Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Kwa hicho anacho kisema hapo maana yake kuwa kweli ndio yeye, kwanini aihusishe kauli ya usaliti kuwa inamgusa?Swali langu kwa Tundu Lisu, je yeye ndio alikuwa anawasiliana na hao mabeberu kuwapa taarifa nyeti alizoiba toka selikalini na kuisaliti nchi..?
Kama jibu ni ndio, kama kweli alikuwa anafanya hivyo basi hastaili kuishi kabisa.
Alafu wakati kauli hii inatoka ndio kipindi kile wale magaidi wa kibiti walikuwa wakifanya mauaji kila kukicha na huyu Lissu nae alikuwa ni mtu wa matamko kila siku mara kupinga tume ya uchunguzi wa madini (akii ni Rubbish) mara kupinga njia inayo tumika kupambana na magaidi wa kibiti (wanauawa hawakamatwi).
Hapo ukifikiri sana utakuja kuona kwamba yawezekana Kuna watu walienda kumpiga risasi Lissu kwa makusudi kabisa ili kuchonganisha wananchi na serikali yao kutokana na matamko yaliyokuwa yanatolewa na mienendo ya huyu Lissu mwenyewe kwa wahalifu makini lazima tu wangelichukulia hilo kama advantage kwao kupenyeza wanachokihitaji.
Hata sasa bado nina wasiwasi sana na usalama wa huyu mtu mana wenye nia ovu bado wapo na kwa hali ilivyo sasa wakimfanyia kitendo chochote kibaya basi watafanikiwa kuvuruga kabisa amani na utulivu vyombo vya usalama viwe makini sana kumlinda huyu mtu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, wakizubaa tu kidogo watu wata take advantage kwa huyu jamaa.