifugo ya wajukuu wa baba Rais mstaafu akiwa mita mbili ardhini. Wajao watajiuliza: "Nchi nzima hakukuwa na wenye akili?"
 
Yeye mwenyewe Lissu hana uhuru kwa wazungu waliomtuma wamemfanya kama panya wa maabara wamemfunga devices mwili mzima asije akawatoroka na madeni baada ya kukosa urais aliowaahidi kwamba atapata wakati anajua wazi kwamba anaonhea usanii mtupu na sio sera ya chama chake, ni kichaa peke yake atakayempigia kura Lissu
Ungejua Pacemaker ni nini na ya nini na nani anayo usingeandika ujinga unaothibitisha ujinga wako. Pacemaker haitengenezwi Chato!
 
Sasa hapo ndipo ninapotofautiana na Lissu. Ubeberu ni real, na asitufanye kwamba hatuoni uhuni wa mashirika makubwa ya kibeberu yanayojikita katika nchi maskini yakitake advantage ya mifumo mibovu ya usimamizi wa raslimali ya serikali za nchi maskini.

Pili, kauli za style ya Lissu anayeizungumzia nchi yake kama isiyojiweza na inayetegemea serikali za magharibi ili tuishi ni kauli za kipumbavu mtu yeyote huru na anayejiamini na anayoipenda nchi yake hawezi kuiunga mkono. Kwamba sisi hatuwezi kujitegemea? Huku kujidharau abaki nako yeye, sisi tunaweza na tunajiweza inferiority complex aliyo nayo yeye ni yake mwenyewe.
Ubeberu aliukaribisha Lissu ?!. Mmeambiwa tangu Mkapa (RIP) akiwa hai. Nani walioingia mikataba ya kishenzi inayoiumiza nchi ?! Ni Lissu ?.

Wafuasi wa Ccm na watawala mmetiwa upofu wa kutaka kurusha lawama hata kwa mambo yalioanzia ndani mwenu .
 
Jamaa anajenga hoja, lkn kwenye ubeberu hajajibu vizuri
Ninyi mbuzi wa lumumba ndo mnahitaji mabeberu ndo maana mnajua jibu zuri kuhusu mabeberu lakini ingefaa zaidi kama ungewashauri waandishi wa Habari waende Dodoma wakamhoji mwenzenu mpate jibu halisi. Neno beberu lilitumika sana wakati TANU inatafuta Uhuru lakini liliachwa kabisa baada ya kupata Uhuru limekuja kuibuliwa tena upya na nguvu zaidi na Awamu ya Tano kwa sababu hawana jipya. Hata matumizi ya wasanii kwenye mikutano ya kisiasa lumumba wamefufua baada ya TANU kuwapumzisha sasanii wakina Makongoro baada ya Uhuru pamoja na zile nyimbo za kisiasa CCM wamezirudisha maana hawana mapya. Mapinduzi ya Chama cha Mapinduzi ndo hayo tunaendelea nyuma!
 
Ubeberu aliukaribisha Lissu ?!. Mmeambiwa tangu Mkapa (RIP) akiwa hai. Nani walioingia mikataba ya kishenzi inayoiumiza nchi ?! Ni Lissu ?.

Wafuasi wa Ccm na watawala mmetiwa upofu wa kutaka kurusha lawama hata kwa mambo yalioanzia ndani mwenu .
Ningekuwa beberu, baada ya miaka takriban 30 ya utajiri wa kuvuna mali za watanzania, ningefanya kila ninachoweza kuwasaidia walioniruhusu waendelee kuwepo. Nina uzoefu nao, wamenisainia mikataba inayoninufaisha, wametunga sheria kuifanya siri na wameendelea kuulinda mshikamano wetu kila ulipokuwa questioned. Kwa nini nihatarishe huu urafiki, miongo mitatu ya neema na uzoefu niliojijengea jinsi ya kula na kipofu huyu, na badala yake niruhusu aje shetani nisiyemjua? Shetani ambaye ameonyesha historia ya kutokuwa upande wangu?

Hata kama ni propaganda, iwe na mantiki.
 
Niyeye Lissu ni Rais wetu wa awamu ya6
✌🏽✌🏽✌🏽✌🏽✌🏽💪🏽💪🏽💪🏽💪🏽💪🏽
 
Tundu Lissu ana akili sana. Natamani niwe namsikiliza saa zoote. Hakika nanufaika sana kumsikiliza huyu Mheshimiwa. Narudia rudia tu kusikiliza hata maongezi yake ya kipindi cha nyuma, sichoki.
 
You can’t prove your accusation to the government nor my selfish interests as you claim to be in defending the government. In other words that’s just your opinion.

Hakuna bylaws zinazo lalamikiwa walau huko ndio watu wanaweza jiamulia kwenye kutunga kanuni.

Lakini sheria zote kabla azijafika bungeni zina stages zake ambazo reps wa wadau watakaoguswa wanashirikishwa kujadili na kutoa mapendekezo, kamati ya bunge inajadili na kuhoji concern za sheria na ndio sheria inaenda jadiliwa bungeni; stages zote hizo kuna amendments.

Sasa leta ushahidi ni sheria gani iliyopita bungeni without the due processes?

Interest of the party not you personally. Rest of what you wrote, you miss me with that, it's an insult on both our intelligence. Sheria zinapita kwa hati ya dharura kitu ambacho sijawahi kuona kabla ya awamu hii, kwa kuungwa mkono na asilimia 100 ya chama (Kati ya mamia ya wabunge hakuna hata 1 anayewaza tofauti ) halafu ndani ya mwaka inabadilishwa pengine kwa presha ya wahisani. Kama sio failure ya chama kufanya kazi yake, acquiescing to the whims of one one man, ina maana hawa wabunge hawakuona hayo mapungufu hadi mhisani akawaonyesha? Hiding behind empty rhetoric of due process is played out, Nyerere alishtakiwa kwa uchochezi, Mandela alifungwa, huku due process ikifuatwa. Hata hivyo, taratibu zisipofuatwa kwenye procurement za serikali haya mahaba ya kufuata taratibu yanaendaga wapi?
I know you are smarter than you present, it's only fair you accord your readers' intelligence the same level of respect.
 
Aisee . . . . ngoja nipite kwanza
 
Back
Top Bottom