Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ahusisha kauli ya Rais Magufuli na kupigwa kwake risasi

Kwahiyo ni kweli alishambuliwa na hao wanaojiita wako kwenye vita ya Uchumi sasa mbona hawakumilisha huo upelezi kuwa ameshambuliwa sababu alikuwa anakwamisha vita ya Uchumi kama wanavotangaza kuuwa majambazi

Mkuu hayo yakusahambuliwa hatuna uhakika nayo kama ameshambuliwa na hao wewe unao wadhani lakini uhakika tulio nao ni Tundu Lissu kukiri kuwa yeye ndio alikuwa ana tusaliti na alikuwa ana wasiliana na mabeberu kutuhujumu...... Tunamshukuru Tundu Lissu
 
Hili jambo ni zito sana na tusipoacha unafiki na kulitatua kwa uwazi litaendelea kutusumbua sana.

Kosa baya sana lilifanyika na badala ya waliolitenda kurudi nyuma na kujitathmini, wanatafuta shortcuts za kuficha sura zao.

Huyo Mwanyika atakuwa ameingizwa kwenye siasa kwa shinikizo, labda aje kumchafua Lissu.

Kwa hiyo Lissu amekiri yeye ni msaliti na ndio alikuwa ana wasiliana na mabeberu kusaliti nchi?
 
Lissu hajawahi kuwa mnafiki anachukiwa sababu anapenda kusema ukweli ndiyo sababu anachukiwa wanafiki wa nchi hii. Hivi leo Deo Mwanyika wa kupitishwa kugombea ubunge. Tuhuma zake hazilingani hata na asilimia 1 ya tuhuma za Lissu

Mkuu Lissu amesema ni yeye ndio alikuwa analisaliti taifa ....
 
Tatizo taratibu zipo lakini hutaki kuzirejea, matibabu ya nje ya nchi yana taratibu zake mbona hapo unakwepa kueleza? Kama unajiamulia kuondoka nchini kwenda kutibiwa nje ya nchi bila kufuata taratibu, gharamikia matibabu mwenyewe usitafute watu wa kulaumu kwa kulazimisha utaratibu usiokuwepo

Kutibiwa sio issue tena hapa. Tunajadili ushahidi aliotoa Lisu. Kauli ya mkulu ni kumiminiwa Risasi
 
Sasa analalamika nini kama yeye siyo aliyekuwa anaisaliti nchi kwanini ahusishe shambulio lake na maneno ya rais juu ya mtu anaesaliti nchi?
Analalamikia kupigwa risasi 16 na hakuna hatua yoyote ile iliyochukuliwa
 
Sijawahi kusikia serikali yenye wahalifu wapumbavu kama Tanzania. Inawezekana Magufuli alikuwa hajui kinachpkwenda kutokea, lakini wahuni wakachomeka kwenye hotuba yake ili aonekane alikuwa anajua shambulizi lile na hivi hata yeye uwezo wa kuchuja maneno ni below 0, basi akalipuka nalo.
Hakuna litakalofichika yote tatajulikana hatimaye.
 
Si amesema alipigwa baada ya kuwa anasaliti nchi?

Ni upotevu wa rasimali kujaribu kuwakamata waliotaka kumuua msaliti wa nchi
Haya ila linaloenda kutokea kila mtu atalia na msiba wake
 
Tundu lissu anajifanya ana akili kuzidi wote ndiyo maana alimtukana hadi founder wa taifa letu kitu ambacho kwa wazungu wanaomtumia kwao angekuwa ameshakula shaba hata kufa
 
Basi Lisu hafai! Lkini pia deo mwanyika huenda alikuwa anatumika kuwanasa wasaliti aina ya Lisu

Hizo ni propanda tu hakuna ukweli wowote kwakuwa Deo Mwanyika alitengenezewa tuhuma nzito lengo lilikuwa ahusishwe na Lissu ili kuaminisha umma. Uwongo huwa haudumu
 
Watu tunaoaminishwa na Jeshi letu la Polisi kuwa ni "watu msiojulikana" mmeanza kujitokeza hadharani na kujitambulisha rasmi kuwa nyiye ndiyo WATU MNAOJULIKANA kwa Jeshi letu la Polisi!
Unakosea sana mkuu. Hakuna mtanzania mwenye roho mbaya kama Lissu ila Watanzania tunamvumilia na hata serikali na vyombo vyake vinavumilia matusi, hivyo hatujahusika wala serikali haina mpango, ila kwa sababu hii ni vita ya maslahi, wazungu walishaazimia lazima tena huyu mropokaji wenu watamtumia kujaribu tena kutupa kete yao ya kuvuruga Tanzania ili wajitwalie rasilimali zetu, walishindwa Mtwara sasa wamekuja na njia mbili, ya kwanza ni kufadhili waislam magaidi huko kibiti (tuliwashinda).

wakawahamishia Msumbiji nako tumeanza kuwasubiri wakinusa tu pua kipigo, kete ya pili ni Lissu, watamtumia wakiona hana uwezekano wa kushinda watamuua, au ikiwa ngumu kumuua basi watampatia hela ili aendeshe maandamano makubwaa na miongoni mwa waandamanaji kutakuwa na watu wenye silaha watawapiga risasi raia ili isemekane serikali inaua watu. Hivyo mjiandae kisaikolojia na huyo kibaraka wetu.
 
Kwqhiyo Lisu akatoboa siri kwamba akikuwa anasaliti taifa?
Huyo jamaa mjinga sana kumbe

Alikuwa anamtuhumu kumchafua tu kama ni kweli na ndiye anayeongoza nchi si angemshitaki na ushahidi alikuwa nao hadi Simu zake amezidukua kwanini asimshitaki. Una vyombo vyote vya dola halafu unamtuhumu mtu kwa maneno tu kuwa msaliti Kwani usaliti siyo kosa la jinai
 
Back
Top Bottom