Tundu Lissu afanya misa ya shukrani Ikungi, Singida. Aahidi kutompitisha mtu kwenye maumivu aliyopitia

Tundu Lissu afanya misa ya shukrani Ikungi, Singida. Aahidi kutompitisha mtu kwenye maumivu aliyopitia

Majinga sana.Hivi kumuita mtu msaliti ni kwamba mlikuwa mna mawazo yanayoelekeana au the same missions to accomplish.Sasa lini Lissu aliwahi kuwa pamoja na vibaka wa CCM?Unamuitaje mtu kuwa amekusaliti wakati hamjawahi kufanana kimsimamo,kichama,kimuono hata maisha tu?The bunch of "green flies" is a catastrophe to the nation itself![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tuombe Mungu sana ili jambo letu litimie ifikapo 28.10.2020 la tokomeza ccm
 
Wewe umewacha lini?
Angalia kwanza jina analotumia.NAWATAFUNA.Ina maana anameza vitu au vitu huingia ndio anavitafuna na kuvimeza.Maana yangu:Kuna kinachoingia na kinachoingiziwa/kiingizwa!Ndiyo umuelewe ni kiingiziwa anatafuna/anameza.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ana haki ya kumshukuru Mungu kwa kweli.

Wapo waliotaka afe lakini Mungu akabatilisha makusudi ya waovu waliyoyafanya kwa Siri.

Kwa kushindwa kumuua Tundu Lisu ni kiashiria kuwa baadhi ya watu ni failure by nature, hawana nguvu ya Mungu ndani yao.
Amina
 
Najiuliza , walio ratibu na wale waliobeba bunduki na kumpiga lissu wanajisikiaje muda huu..

Maana nijuavyo roho ya binadamu huongea sana pale inapo jutia kukosea.

Kupanga kumwua binadamu mwenzio sio kitu kidogo..

Labda kama hao nao walisha uawa..
IMG-20200810-WA0002.jpeg
 
Angalia kwanza jina analotumia.NAWATAFUNA.Ina maana anameza vitu au vitu huingia ndio anavitafuna na kuvimeza.Maana yangu:Kuna kinachoingia na kinachoingiziwa/kiingizwa!Ndiyo umuelewe ni kiingiziwa anatafuna/anameza.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nimekusoma kiongozi, hatusumbui tena maana tushajua shughuli zake tayari
 
View attachment 1532875View attachment 1532878

Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeo (Chadema), Tundu Antiphas Lissu, leo Jumatatu, Agosti 10, 2020 amefanya Misa ya Shukrani kwenye kanisa la Mtakatifu Rita wa Kashia lililopo Ikungi, jimboni kwake Singida Mashariki.

Kwenye Misa hiyo iliyoongozwa na Paroko Laurent Bahale, Mheshimiwa Lissu amewashukuru Watanzania kwa kumuombea alipokuwa mgonjwa mpaka sasa alipopona kabisa.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru Watanzania wote kwa dini zao kwa kuniombea wakati nilipokuwa mahututi, nilipopata nafuu mpaka nilipopona kabisa"

“Mungu wetu ni wa ajabu. Amesikia sala zenu na leo nipo nanyi mzima wa afya tayari kutekeleza kazi iliyosalia. Niliumizwa sana ndugu zangu. Wiki mbili za mwanzo baada ya kushambuliwa nilipata maumivu makali ambayo sikuwahi kuhadithiwa. Mwili ulikuwa unawaka moto. Naahidi sitampitisha mtu yeyote kwenye maumivu yale niliyoyapata hata kama atakuwa amenikosea kwa kiwango gani” alisema Mheshimiwa Lissu

Kwenye Misa hiyo, mheshimiwa Lissu aliongozana na mgombea mwenza, Mheshimiwa Salum Mwalim ambao juzi Jumamosi, Agosti 8 walichukua fomu ya kugombea Urais kupitia Chadema.

Imetolewa leo Jumatatu, Agosti 10, 2020
View attachment 1532999View attachment 1532998
Asante kwa ujumbe murua, haki ita tendeka tu wananchi wanajua ukweli sasa na akina nani wanahusika.
 
Uzi kama huu kwa watu wengine ni sawa na kuwanywesha sumu.

Wanakuwa very uncomfortable wanapoona uzi kama huu kwani mchawi anapozungumzwa hutamani ardhi ipasuke aingiemo.

Hili swala litawatesa mno hawa wanaojiita wasiojulikana sambamba na waliokuwa wakiwatumia kwa maisha yao yote.

Kwani tunasikia spika aliamurishwa mauaji yakishakamilika mhanga akazikwe haraka kama mzoga.

Sasa wewe mtu hujui wewe kifo chako kitakuja kwa style gani halafu unaagiza wengine wauwawe na baadaye eti unaenda kanisani kusali. Hiyo ni kejeli kubwa sana kwa Mungu. Bogus kabisa.
 
Mabenchi matupu. Mpaka watu wa chache kijijini kwao wamemkataa.
 
Ni kauli ya Tundu Lissu leo 10.08.2020 baada ya kushiriki Misa ya shukrani, Kanisani Ikungi, Singida.
August 10 2020
Ikungi, Singida
Tanzania

IBADA YA SHUKURANI IKUNGI SINGIDA



Source : CHADEMA MEDIA TV
 
Back
Top Bottom